Nina hamu sana Siku moja wanaokamatwa au kuhusishwa na Vitendo vya Kigaidia duniani nisikie wakiwa na Majina haya..

1. Frank
2. George
3. Kelvin
4. Alex
5. Samuel
6. Dominic
7. Richard

badala ya kila Siku tu kuyasikia haya Majina ya akina:

1. Athumani
2. Mohammed
3. Kassim
4. Suleiman
5. Abdallah
6. Issa
7. Hassan

Nawasilisha.

WAKINA GEORGE , KELVIN NA WENZAO WAO HAWAITWI MAGAIDI WANAITWA WATEKAJI AU MAJAMBAZI KWANI HUONI MAREKANI MTU ANAAMUA KUITEKA CHUO NA KUANZA KUUWA WANAFUNZI NA SIO MARA MOJA KILA MARA HUWEZI KUSIKIA WANAITWA MAGAIDI. SASA PAMOJA NA VITUKO VYOTE HIVYO BADO WATU WANAINGIA UISLAMU KWA WINGI


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Siku hizi, suala hili linaloeleweka vibaya ni miongoni mwa lililoenezwa mno kabisa kuhusu Uislamu. Lakini bado ndani ya Qur-aan, Muumba Anaeleza bila ya utata (tafsiri):

{{Wala msiue nafsi ambayo Allaah amekataza (kuiua) isipokuwa kwa haki (Akahuhumu hakimu kuwa mtu huyo anastahiki kuuawa na akatoa amri ya kuuawa). Na mwenye kuuawa kwa kudhulumiwa, basi Tumempa nguvu mrithi wake (juu ya muuaji huyo, akitaka ataomba kwa hakimu kuwa amuuwe kama alivyomuuwa mtu wake na akitaka atamsamehe, na akitaka atamtoza kitu). Basi (huyo mrithi asifanye fujo katika kuua kwa ajili ya huyo mtu wake aliyeuliwa). Hakika yeye atasaidiwa (na Sharia maadamu anayo haki).}} [17:33]



Tukiegemea kwenye aya hii, hairuhusiki kwa Uislamu kuua mtu yeyote asiye na kosa kwa baadhi ya makosa ya jinai. Ni vyema tukakumbuka katika nukta hii, tofauti iliyofanywa hapo juu baina ya Qur-aan na Sunnah, na Waislamu; ni Qur-aan na Sunnah pekee ndizo zilizoafikiwa kuwa zinaendana pamoja na matakwa ya Muumba, wakati Waislamu wanaweza sana kutetereka. Hivyo, kama Muislamu yeyote ataua mtu asiye na hatia, Muislamu huyo ametenda dhambi mbaya kabisa, na hakika tendo hilo haliwezi kudaiwa kuwa limefanywa “kwa jina la Uislamu”.



Na itambulike wazi basi, kwamba “Gaidi Muislamu” inafanana na maneno mawili yenye kupewa maana tofauti ili kutoa msemo mmoja oxymoron: kwa kuua watu wasio na hatia, Muislamu anatenda dhambi kubwa, na Allaah ni anayefanywa kuwa Muadilifu personified. Msemo huu ni wa kukosa nidhamu na kuushushia hadhi Uislamu, na ni lazima uepukwe. Inategemewa kwamba; kwa vile uelewa na hamasa ya Uislamu inapanda juu kwa jamii iliyo ya kawaida ya watu, basi watu watayatenganisha mbali mbali maneno ya “ugaidi” na “Uislamu”, yasitumike ndani ya msemo mmoja.



Sababu nyingine inayokuzwa ili kukubaliana na suala hilo linaloeleweka vibaya ni kwamba Muumba Ameweka “jihaad” juu yetu. Tamko la “vita tukufu” linatokana na enzi za Vita vya Msalaba Crusades na limechimbuka ndani ya Uingereza kama ni kilio cha kasi dhidi ya Waislamu huko Jerusalem. Jihaad ni neno la Kiarabu lenye maana ya kupambana, lakini kwa mujibu wa maelezo ya aya nyingi ndani ya Qur-aan, linabeba maana ya mpambano wa kijeshi, au vita. Allaah Amewasilisha hatua kwa hatua wajibu wa mpambano wa kijeshi kwa jamii ya Waislamu wakati wa kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Aya ya mwanzo iliyoshushwa kwa mnasaba huo ni kama ifuatayo (tafsiri):

