Nina hakika Mzee wa Msoga saa hizi anashangilia huku akijisema moyoni Mungu hamfichi.....

magufuri akiingia madarakani mm nitastafu kwa raaaha na kupata usingizi by jmk

sasa ww hizo kelele za umajunguni unazutoa wapi wakati mkwere anashinda ikulu kumpongeza jpm
chadema wanakiwanda cha majungu na uongo by jpm
Kumbuka chadema kwa sasa wapo kwenye kikaango cha moto..wanafundishwa kufanya siasa za ustaarabu na kuheshimu watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magu endelea kutunyosha baba, ukikaza, sis mtaan tunasikia...ni bora vinavyoonekana kwa macho kuliko vya kufikirika, unafiki hautaisha Tanzania, lkn tutakulinda na tupo kwa ajili yako...
 
Kwa spidi hii, upinzani huu hata Magu baada ya kuondoka madarakani mtamkumbuka kwa mazuri na kumsifia.
Leo kikwete ni kama shujaa kwa wapinzani.
 
Chezea wanafiki...aliyekuwa mtetezi namba wani wa Mzee wa Msoga humu ndani, FaizaFoxy, sasa kampa kisogo na kuachana na chakacha ya pwani anasakata rumba ya bara anakotoka Jiwe. Sijui kaka yake Ritz yeye kapotelea wapi...kweli dunia mviringo.
Mkuu, hawa jamaa ni ccm damu. Usipoteze muda kuwa watakuwa upande wako kwa kuwapaka mafuta.
 
Kwa spidi hii, upinzani huu hata Magu baada ya kuondoka madarakani mtamkumbuka kwa mazuri na kumsifia.
Leo kikwete ni kama shujaa kwa wapinzani.
Silver Back

Unajua kawaida ya kila mwanadamu, ni hii. Binadamu kwa asili ni mbinafsi, kwa hiyo katika kila alitendalo ni kutoka na nguvu ya ule ubinfsi wake, kwamba ni lazima liwe na tija kwake. Kwa jinsi hiyo, hutaweza hata siku moja kukubaliwa na watu wote, na hasa unapokuwa kiongozi.

Lakini jambo zuri kuhusu sisi binadamu, mara zote tumekuwa tukitekeleza mambo kwa ajili ya kuhakikisha walio karibu yetu wanatukubali na kutufurahia. Hapo tunakuwa na ile hali ya upendo wa asili wa mtu kwa mtu. Hata hivyo, bwana Silver... Tunakuwa tunakosea wakati mwingine, mara nyingi katika utendaji wetu. Lakini kukukosea huko haikanushi ile dhamiri zetu kwa watu hao wenzetu.

Ni ukweli kuwa mzee Kikwete ametenda mazuri mengi sana katika kustawisha uchumi wa Tanzania hii ya sasa. Kama mwanadamu alipokosea alisema waziwazi bila kificho. Vivyo hivyo kwa Rais wa sasa, haya anayoyatenda sasa umuhimu wake utaonekana baadaye; na kama ni ushujaa, ni imani yangu wanaompinga sasa watampa ushajaa mara baada ya mzee huyu kutoka madarakani. Kwa sasa hawawezi kumuelewa kwa sababh wamezongwa na kelele za wababaishaji ambao kwa ubinafsi wao hawataki kuyasema wazi yaliyomazuri; badala yake wanayafunika kwa kuzusha malalamiko bandia, ili wakipate wanachokitafuta kwa ajilo ya binafsi zao.

Ni suala la wakati tu. Amini nakuambia kaka, umuhimu wa mzee huyu utapata kujidhihirisha akishamaliza muda wake wa uongozi. Ikumbukwe hata mtume Muhammad (SAW) kwa mara ya kwanza alipowapa watu wake ujumbe utokao kwenye kuran tukufu, hawakumuelewa! Wakamuita mzushi na muongo. Lakini sasa, wengi wamemuelewa na wengi wameyapokea mafundisho yake.
 
Afadhali mwenzie alikuwa anazembea baadhi ya mambo lakini hakuwa na roho ya Shetani , katili, na hazikupotea tilioni 2.4 .

Zimepotea? Are you sure ? Si Heri hata Sasa unaskia uliibiwa na mkeo hukujua Sasa unajua. Na hapo utakuwa Wa Kwanza kupanda Train La umeme umekenua meno na unatuma ujumbe jF kutukana. Baadhi ya Watz kama wewe Wanafiki sana
 
Mzee huyu baada ya kuondoka ofisini zaidi ya miaka mitatu iliyopita, mrithi wake amekuwa akimshambulia kimafumbo kwamba aliacha kila kitu kiende hovyo hovyo na watu wapige madili.

Mzee wa watu hakuwahi kujibu hata kwa .mafumbo bali alijikalia kimya pengine akiamini muda ndio utahibitisha kama kweli bwana yule atakuwa mtu wa tofauti.

Leo hii ikiwa ni miaka 3 na zaidi, ukweli umeanza kujidhirisha kwani kwa sasa ni mwendo wa kashifa kuibuka moja baada ya nyingine huku bwana yule akikaa kimya utadhani hayupo au sio yule aliekuwa akimnanga mwenzake majukwaani kuwa alikuwa anazembea.

Kwa haya yanayoendelea kuibuka kila kukicha huku tukitarajia mengine kuendelea kuibuka katika siku zijazo, nina hakika mzee wa msoga kwa sasa anashangilia na pengine anajisemea maneno: "Mungu si athumani, Mungu hamfichi mnafiki, n.k".

Hata hivyo, sisi wengine tulijua mapema kuwa huyu bwana ni wale wale tu na kwamba hakuwa na uhalali wowote wa kumlaumu mzee wa msoga kwani wote ni wa ukoo ule ule wa kijani na sasa muda unathibitisha.

Nawaza tu sijui kwa sasa akikutana na huyu mzee atakuwa anaweza kumuangalia usoni bila chembe ya aibu!

Na sijui bado atakuwa na guts za kuendelea kumshambulia mtanguli wake?

Ama kweli utamu wa ngoma, ingia ucheze.

Unalipwa sh ngapi mkuu . Tupeni uzi za Chadema. Sera tuzijue. JPM
Mmeshamtungia sana uzi. Na ukiona mgonjwa analia jua kaguswa. We unaongoza.
 
Sijui ni kwanini vyama vya Upinzani hapa Tanzania huwa siwaelewi-elewi...Nawaona kama Wahuni wahuni Walio na ngozi za kondoo.

Je,Wanafanya biashara ya kisiasa..?

Kunatoafuti gani Kati ya harakati na siasa...? Naam wengine Watasema Utofauti upo kiduchu.

Waliopo washatuchosha mno na Upuuzi wao usio hesabiki,Je Watakao tuwape wapo imara kweli au ni Washenzi wanaosukumwa na Njaa na Urafi...?

Nilikuwa napitia Mataifa ya Africa Vyama vya Upinzani vilivyochukua serikali kwa kiasi kikubwa mambo yalibaki kama vile vile.Nikang'amua Africa kazi ipo kubwa.

Jambo la kwanza Taasisi.

Taasisi nyingi ni dhaifu Mno,zinaendeshwa na kuongozwa na akili kisoda,Rushwa (Pesa & Ngono), Ubunifu ziro,Watu wapeana dili kindugu,Maneno mengi vitendo sifuri.

Nb: Nipo huru,Sina chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umesema ukweli hakuna upinzani unaweza fanya nusu ya aliyofanya ccm kwasasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee huyu baada ya kuondoka ofisini zaidi ya miaka mitatu iliyopita, mrithi wake amekuwa akimshambulia kimafumbo kwamba aliacha kila kitu kiende hovyo hovyo na watu wapige madili.
kwa hiyo unakataa?si ulisema kikwete ni dhaifu anacheka cheka tu?zipo posts zako humu
 
Kwa spidi hii, upinzani huu hata Magu baada ya kuondoka madarakani mtamkumbuka kwa mazuri na kumsifia.
Leo kikwete ni kama shujaa kwa wapinzani.
Nimesema hapo juu kumbe jamaa mleta uzi alishaponda.

Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
 
Mzee huyu baada ya kuondoka ofisini zaidi ya miaka mitatu iliyopita, mrithi wake amekuwa akimshambulia kimafumbo kwamba aliacha kila kitu kiende hovyo hovyo na watu wapige madili.

Mzee wa watu hakuwahi kujibu hata kwa .mafumbo bali alijikalia kimya pengine akiamini muda ndio utahibitisha kama kweli bwana yule atakuwa mtu wa tofauti.

Leo hii ikiwa ni miaka 3 na zaidi, ukweli umeanza kujidhirisha kwani kwa sasa ni mwendo wa kashifa kuibuka moja baada ya nyingine huku bwana yule akikaa kimya utadhani hayupo au sio yule aliekuwa akimnanga mwenzake majukwaani kuwa alikuwa anazembea.

Kwa haya yanayoendelea kuibuka kila kukicha huku tukitarajia mengine kuendelea kuibuka katika siku zijazo, nina hakika mzee wa msoga kwa sasa anashangilia na pengine anajisemea maneno: "Mungu si athumani, Mungu hamfichi mnafiki, n.k".

Hata hivyo, sisi wengine tulijua mapema kuwa huyu bwana ni wale wale tu na kwamba hakuwa na uhalali wowote wa kumlaumu mzee wa msoga kwani wote ni wa ukoo ule ule wa kijani na sasa muda unathibitisha.

Nawaza tu sijui kwa sasa akikutana na huyu mzee atakuwa anaweza kumuangalia usoni bila chembe ya aibu!

Na sijui bado atakuwa na guts za kuendelea kumshambulia mtanguli wake?

Ama kweli utamu wa ngoma, ingia ucheze.
Hw What is this. Mambo gani kwa mfano! Hebu yataje! Maan wengine hatuyaoni zaidi ya Infrastructure kuboreka nk. Hata akitaka kumtegea aanguke hamuwezi at all!
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom