Nina bima ya afya NHIF naombeni mnishauri kuhusu body check-up

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,544
44,690
Wakuu naombeni mniambie niende hospital gani ambayo nikifika tu nikiwaambia nimekuja kufanya check up watanipima magonjwa mbalimbali kuanzia kisukari, hepatitis, matatizo ya Figo, matatizo ya moyo, cancer na vidonda vya tumbo. Hospital iwe ndani ya jiji la Dar es Salaam na vipimo vyote nifanye bila gharama kwani Nina bima ya afya NHIF.

Natanguliza shukrani
 
Njoo Muhimbili ila hepatits B haipo kwenye bima utalipia 35 vipimo vingi kulingana na dr atakavyo order
 
Niliambiwa Body Checkup haipo kwenye Bima (NHIF)
Sio check up tu, hata dawa ni nadra sana kupata.Utaambiwa tu zimeisha katafute pharmacy. Hii bima haina nguvu kabisa... Labda kwa upande wa malaria tu kujaziwa makapu ya mseto na antibiotics za UTI. Ila kwenye serious cases... Lazima Shati iwe ya mikono mirefu.
 
Bima ya afya pekee isiyo na usumbufu
IMG-20190721-WA0002.jpeg
 
Wakuu naombeni mniambie niende hospital gani ambayo nikifika tu nikiwaambia nimekuja kufanya check up watanipima magonjwa mbalimbali kuanzia kisukari, hepatitis,matatizo ya Figo,matatizo ya moyo,cancer na vidonda vya tumbo.hospital iwe ndani ya jiji la dar es salaam na vipimo vyote nifanye bila gharama kwani Nina bima ya afya NHIF.natanguliza shukrani
Bima yako ni kifurushi gani?Then nimeona umeandika Unataka kupima Hepatitis b(Kwenye hili nakushauri ikiwezekana baada ya kusoma ujumbe wangu ukapime damu 10k then uchome chanjo 15k.Wahi haraka sana huu ugonjwa ni hatari kuliko magonjwa yote uliyotaja hapo juu.Mwisho ni kwamba bima zina usumbufu sana,kuna wakati nimekuwa siitumii kabisa bima yangu kukwepa huduma mbovu.
 
Mkuu hospital gani wanapima homa ya ini na chanjo?
 
Back
Top Bottom