{{Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa, kwa sababu wamedhulumiwa. Na kwa yakini Allaah ni Muweza wa kuwasaidia}} [22:39]



Aya hii inaweka bayana masharti kabla ya kupigana vita vyovyote ndani ya Uislamu; ni lazima kuwepo masharti ya kuwepo unyanyasaji kwa watu. Muumba Ameweka wazi amri juu yetu ya kupigana dhidi ya unyanyasaji na udhalimu, hata kama ikiwa kwa gharama ya kumwaga damu kama aya ifuatayo inavyoonesha (tafsiri):

{{Na piganeni katika njia ya Allaah na wale wanaokupigeni, wala msipundikie mipaka (mkawapiga wasiokupigeni). Kwani Allaah hawapendi warukao mipaka. Na waueni (hao wanaokupigeni bure) popote muwakutapo, na muwatowe popote walipokutoweni; kwani kuwaharibu watu na dini yao ni kubaya zaidi kuliko kuua. Wala msipigane nao karibu na Msikiti Mtakatifu (wa Makka) mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni (huko) basi nanyi pia wapigeni. Namna hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri. Lakini kama wakikoma, (basi); na Allaah ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.}} [2:190-192]



Kama ambavyo mtu anaweza kufikiria, taratibu za mpambano wa vita umetafsiriwa wazi na kwa upana ndani ya Qur-aan na Sunnah. Kwa vile hili ni somo moja lililo kubwa mno, tunafupisha kwa urahisi sehemu moja wapo kwa kutanabahisa kwamba haifai kuua wanawake, watoto, walemavu, wazee, na walio waadilifu. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sahih al-Bukhaariy, tunaona:

Imesimuliwa na ‘AbduLlaah: Wakati wa kipindi fulani cha vita Ghazawat enzi za Mtume, mwanamke alikutikana ameuawa. Mtume wa Allaah hakukubaliana na kuuawa kwa wanawake na watoto.



Suala (jengine) linaloeleweka vibaya ambalo linahusiana na jihaad, kawaida linatangazwa na Waislamu wanaosema kwamba “Jihaad ni kwa kuhami mipaka.” Qur-aan na Sunnah inakataa kabisa dhana hii. Kama aya iliyonukuliwa hapo juu inavyoonesha, jihaad ni wajibu wakati wote panapotokezea dhulma (na sio tu wakati wa kuhami mipaka), na Waislamu hawahitajii matamshi ya uongo yanayotolewa duniani pale inapokuja kusimamisha wajibu huu. Kutokana na Sunnah, hususan ndani ya somo la Sunnah linaloitwa Sahih al-Bukhaariy, tunaona:

Imesimuliwa na Abuu Mussa: Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuuliza, “Mtu anapigana vita kwa ngawira; mwengine anapigana kwa umaarufu na wa tatu anapigana kwa kujionesha, ni yupi miongoni mwao anayepigana kwa ajili ya Allaah?” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Yule anayepigana kwa Neno la Allaah (yaani Uislamu) atakuwa bora, anayepigana kwa ajili ya Allaah.” [4:52:65]



Hivyo, Muumba Anatuwajibisha kupigana vita wakati wowote pale watu wanapokandamizwa vibaya hata kukosa uhuru wa kumsikiliza au kumfanyia kazi Mjumbe wa Allaah kama ilivyo ndani ya Qur-aan na Sunnah.



Sababu ya tatu ambayo kawaida huwa inanukuliwa kuhusu suala hili linaloeleweka vibaya katika Uislamu inasema kwamba njia hii ya maisha inakubaliana na kuuwa watu wasio na hatia kwasababu mfumo wake wa sheria ya Uislamu ni wenye ukatili usio na maana. Hoja hii ni nyepesi kwa namna mbili. Kwanza, inawafanya wanaadamu kuwa ni waadilifu na waliotakasika kuliko Muumba, na hivyo tunaweza kubadili Shariah. Pili, mara nyingi imeegemezwa kuidhania Shariah za Kiislamu ni zenye kutekelezeka kiulaini, kama vile kusema “wizi wote wanapata kukatwa mikono yao.”



Qur-aan na Sunnah imeweka wazi kwamba sheria ya kisasi, ni juu yetu kwa mauaji na jeraha la mwili, lakini msamaha ni bora kama aya zifuatazo kutoka Qur-aan zinavyoonesha (tafsiri):

{{Enyi mlioamini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika waliouawa – muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anayesamehewa na ndugu yake (yaani yule aliyeuliwa wake) basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe (na kulipishwa) kwa ihsani. Hiyo ni tahfifu itokayo kwa Mola wenu na ni rehema. Na atakayeruka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu iumizayo.}} [2:178]



{{Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na (ubaya) huo; lakini anayesamehe na kusuluhisha ugomvi; ujira wake uko kwa Allaah; bila shaka Yeye hawapendi madhalimu. Na wale wanaolipiza kisasi baada ya kudhulumiwa, hao hakuna njia ya kulaumiwa. Bali lawama iko juu ya wale wanaodhulumu watu na wakawafanyia jeuri katika ardhi pasipo haki; hao ndio watakaopata adhabu iumizayo. Na anayesubiri na kusamehe (atalipwa wema wake). Bila shaka hilo ni katika mambo makubwa ya kuazimiwa kufanywa (na kila Muislamu).}} [42:40-43]



Muumba Ameamrisha sheria ya kisasi juu yetu Akitambuwa vilivyo kwamba tunaweza kuijadili. Ndani ya jamii nyingi za leo zisizokuwa za Waislamu, kuna majadiliano yanayoendelea kuhusu adhabu ya kifo. Kwa Uislamu, mjadala huu ni butu, Muumba Amekwishalitolea maamuzi suala hilo kwa ajili yetu. Hata hivyo, Ametupatia aya ya ajabu ndani ya Qur-aan ambayo inatushauri kufikiria vyema suala hilo vizuri kama tunahitaji kuielewa (tafsiri inafuata):

{{Mtakuwa nao uhai (mzuri) katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.}} [2:179]



Watu wengi pia hawapo na uelewa wa sharti zilizo kali ambazo ni lazima zitimizwe kwa sheria ya kisasi kufanyiwa kazi. Sunnah imejaa mifano ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ikituonesha pale sharti za sheria ya kisasi zinapotimizwa kabla ya kufanyiwa kazi. Kwa mfano, mwizi atawajibika tu kukosa mkono wake kama bidhaa aliyoiba imevuka kiwango fulani, na kama ikithibitishwa kwamba bidhaa hiyo imehamishwa kutoka sehemu yake ya awali. Wizi wa chakula hauna adhabu ya mtu kukosa mkono wake, na bidhaa nyengine pia zimesameheka. Huu ni mfano tu wa namna sheria zinavyofanyiwa kazi kwa hadhari sana ndani ya Uislamu.



Mwisho, hoja nyengine inayokuzwa kwa suala hili linaloeleweka vibaya mno ni kwamba Uislamu ‘umeenea kwa panga’. Ni lazima ieleweke kwa sasa kwamba ni lazima daima tutofautishe baina ya Qur-aan na Sunnah na Waislamu pale inapofika hatua ya kutambua nini Muumba Ametuhitajia (sisi kufanya). Allaah Ameeleza wazi ndani ya Qur-aan (tafsiri),

{{Hakuna kulazimishwa (mtu kuingia) katika dini. Uongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anayemkataa shetani na akamwamini Allaah, bila shaka yeye ameshika kishiko chenye nguvu kisichokuwa na kuvunjika. Na Allaah ni Mwenye kusikia (na) Mwenye kujua.}} [2:256]



Hivyo, HAIWEZEKANI kukubali Uislamu kwa nguvu. Hata kama Waislamu wasio na uongofu watajaribu ‘kulazimisha’ Uislamu namna fulani kwa wengine, haitokubaliwa na Muumba kwa mujibu wa aya hii.

Mijadala ya taariykh ambayo inajaribu kufafanua kwamba Waislamu ‘hawajawabadili wengine kwa nguvu’ hakika ni hoja ndogo kwa mjadala uliopo hapo juu. Hata hivyo, ni vyema kubainisha kwamba (kwa mujibu wa) taariykh, Uislamu umeenea kwa njia za amani. Ujumbe wa Muumba ulifikishwa Afrika na kusini mwa mashariki ya Asia kwa wafanyabiashara walio Waislamu, na leo nchi kubwa kabisa yenye Waislamu duniani ni Indonesia. Safari za kijeshi zilizopelekea kuteka nyara kwa kuzungushia mipaka ya Ulaya na Asia ya kati, zote zilifanikiwa kwa (Uislamu) kustahamilia imani na kanuni (za dini) nyengine.



Kwa mara nyengine, ni muhimu kukumbuka kwamba Allaah Anatamka kwamba HAIWEZEKANI Uislamu kulazimishwa kwa mtu, hivyo Waislamu hawaoni haja ya kujaribu!
facts

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Frank
2. George
3. Kelvin
4. Alex
5. Samuel
6. Dominic
7. Richard


badala ya kila Siku tu kuyasikia haya Majina ya akina:

1. Athumani
2. Mohammed
3. Kassim
4. Suleiman
5. Abdallah
6. Issa
7. Hassan


Nawasilisha.
Soma kuhusu George Habash
Soma kuhusu Carlos The Jackal (Ilich Ramirez Sanchez).

Utaelewa nini maana ya ugaidi.

Unafahamu kuwa Nelson Mandela alihukumiwa maisha kwa ugaidi? Na kutumikia miaka 27 kifungoni?

"One person's terrorist is simply another's freedom fighter".
 
Umeshawahi kumsikia Mario Morreti? Huyu alimteka mpaka waziri mikuu wa Italy! Aldo Moro.


Moro, photographed during his detention by the Red Brigades

Unajua kundi lake la ugaidi likiitwaje?

Brigate Rosse (Red Brigades), naam Red Brigade kama kikosi cha chadema.

Unawajuwa wakuu wa kikundi hicho wanaitwa nani?

Renato Curcio, Marguerite Cargol na Alberto Franseschini.
 
ngumu kwa sababu mamlaka zimeshakalili kuwa ugaidi unatokana na dini fulani hatakama Frank akilipua bomu ataitwa jambazi ila kwa Juma itakuwa gaidi. huenda wakashirikiana mmoja atashtakiwa kwa ugaidi mwingine ujambazi
 
Mnajuwa kwa nini mbwa koko hafundishiki lakini German Shepherd anafundishika!!
Ndicho kilichofanya wenye akili mabeberu yatumie watu wenye majina hayo kutengeneza ugaidi kwa manufaa yao Jonson Dini yako inakupagia sadaka toa kiasi fulani Juma anaambiwa toa mkono wa kushoto usijuwe ulicho toa ata kama ni mia moja!
Juma anaambiwa vyote vya hapa Duniani utaviacha havina msaada kwako utaondoka kama ulivyokuja utazikwa na sanda tu kama ulivyo kuja Duniani ukiwa kwenye mfuko wau uzazi wa mama yako hutaondoka na chochote!
Juma Ana ambiwa ndugu yako ni wa Imani yako akipigwa umepigwa wewe!
Na mengineo mengi mabeberu wakatambua hawa German Shepherd wamefundishwa vizuri sasa Sisi tuwa tumie tuwatengenezee watu wa kuwambia wakajibu tutakapo wachokoza maana wana mafundisho yote tuwape na vitendea kazi!!
Kumbuka Juma Ana fundishwa kuwa Imani ndio itakayo kupeleka mbingu sio ulicho nacho!!
Jonson Ana fundishwa ukitoa Sana ndicho kitakacho kupeleka mbinguni!
 
1. Frank
2. George
3. Kelvin
4. Alex
5. Samuel
6. Dominic
7. Richard

badala ya kila Siku tu kuyasikia haya Majina ya akina:

1. Athumani
2. Mohammed
3. Kassim
4. Suleiman
5. Abdallah
6. Issa
7. Hassan

Nawasilisha.
Umesahau akina Nelson Mandela, Samora Machel na Edward Mondlane walipowekwa kwenye Terrorists lists miaka hiyo ???

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom