Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Mzee huyu baada ya kuondoka ofisini zaidi ya miaka mitatu iliyopita, mrithi wake amekuwa akimshambulia kimafumbo kwamba aliacha kila kitu kiende hovyo hovyo na watu wapige madili.
Mzee wa watu hakuwahi kujibu hata kwa .mafumbo bali alijikalia kimya pengine akiamini muda ndio utahibitisha kama kweli bwana yule atakuwa mtu wa tofauti.
Leo hii ikiwa ni miaka 3 na zaidi, ukweli umeanza kujidhirisha kwani kwa sasa ni mwendo wa kashifa kuibuka moja baada ya nyingine huku bwana yule akikaa kimya utadhani hayupo au sio yule aliekuwa akimnanga mwenzake majukwaani kuwa alikuwa anazembea.
Kwa haya yanayoendelea kuibuka kila kukicha huku tukitarajia mengine kuendelea kuibuka katika siku zijazo, nina hakika mzee wa msoga kwa sasa anashangilia na pengine anajisemea maneno: "Mungu si athumani, Mungu hamfichi mnafiki, n.k".
Hata hivyo, sisi wengine tulijua mapema kuwa huyu bwana ni wale wale tu na kwamba hakuwa na uhalali wowote wa kumlaumu mzee wa msoga kwani wote ni wa ukoo ule ule wa kijani na sasa muda unathibitisha.
Nawaza tu sijui kwa sasa akikutana na huyu mzee atakuwa anaweza kumuangalia usoni bila chembe ya aibu!
Na sijui bado atakuwa na guts za kuendelea kumshambulia mtanguli wake?
Ama kweli utamu wa ngoma, ingia ucheze.