Nataka kusoma lakini wazazi wangu hawana uwezo wa kunisomesha

Upo sahihi ila note that college zina kitu knachoitwa fees na hata hzo library pia na huwezi kwenda kusoma cku 1 au 2
angalia una uwezo gani au kipaji gani, then unajisomesha kutokana na kipaji chako, mfano biashara vipo vitabu ving vya biashara, na fanya hivi huku ukitafuta hiyo nafasi unayoitaka lakini kukaa kusburi shule ni vigumu na unaweza kuzeeka ukisubir.
 
uza hiyo simu ya laki unayotumia ni mtaji tosha wa kwa baadhi ya biashara kama genge nk
 
Tafuta vibarua kwenye construction companies au garage kama unapenda ufundi. Chagua kitu kimoja ambacho utakipenda na ukifanye vizuri sana. Mfano: kutengeneza tiles, bomba, rangi, umeme wa magari, au wa nyumba. Hapo hapo kazana hadi uwe expert. Hata kama wapo wengi wanafanya hivo wewe kazana tu ndio ushindani. Focus ujue hadi kuwashinda wenye vyeti. Najua kazi kama.hizo wengi hua wanapata kutokana na sifa za kazi walizofanya (word of mouth). Nna mifano ya kaka zangu wametoka na wanapata tenda kubwa sasa kutokana na ujuzi wa kijiweni (kua nyoka).
Hata ukichekwa we kazana tu. Hayo ndio nayofkiria kwa sababu nina mifano halisi. Inawezekana ukapata option nyingine nzuri zaidi kutoka kwa wengine. Na cha msingi omba Mungu kwa kila ufanyalo. Usikubali mtu akukatishe tamaa.
 
kweli haya tunapitia vijana wengi sana ila capital ni tatzo yan nimekuwa dissapointed kwel na hii story
 
Achana na mawazo ya kutamani kufa kwa sababu hiyo sio shortcut ya kukwepa matatizo...wewe jiulize tu ni kwa vipi Mungu aruhusu changamoto kwa binaadamu alafu papo hapo kumbe kifo kinaweza kuwa njia ya mkato?

Ukifika huko unapoenda baada ya kufa kwa kudhani umezikimbia changamoto basi ujue utaanza upya...bora upambane labda tu itokee umefikwa mauti bila kukusudia.

....amin amin nakwambia, hivyo ndivyo ilivyo na usithubutu kukata tamaa na kutamani mauti...dont stop till you get enough.
 
mmezoea kuchagua hovyo hovyo hivyo msilalamike hovyo hovyo! ila yote tisa, una akili sana mdogo wangu, kwanza kitendo cha kujitambua kimenifanya nikuone wa maana sana na nna imani Mungu atakuwa pamoja nawe! kuna watu wa umri wako hujiona bado wadogo na hawawazi chochote kuhusu maisha, jitume kufanya kazi yoyote ile HALALI ilimradi isiwe ya kudhalilisha na ifanye kwa moyo mmoja na kwa uaminifu mkubwa na hapo ndipo Mungu atakufungulia milango ya mafanikio. kuwa MUAMINIFU katika kazi na utaona mafanikio...........
 
KUMBUKA:Kama hujisikii kunishauri na upo hapa kukosoa naomba usisome hii post


Wana JF nina stress kwanza mzazi wangu hana uwezo na mm nataka kusoma so nikiangalia wenzangu ambao tulisoma wote O lever wpo chuo wanasoma diploma na bachelor and mm nipo home tuu, in addition sina kazi na nimetafuta kazi mpaka nmechoka (japo cjakata tamaa ) na cjafanikiwa, kadhalika sina sina rafiki wa kukaa nae kunipa ushauri maana sisi vijana wa cku hizi kwnza wavivu,tunataka short cut so story zao ni uhuni,mapenzi,muziki na mipira tuu vitu ambvyo havitanijenga na nikisema nitafute wenye mawazo mbadala wote huwa bize na kazi zao so in this case nabaki tuu na strees tuu mpka nakosa hamu ya kula, na najiona cna sabab ya kuishi na nikiona mtu aliye na mafanikio mwenye rika langu (22yrs) nataman kufa yani ,
Nawasilisha
Mkuu, kukata tamaa ni kujikosea mwenyewe na kumkosea Mungu aliyekuumba!!!

Usirudie tena kusema na kuwaza hivo...Nakukanya mdogo wangu,...

Nakushauri hivi...ukizingatia utaona utakavotoka na kusa na pesa ya kutosha!!


1st kaa ujichunguze...unapenda nn kufanya nje ya ajira ya ofcn...mfano makenika, ushonaji, ufund mwash, kuchomea vyuma na kutengeneza mageti, upishi, kupamba !!
2nd Anza kupenda unachokipenda..maanisha kupenda
3rd Anza kujiweka karibu na wanaofanyanshughuli hiyomkwa kuwa mwaminifu yaan kwako na kwa uliyejishikisha kwake....kuwa mwaminifu pia kwa nafsi yako yaani unataka kujifunza na kujua na kuja kufanya kwa kujisimamia na kusimamia wengine..maanisha..nasema umaanishe
Hapa unaweza kuwa kibarua au akuajir kwa mkataba wa miezi 6 huku ukiwa na siri ya kujifunza na kuwa compitent hapo baadae ukiridhika sasa unaweza fanya
4th mtaji sio taabu...ukijua kitu mtaji utapata...jifunze kwanza na kujitahidi kusave kila Tsh 10 unayoipata
5th Utakuwa na furaha sasa maana utakuwa ushakuwa compitent...unaweza fanya kazi za watu sasa....

Kumbuka...kitu unachokipenda...mfano mm zaidi ya kufanya kazi ninayoifanya napenda "ushonaji"...

Kila la kheri Mkuu
 
Kwanza pole sana mdogo wangu, ila kumbuka kwa kiswahili kuna msemo mmoja "mbuyu pia ulianza kama Mchicha" au kwa kimombo wanasema Every boss started as a worker. Sioni sababu ya wewe kutamani kufa. Mitihani is part of life unapoesema unatamani kufa its wrong unamkufuru mungu. The only thing I can advice in get a job usikimbilie high jobs coz huna experience or profession once ukipata unaweza ukajisomesha. Nitafute in private I will give you a brief history of my life how I started mpaka Leo Niko niliko.
Nakutafuta nami pia
 
Subiri na sali sana kama unasubiri kwenda kusoma Darasani, Hukubahatika kusoma mpaka muda huu na pia unataka kwenda kukaa darasani?
Unategemea kumaliza lini kusoma na kupata ajira?
Eti kureview vitu? Kuna njia mbili za kusoma
1. Kusoma kwa uwepo wa mwalimu
2. Kusoma kwa kutokuwepo mwalimu(Kwa kutumia vitabu).
ulifkiri akina Bill gates, Steve Jobs na wengne walisubiri na kun'gan'gania shule hadi leo? ulifkiri walipoteza muda wao kama wewe kusubiri kuingia darasani? nafkiri kwanza tafuta maana ya knowledge na jinsi gani inapatikana then ndo uanze njia za kutafuta ili urudi darasani. Itumie akili yako.
Kabisa
 
Kwa kuwa umesema hauchagua kazi yoyote halali jaribu kutembelea sehemu zifuatazo bila kujali kama wametangaza nafasi za kazi au la, wakati mwingine riziki tunakutana nazo huko huko;-
1. Kampuni za Ulinzi
2. Kwenye Hoteli za Kitalii na Kawaida kuna baadhi ya Kazi huitaji kuwa umesoma Hotel Management Whatever
3. Car Wash/ Sehemu za kuosha Magari
4. Kampuni za Ujenzi/ Construction Sites.
5. Viwandani hususani vya Wachina/Wahindi hawa ni mabingwa wa kuajiri na kufukuza papo kwa papo
6. Bado naendelea kufikiria...........................
Umeongea
 
Pole sana
KUMBUKA:Kama hujisikii kunishauri na upo hapa kukosoa naomba usisome hii post


Wana JF nina stress kwanza mzazi wangu hana uwezo na mm nataka kusoma so nikiangalia wenzangu ambao tulisoma wote O lever wpo chuo wanasoma diploma na bachelor and mm nipo home tuu, in addition sina kazi na nimetafuta kazi mpaka nmechoka (japo cjakata tamaa ) na cjafanikiwa, kadhalika sina sina rafiki wa kukaa nae kunipa ushauri maana sisi vijana wa cku hizi kwnza wavivu,tunataka short cut so story zao ni uhuni,mapenzi,muziki na mipira tuu vitu ambvyo havitanijenga na nikisema nitafute wenye mawazo mbadala wote huwa bize na kazi zao so in this case nabaki tuu na strees tuu mpka nakosa hamu ya kula, na najiona cna sabab ya kuishi na nikiona mtu aliye na mafanikio mwenye rika langu (22yrs) nataman kufa yani ,
Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini usitafute kajibiashara tuu fulani, hako kanaweza kukusaidia kupata vijisenti vya kulipia shule au kozi unayotaka kusoma. usikate tamaa. Huna haja ya biashara kubwa sijui ukatafute mikopo, biashara ndogo tuu. Na wala usiangalie nani anakuangalia, haya ni maisha yako. All the best, kila kitu kinawezekana chini ya jua.
 
Back
Top Bottom