Nina hofu ya Hepatitis B naomba ushauri

One of my family members was diagnosed with hepatitis B three decades ago, akaambiwa hakuna tiba. Baadae akapata complication ya ini. Alifuata masharti ya dr ya don’ts. My late mother alihangaika na dawa za kienyeji mbalimbali. Ajabu mgonjwa alipona na anadunda vizuri, lakini hajui specifically ni dawa ipi ilimponya kwa sababu alitumia concoction ya kutosha
Muulize huyo muhusika kwani wewe huoni hiyo ni dili kwako kujua dawa ya ugonjwa unaosemekana ni incurable??!! 😷
 
Mkuu pole sana kwa hayo maradhi yako ya homa ya ini aka Hepatitis B Virus. Ni kweli Hakuna dawa za Hospitali zinazo weza kukutibu hayo maradhi yako ya Hepatittis B Virus lakini kwa dawa zetu za asili zipo dawa za kuweza kukutibia hayo maradhi na ukaweza kupona. ukihitaji dawa za asili ili uwezekutibiwa na kupona nitafute kwa wakati wako uguwa pole
Ni kweli kabisa hakuna ugonjwa usiokuwa na dawa, shida ni jinsi gani ya kupata hiyo dawa.
 
Hofumoyoni,
Pole kwa yote unayopitia...te.

Mkuu habari.
Nimekuwa nikifanya kipimo cha viral load test ambapo kwenye majibu inasomeka.
Hepatitis B Viral Load: IU/ml
HBV. DNA NOT DETECTED.
Hepatitis B envelop antigen: Negative
Hepatitis B envelop antibody: Positive.
Nimenukuu neno kwa neno.

Nilimuuliza Dr. Juhudi tafsiri ya majibu akasema, positive HBV antibody inaongeza uwezo wa mwili kufight dhidi ya Virus. Pia alisema hii ni ishara nzuri Kwa kuwa mwili unatengeneza kinga.

Kwenye upande wa antigen kuwa un detected pia inaonesha mwili na dawa ninazotumia (tenofovir) vilivyoweza Ku suppress virus. Alisema in case ikiendelea kuwa undetected Kwa miaka 5 huku nikiendelea kutumia dawa kuna uwezekano japo ni mdogo wa kuweza kuclear virus kabisa.

Kwa sasa ninahudumiwa na daktari bingwa wa njia ya chakula (Gastro) pale Muhimbili.
Thanks for being concerned.
 
Toa hofu ndugu Mimi nilikua natumia dawa za hepatitis b yaani truvada (arv) nilitumia miez 18 baadae hi hospital ya hapa mkoani kwetu wakanambia hawatoi dawa Tena niende nikachukue muhimbili,Basi nikaenda kwa doctor ili aniandikie transfer ya muhimbili...
Asante ndugu.

Nakushauri uende Muhimbili kama inaweza, tatizo la HBV ni kwamba unakaa mwilini kimya kimya huku ikiendelea kumomonyoa taratibu.

Endelea na clinic hata kama hutapewa dawa za kutumia.
 
Nenda hospitali kuna dawa moja kati ya zile za ukimwi kitu kama niverapin inatibu kbisa na unapoma sema huwa sio rahisi kuitoa maanazile zilikuja kwaajili ya ngwede. Kwahiyo nenda kaonane na aktari amnaye yuko ctc atakupatia.itapona tu
 
Ndugu, habarini za maisha.

Nachukua fursa hii kuwashirikisha hofu kubwa na kujikatia tamaa kunakoniandama kutokana na kugunduliwa kuwa na HBV..
Mkuu Pole sana Kama jina lako lilivyo na maradhi uliyokuwa nayo jinsi yalivyo. Siku nyingine usipende kujipa jina baya kama ulilo jipa wewe humu Jamvini kwani ukijipa jina lolote baya baada ya miezi 3 tangu ujipe hilo jina huwa linafanya kazi yake. Ushauri wangu kama wewe ni Mkristo kwa kuondosha Maradhi pamoja na hofu moyoni mwako funga siku 40 kama alivyo funga bwana Yesu funga kuanzia asubuhi saa 11 alfajiri mpaka usiku saa 1 usiku ndio waweza kula chakula.

Fanya hivyo kwa siku 40 Kisha nenda hospitali Ukapime utakuta huna tena maradhi. Kama ni wewe ni Muislam Funga siku 30 kisha nenda kapime hospitali utakuta huna tena maradhi mwilini mwako. Kufunga aka kukaa na njaa kuanzia asubuhi mpaka usiku ni dawa kubwa sana na pia ni tiba kwa kila maradhi ninakutakia afya njema.
 
Mkuu Pole sana Kama jina lako lilivyo na maradhi uliyokuwa nayo jinsi yalivyo. Siku nyingine usipende kujipa jina baya kama ulilo jipa wewe humu Jamvini kwani ukijipa jina lolote baya baada ya miezi 3 tangu ujipe hilo jina huwa linafanya kazi yake..
Nnikawa najarijbu kuangalia jina ulojipa ili nijfunze kujipa jina zuri.

Asante kwa ushauri
 
We nenda hospitali ya wakorea ile. Tatizo kwisha. Wao hutibu chanzo cha tatizo. Achana na hawa jamaa wa Hospitali zetu za kibongo. Utalundikiwa midawa inayopunguza makali tu ila huponi.
 
We nenda hospitali ya wakorea ile. Tatizo kwisha. Wao hutibu chanzo cha tatizo. Achana na hawa jamaa wa Hospitali zetu za kibongo. Utalundikiwa midawa inayopunguza makali tu ila huponi.
hii hosp nimeshawahi kuisikia sijui ipo maeneo gani
 
Mwili una namna yake ya kuheal na kudeal na matatizo ya kiafya unapokuwa katika hali ya utulivu.

Immunity system yako inafanya kazi ila shida ni lishe zetu miaka hii ni za ajabu hadi miili unashindwa kupambana na maradhani. Kula vizuri especially vyakula vya kuimarisha ini na damu. Then kuwa na utulivu wa akili achana na stress, mwili utadeal na hiyo hali hautaamini.

Kinachowaua watu wengi na magonjwa ya kisasa ni lishe, hofu na kutokuzingatia mahitaji ya mwili.
 
Kaka pole sana kwa changamoto hiyo.

Kitu pekee ningependa nikushauri Simama na Yesu Kristo Bwana Wetu kwa kila hali.

Warumi 5: 1-5.
 
Back
Top Bottom