magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,201
- 3,322
Wanajamvi Salaam!
Zoezi la kusajili laini za mitandao ya simu litakamilika rasmi December 31. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na TCRA, Waziri anayehusika na mawasiliano pamoja na kampuni za Simu, zoezi hilo litakapokamilika muda hautoongezwa.
Kwa maoni yangu, naomba niwaondoe wasiwasi Watanzania wenzangu, kutokana na sababu chache nitakazozitaja hapa chini, zoezi hilo iwe isiwe lazima litaongezwa muda, tena siyo muda tu, muda wa kutosha!
Sababu hizo ni hizi zifuatazo:
1. Utaratibu wa kupata kitambulisho cha uraia sio rafiki kwa wananchi, na makosa kwa 85 yapo kwa NIDA wenyewe, hivyo kwa vyovyote vile serikali haiwezi kuwaadhibu wananchi wasio na kosa kwa kuwafungia mawasiliano.
2. Kampuni za simu kwa sasa zina mchango mkubwa sana katika kuchangia uchumi wa nchi. Serikali haiwezi kujiingiza kwenye mkenge wa kupoteza mapato.
3. Serikali ya awamu hii ni ya wapenda kiki. Kwa vyovyote vile number 1 atatafutia kiki hii issue. Kama TCRA na Waziri wataendelea kukomaa kuwa wanafungia laini za simu, number 1 atatoka kama kawaida yake na ataongeza muda wa kutosha! Kumbukeni mwaka ujao ni uchaguzi mkuu. Number 1 hawezi kukubali kuharibu kura hadi za CCM.
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app