Nina Hasira nao hawa lazima niwafanyie.

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,246
2,000
Hapa nimemaliza Kazi iliyonileta Moshi jioni hii baada ya kupata shida ya Usafiri huko Arusha.

Nilifika Stendi saa Tisa nikakuta abiria wamejaa lakini hakuna magari. Kama tisa unusu hivi coaster moja ikaja ikabidi nituke Samasoti na kuchumpa ndani kupitia dirishani huku nikiwaacha abiria wengine wakisuguliana miili mlangoni.

Hatimaye nimefika Moshi saa kumi na mbili kamili na kufanya kaza lisaa limoja na kuingiza 200k TSH.

Huku nimejawa tabasamu sasa naingia ndani ya gari kampuni ya Shabco, linaonekana kujaa lakini naingia hivyo hivyo. Nakutana na mabinti wawili Kwenye Siti G3, G4 na G5 wameweka mabegi yao kwenye siti G4. Nawauliza kama kuna mtu anarejea kwenye siti wanabaki kulaliana na kunikodolea macho na dharau. Nadhani hawajui kuwa nimetoka kwenye kazi ya kiume hivyo sura imekaza na jasho lingi ukizingatia Joto la Moshi.

Basi wanavunga nawauliza kama mara tatu maana naona hamna nafasi nyingine. Wananiangalia kwa kurembua kimadharau na mie naamua nishuke. Lakini Kondakta anakuja na kuniambia nikae hapo. Basi wanatoa mabegi yao na kuyabeba na kuniacha nikae siti G3.

Sasa natafuna Bublish ambayo muda si mrefu nitaitema maana nimenunua Novida na nataka kuinywa. Pindi nitakapoitema nitaidondoshea kitini waikalie shwain wameniuzi sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom