mkolaj
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 3,020
- 1,087
Katibu Mkuu mpya wa
Chadema, Dk Vincent Mashinji
ametamba kuwa licha ya umri mdogo
alionao na kipindi kifupi cha
uanachama ndani ya chama hicho,
ana uwezo, nia, dhamira na lengo la
kukiandaa kushika dola mwaka 2020.
“Nilikuwa mwanachama wa
Chadema asiye na kadi ya
uanachama kwa kipindi kirefu,
baadaye bila malipo, kushawishiwa
wala kutumwa, mimi na wasomi
wenzangu tuliandaa na kutekeleza
mikakati ya kukijenga chama nje ya
mfumo rasmi wa chama,” ni kauli ya
Dk Mashinji wakati akizungumza na
wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema
juzi usiku.
Daktari huyo wa binadamu
aliyetambulishwa jana kwenye
mkutano wa hadhara jijini Mwanza,
alisema baada ya kukutana na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, yeye na wenzake
walikutanishwa na aliyekuwa Katibu
Mkuu, Dk Wilbrod Slaa.
“Baada ya kutusikiliza na kuelewa
mikakati yetu, Dk Slaa alituhoji
iwapo sisi ni wanachama hai wenye
kadi za Chadema. Swali lililotushtua
kwa sababu miongoni mwetu hakuna
aliyekuwa na kadi,” alisema na
kuendelea.
“Tulimjibu Dk Slaa kuwa uanachama
wetu uko mioyoni; hoja aliyoikubali,
lakini akatuelekeza kujiunga na
kuchukua kadi rasmi kwa sababu
yapo majukumu ambayo hatuwezi
kuyatekeleza bila kuwa wanachama
hai,” alisema na kuongeza:
“Nilichukua rasmi kadi ya Chadema
Machi Mosi, 2013 kutekeleza ushauri
wa Dk Slaa,” alisema Dk Mashinji,
mwenye umri wa miaka 43.
Ilani ya chama
Aliongeza: “Kwa sababu nilishiriki
kuandaa ilani ya uchaguzi na sasa
nimekabidhiwa jukumu la kuwa
Katibu Mkuu wa chama, nitasimamia
utekelezaji wa ilani hiyo katika
halmashauri zote za wilaya
zinazoongozwa na Chadema.”
Aliwataka mameya na wenyeviti wa
halmashauri zilizo chini ya chama
hicho kuisoma, kuilewa na
kuitekeleza ilani hiyo aliyosema
sehemu kubwa imeigwa na CCM ili
kuwaonyesha wananchi tofauti ya
vyama hivyo kivitendo linapokuja
suala la maendeleo na maslahi ya
umma.
Mshikamano kuelekea 2020
Akizungumzia mkakati wake
kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka
2020, Dk Mashinji alisema dhamira
yake kuu ni kuwaunganisha
wanachama, viongozi, wapenzi na
wafuasi wa Chadema kwa kutoa
fursa kwa kila mmoja kutimiza
wajibu wake kufikia lengo la kushika
dola miaka mitano ijayo.
“Kila mwana Chadema aweke lengo
la kukijenga chama tayari kwa
ushindi 2020. Tuige tabia ya maji
mtoni ambayo kila tone dogo
hujiunganisha na tone lingine na
kufanya mafuriko makubwa
yanayotembea,” alisema.
Mashinji ni nani?
Akisimulia historia yake fupi, Dk
Mashinji alisema alizaliwa mjini
Musoma mkoani Mara, makuzi yake
ni jiji la Mwanza na kusomea Uganda
namna ya kuishi katika mazingira
magumu, zikiwamo vurugu.
“Ninachomaanisha ni kutuma salaam
kwa watani zetu kuwa mimi siyo mtu
legelege hata kidogo,” alisema na
kuibua shangwe ukumbini.
Alisema kwa kuzaliwa mkoani Mara,
amefanikiwa kubeba tabia ya ujasiri,
uthubutu na kutohofia lolote
wanalosifika kuwa nalo watu wa
mkoa huo na papo hapo amerithi
tabia ya upole, lakini wenye
msimamo wa jamii ya mkoa wa
Mwanza na kuahidi kuzichanganya
pamoja katika uongozi wake.
Maoni ya wachambuzi
Wakitoa maoni yao wachambuzi wa
masuala ya siasa wamesema chama
hicho kinahitaji mtu atakayekijenga
ili kiendelee kuwa chama chenye
nguvu nchini.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha
(Rucu), Gaudence Mpangala alisema
chama hicho kinahitaji mtu mwenye
msimamo na uwezo wa kukabiliana
na mbinu kali za chama tawala CCM.
Alisema katibu mkuu ndiye mtendaji
wa chama, kwa hiyo nafasi hiyo
inahitaji mtu mwenye uwezo wa
kuwaleta watu pamoja na kukifanya
chama kuwa kimoja.
“Siwezi kumzungumzia huyu
aliyeteuliwa jana (Mashinji) kwa
sababu simfahamu. Bila shaka
Baraza Kuu limeona anafaa ndiyo
maana amepitishwa. Wengi
tulitarajia watu wenye majina
makubwa kushika nafasi hiyo,”
alisema Profesa Mpangala.
Hata hivyo, alisema hajashtushwa na
uamuzi huo kwa sababu
waliompitisha wanamfahamu vizuri
na wanaamini atatekeleza majukumu
yake vizuri.
Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi,
Mosena Nyambabe alisema nafasi ya
katibu mkuu wa chama inahitaji mtu
mkali ambaye atawasimamia
watendaji wengine wa chini yake,
maadili na katiba ya chama chake.
“Siwezi kumzungumzia huyo
(Mashinji) moja kwa moja kwa
sababu simfahamu. Lakini ana kazi
kubwa ya kukijenga chama chake na
kuhakikisha kwamba katiba ya
chama inafuatwa,” alisema.
Nyambabe aliongeza kuwa ana imani
Mashinji atafanya kazi vizuri kwa
sababu viongozi wa juu wa Chadema
wameridhia uteuzi wake.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (Udom), Emily Jonathan
alisema hana uhakika kama Mashinji
anaweza kuvaa viatu vya Dk Slaa
kwa sababu katibu huyo mkuu wa
zamani wa Chadema alikuwa na
nguvu na ushawishi wa kipekee
katika uongozi.
Alisema pengo la Dk Slaa
limeonekana wakati wote tangu
alipoondoka Chadema. Alisema mtu
wa kuziba pengo hilo anatakiwa
kuwa na haiba yake au kuwa na
mtindo mwingine wa uongozi ambao
utamfanya kuwa na ushawishi kwa
wanachama na viongozi wenzake.
Chadema, Dk Vincent Mashinji
ametamba kuwa licha ya umri mdogo
alionao na kipindi kifupi cha
uanachama ndani ya chama hicho,
ana uwezo, nia, dhamira na lengo la
kukiandaa kushika dola mwaka 2020.
“Nilikuwa mwanachama wa
Chadema asiye na kadi ya
uanachama kwa kipindi kirefu,
baadaye bila malipo, kushawishiwa
wala kutumwa, mimi na wasomi
wenzangu tuliandaa na kutekeleza
mikakati ya kukijenga chama nje ya
mfumo rasmi wa chama,” ni kauli ya
Dk Mashinji wakati akizungumza na
wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema
juzi usiku.
Daktari huyo wa binadamu
aliyetambulishwa jana kwenye
mkutano wa hadhara jijini Mwanza,
alisema baada ya kukutana na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe, yeye na wenzake
walikutanishwa na aliyekuwa Katibu
Mkuu, Dk Wilbrod Slaa.
“Baada ya kutusikiliza na kuelewa
mikakati yetu, Dk Slaa alituhoji
iwapo sisi ni wanachama hai wenye
kadi za Chadema. Swali lililotushtua
kwa sababu miongoni mwetu hakuna
aliyekuwa na kadi,” alisema na
kuendelea.
“Tulimjibu Dk Slaa kuwa uanachama
wetu uko mioyoni; hoja aliyoikubali,
lakini akatuelekeza kujiunga na
kuchukua kadi rasmi kwa sababu
yapo majukumu ambayo hatuwezi
kuyatekeleza bila kuwa wanachama
hai,” alisema na kuongeza:
“Nilichukua rasmi kadi ya Chadema
Machi Mosi, 2013 kutekeleza ushauri
wa Dk Slaa,” alisema Dk Mashinji,
mwenye umri wa miaka 43.
Ilani ya chama
Aliongeza: “Kwa sababu nilishiriki
kuandaa ilani ya uchaguzi na sasa
nimekabidhiwa jukumu la kuwa
Katibu Mkuu wa chama, nitasimamia
utekelezaji wa ilani hiyo katika
halmashauri zote za wilaya
zinazoongozwa na Chadema.”
Aliwataka mameya na wenyeviti wa
halmashauri zilizo chini ya chama
hicho kuisoma, kuilewa na
kuitekeleza ilani hiyo aliyosema
sehemu kubwa imeigwa na CCM ili
kuwaonyesha wananchi tofauti ya
vyama hivyo kivitendo linapokuja
suala la maendeleo na maslahi ya
umma.
Mshikamano kuelekea 2020
Akizungumzia mkakati wake
kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka
2020, Dk Mashinji alisema dhamira
yake kuu ni kuwaunganisha
wanachama, viongozi, wapenzi na
wafuasi wa Chadema kwa kutoa
fursa kwa kila mmoja kutimiza
wajibu wake kufikia lengo la kushika
dola miaka mitano ijayo.
“Kila mwana Chadema aweke lengo
la kukijenga chama tayari kwa
ushindi 2020. Tuige tabia ya maji
mtoni ambayo kila tone dogo
hujiunganisha na tone lingine na
kufanya mafuriko makubwa
yanayotembea,” alisema.
Mashinji ni nani?
Akisimulia historia yake fupi, Dk
Mashinji alisema alizaliwa mjini
Musoma mkoani Mara, makuzi yake
ni jiji la Mwanza na kusomea Uganda
namna ya kuishi katika mazingira
magumu, zikiwamo vurugu.
“Ninachomaanisha ni kutuma salaam
kwa watani zetu kuwa mimi siyo mtu
legelege hata kidogo,” alisema na
kuibua shangwe ukumbini.
Alisema kwa kuzaliwa mkoani Mara,
amefanikiwa kubeba tabia ya ujasiri,
uthubutu na kutohofia lolote
wanalosifika kuwa nalo watu wa
mkoa huo na papo hapo amerithi
tabia ya upole, lakini wenye
msimamo wa jamii ya mkoa wa
Mwanza na kuahidi kuzichanganya
pamoja katika uongozi wake.
Maoni ya wachambuzi
Wakitoa maoni yao wachambuzi wa
masuala ya siasa wamesema chama
hicho kinahitaji mtu atakayekijenga
ili kiendelee kuwa chama chenye
nguvu nchini.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha
(Rucu), Gaudence Mpangala alisema
chama hicho kinahitaji mtu mwenye
msimamo na uwezo wa kukabiliana
na mbinu kali za chama tawala CCM.
Alisema katibu mkuu ndiye mtendaji
wa chama, kwa hiyo nafasi hiyo
inahitaji mtu mwenye uwezo wa
kuwaleta watu pamoja na kukifanya
chama kuwa kimoja.
“Siwezi kumzungumzia huyu
aliyeteuliwa jana (Mashinji) kwa
sababu simfahamu. Bila shaka
Baraza Kuu limeona anafaa ndiyo
maana amepitishwa. Wengi
tulitarajia watu wenye majina
makubwa kushika nafasi hiyo,”
alisema Profesa Mpangala.
Hata hivyo, alisema hajashtushwa na
uamuzi huo kwa sababu
waliompitisha wanamfahamu vizuri
na wanaamini atatekeleza majukumu
yake vizuri.
Katibu Mkuu wa NCCR – Mageuzi,
Mosena Nyambabe alisema nafasi ya
katibu mkuu wa chama inahitaji mtu
mkali ambaye atawasimamia
watendaji wengine wa chini yake,
maadili na katiba ya chama chake.
“Siwezi kumzungumzia huyo
(Mashinji) moja kwa moja kwa
sababu simfahamu. Lakini ana kazi
kubwa ya kukijenga chama chake na
kuhakikisha kwamba katiba ya
chama inafuatwa,” alisema.
Nyambabe aliongeza kuwa ana imani
Mashinji atafanya kazi vizuri kwa
sababu viongozi wa juu wa Chadema
wameridhia uteuzi wake.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (Udom), Emily Jonathan
alisema hana uhakika kama Mashinji
anaweza kuvaa viatu vya Dk Slaa
kwa sababu katibu huyo mkuu wa
zamani wa Chadema alikuwa na
nguvu na ushawishi wa kipekee
katika uongozi.
Alisema pengo la Dk Slaa
limeonekana wakati wote tangu
alipoondoka Chadema. Alisema mtu
wa kuziba pengo hilo anatakiwa
kuwa na haiba yake au kuwa na
mtindo mwingine wa uongozi ambao
utamfanya kuwa na ushawishi kwa
wanachama na viongozi wenzake.