Nina hofu huenda nimeambukizwa UKIMWI, Naombeni ushauri wenu jamani!

Punguza kunywa vinywaji baridi hio ni tezi la koo Kiukweli linaumaga sana ila ucjaribu kurudia tena kusex na huyo mama huwez jua
 
Yaani wewe ulikua umekaa tu wakati unaanza kushawishiwa ukazidi kutega sikio na hisia mwisho ukajikuta sivyo ndivyo pole sana . Sasa cha msingi hapo ondoa hofu hata kama umeathirika usiogope kwani hauko peke yako wapo wengi wameathirika si kwa uzinzi bali zipo sababu nyingi zinazopelekea kuathirika. Huyo mchumba wako mwambie masahibu yaliyokupata lkn usiseme umelazimishwa tafuta namna nyingine au sema mwende mkapime kabla ya ndoa naamini hawezi kukataa.

Sali zaburi ya 51 kila siku mpaka utakaposikia amani moyoni mwako.
Amen
 
Wewe jamaa waonyesha unaugua uoga kuliko ugonjwa.

Cha muhimu kuelewa ni kuwa hata ukipata maambukizi wakati huu Duni imepiga hatua kubwa sana kwenye matibabu ya Ukimwi.

Pia ukumbuke kuwa kuna Magonjwa mengine yasiyoambukizwa na ni hatari mara kumi zaidi ya ukimwi, na ni bora uombe sana Mungu usiugue hayo...Magonjwa kama Kisukari, Presha, Saratani n.k.

Kwa dalili ulizotaja una chansi ndogo sana kuwa ni ukimwi, unless kama vipimo vyenu vya awali havikuwa sahihi.
 
Nakumbuka hali kama hiyo ilinikuta mimi nikiwa form five tosa boysnilishindwa hata kusoma nikarudi nyumbani kupumzika nikijikuta naumwa tu kitu nachoumwa hakionekani ila ilikua ni hofu tu baadae nikawa freshhiyo ni hofu tu tulia mkuu utakua poa usijali!!
Hahaa
Tosa boy ulienda kupiga peku peju Ipamba kwa manesi au Iringa girls (Zoo)?
Au ulienda kula mizigo ya kujiuza town?
 
Habari zenu, poleni na majukumu ya siku!

Ndugu zangu ni muda wa miezi mitatu sasa nikiwa katika hali ya sintofahamu juu ya afya yangu na nimekuwa katika depression kubwa sana..

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 30. Nina mchumba ambaye nimedumu naye kwa muda wa mwaka mmoja sasa, hatujawahi kukuta kimwili na binti huyo, tuko wilaya tofauti ndani ya mkoa mmoja.

Tarehe15 Novemba 2014, siku ya jumamosi saa moja jioni nilienda kwa mama mmoja ana km miaka 33 hivi ni anafanyabiashara ya asali hapa mjini.

Nilienda kutafuta asali mbichi kwa ajili ya kuchanganya na dawa ya vidonda vya tumbo. nikiwa ndani mwake nilishawishiwa na yule mama kwa namna nisiyojua nikajikuta nimefanya naye mapenzi (ngono zembe) na kibaya zaidi sikutumia kondom, ilikuchukua almost dk 2 kumaliza. Nikachukua asali yangu na kuondoka kwenda kwangu.

Nikiwa njiani majuto yakaanza na kujilaumu kwann nimezini na mtu nisiyefahamu afya yake bila kinga, nilipofika home nilipiga magoti na kumuomba Mungu anisamehe dhambi yangu. Nilifikiria kumpigia yule mama usiku huo ili nimuulize juu ya afya yake ila sikuwa na afya yake, nilazimika kutafuta namba zake na kumpigia simu usiku huo.

Nilimpigia simu nikamuomba aniambie iwapo kama yeye ni mgonjwa (Muathirika wa HIV) ili niwahi kuripoti hospital within 72 hrs. Lakiniyule mama aliniambia kwamba yeye ni mzima na hata nikitaka tukapime. Majibu yake yalinipa matumaini na nikaendelea na shughuli zangu za kila siku, baada ya muda ya wiki 2 net niliugua mafua makali sana makamasi mazito sana yenye mchanganyiko na damu na hata dawa za mafua nilizotumia hazikusaidia chochote!

Baada ya wiki 2 mafua yalikata, kichwa kikaanza kuniuma sana kuanzia kwenye paji hadi utosini km muda wa wk moja hv. kwakweli niliona dalili zilizonitisha, nililazimika kumuambia yule mama kwamba ameamua kuniangamiza maisha yangu kwa kunipa maradhi makusudi, yule mama alikataa kata kata kwamba yeye anajujua ypo vuzuri hata maradhi, kwamba n wasiwasi wangu tu.

Tarehe 02 January tulienda naye tukapima HIV lkn matokeo yakawa negative wote. hyo ilikuwa muda wa mwezi mmoja na nusu tangu nisex naye.

Baada ya majibu hayo nilijipa matumaini ya uzima lakini mpaka naandika uzi huu hapa mambo totauti kabisa nimeona dalili tofauti za kunitisha, mwili hauko vizuri kwa ujumla tatzo kubwa zaidi ni maumivu ya koo na kuvimba kwa tezi shingoni karibu na taya ni muda wa km wiki tatu tangu uvimbe uanze.

Nikijaribu kusoma makala kwenye google juu ya kipimo cha HIV na kufahamu iwapo umeathirika, ile makala inaeleza kwamba kuvimba kwa tezi shingoni (mtiko) ni njia mojawapo ya kutambua kuwa una HIV. njia ya pili ni kupima HIV test.

Leo 19 February 2015 nimepima HIV Hospital ya wilaya nikaambiwa ni Negative. Nashindwa kuelewa kwamba ni muda wa irus kuonekana kwenye vipimo ndo haijafika au namna gani? Kibaya zaidi tulipanga kuoana na yule mchumba wangu mwezi machi mwanzoni na ninashindwa kumueleza kuwa mi ni mgonjwa ili hali vipimo havioneshi kwamba mi ni mgonjwa, atasema ni mbinu ya kutaka kumuacha.

Jamani nifanye nini mie sitaki kumuangamiza roho isiyo na hatia. Naombeni ushauri wenu wanajf wenzangu.
Kumbe jamaa ni bingwa wa ngono zembe wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh ulimaliza ndani ya DK 2 ...halafu unahofu ya ngoma???? Tupia kapicha ka mama asali mkuu
 
Back
Top Bottom