Nina addiction na simu kupita kiasi. Nitapunguzaje?

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
1,457
2,435
Shalom wakuu.

Nina addiction na simu kupitiliza.
- Kila muda ipo mkononi hata kama sina matumizi nayo (siwezi kuiweka kwenye mfuko).

- Nakuwa kwenye mitandao ya kijamii na Internet kiujumla kwa muda wote.

- Kama nina kazi kidogo, naweza nikaiacha ili nijibu text iliyoingia au simu inayopigwa.

- Nikiwa na simu sitaki hata kukaa na watu kwa kuogopa usumbufu nikiwa naperuzi.

- Nikikurupuka ghafla usingizini nakuwa na hofu ya kupoteza simu hivyo kuanza kuitafuta haraka.

  • Naweza kuwa natembea huku naangalia simu, ikishindikana huwa natembea haraka haraka ili nikakae vizuri niendelee kutumia.
  • Hata nikiangalia TV siwez kuacha simu na nilikuwa mpenzi wa radio ila nimeacha (tangu 2016) kwa sababu ya simu.

Madhara niliyogundua ni maumiv ya kichwa, kukosa usingizi, macho kuuma usiku na kutoa kama machozi n.k.. Kiufup inanipa shida na nashindwa kuacha.

Je, nifanyeje?
 
Kuna kipindi kama nilikaa mahali isiyo na network kama miezi miwili hv, aisee niliteseka sana sana, nilipanda sana juu ya miti na kufanya kila aina ya jitihada lakin wap!

Katika kipindi hicho cha 2 months nilipata muda wa kulala vizuri na niliona mabadiliko fulani ambayo nimegundua kuwa kumbe simu ndio inanifanya niwe hivyo.
 
Pole sana mkuu,

Fanya haya

1. Kuwa na Simu mbili, simu ya kawaida isiyo na Internet pamoja na yenye internet

2.Simu yenye uwezo wa Internet iache nyumbani unapotoka au chumbani wakati ukiwa na shughuli nyumbani.

3. Tenga muda wa kuperuzi mtandaoni, kwa mfano kwa ajili ya kupata taarifa muhimu u aweza kuwa unaingia mtandaoni kuanzia Jioni saa 12 mpaka saa 3 usiku mwisho. Usivuke hapo. na katika huo muda usitumia zaidi ya saa moja na nusu.

4.Alfajiri pia unaweza kuingia mtandaoni kuanzia saa 10 mpaka saa 12 na nusu. ikifika saa moja kamili weka simu mbali na wewe. na katika huo muda usitumia zaidi ya saa moja na nusu kukaa mtandaoni.

Fanya hivyo, mzunguko uwe huohuo utakuja kuona mafanikio na tija kubwa, muda ambao utakuwa hutumii simu utaona unaweza kuutumia kufanya mambo mengine ya msingi, na zaidi ya hapo utaona unapata utulivu mkubwa wa akili na kuona kumbe kuna mambo mengine muhimu yanahitaji muda wako zaidi ya kutumia muda mwingi kwenye simu.

Kila la kheri.
 
Swala la kuuma kichwa ama macho kuuma hata mm yalinikuta ...tatizo ni simu nikabadili nikanunua samsung yenye kioo cha super amoled lcd yaaa nikasahau maumivu sasa japo bado na infinic ila simu nayo tumia mda mrefu ni samsung
 
Uraibu wa simu kwasasa umekuwa mkubwa sana, uzuri umeshagundua upo sehemu nzuri. Kiundani zaidi ni kwamba makampuni ya social media kama google, fb, whatsapp wanapata billion of $$ kwa wewe kuwa unatumia kila mara wanalipwa na matangazo. Hivyo wanatumia mbinu za kisaikolojia kufanya watu wapate uraibu zaidi sababu kwao ni pesa zaidi, vitu kama notifications, pop up, n.k ni mbinu za kuongeza uraibu.

Kwa kuanza angalia screen time yako, utashtuka kujua ni muda gani unatumia kwenye simu, ukishajua Weka daily limit ya mitandao unayotumia zaidi mfano instgram 2 hours, twitter 1 hr, youtube 30min unaweka limit kwenye setting muda ukiisha inakata kabisa inatoweka mpaka ubadili setting. Kama unatumia android, search digital wellbeing.
 
Kuna kipindi kama nilikaa mahali isiyo na network kama miezi miwili hv, aisee niliteseka sana sana, nilipanda sana juu ya miti na kufanya kila aina ya jitihada lakin wap!

Katika kipindi hicho cha 2 months nilipata muda wa kulala vizuri na niliona mabadiliko fulani ambayo nimegundua kuwa kumbe simu ndio inanifanya niwe hivyo.
Nunua simu zisizo na internet access kama vi nokia tochi utanishukuru baadae
 
Back
Top Bottom