Nina ADA, CPA(T) na Masters in Accounting and Finance lakini sina kazi zaidi ya mwaka sasa!

Jamani wadau naomba msaada, mana nimeangaika hadi nimechoka kutafuta kazi. Nina Ordinary Diploma in Accountancy GPA 4, Advance Diploma in Accountancy GPA 4.2. zote nimepiga IFM.

Nilipomaliza Advance mwaka 2009 niliunganisha kufanya masters ya Accounting and Finance toka Mzumbe University, and on the same time nikawa nafanya CPA.

CPA nilipass zote at 1st sitting na June mwaka jana nikawa nimeipata. Masters nina GPA 4.1, bado kudefend thesis tu. lakini wadau nimetafuta kazi tangu nilivyopata hiyo CPA hadi leo hola! Nisaidieni basi ndugu zangu!

Unakuwaje na Master's degree kabla ya kupata matokeo ya dissertation? Je unafahamu baada ya kupata marks za hiyo dissertation hiyo GPA inaweza kupanda au kushuka? Pia ufahamu kuwa interview uanza kwenye shortlisting sasa kama kuandika kwako maombi kunaonesha walakini basi kupata kazi ni issue. Pia inawezekana wengine wengi wa calibre yako wamefaulu sana kuliko wewe yaani wana GPA 4.5 na kuendelea!!

Ndiyo Masters ya Mzumbe, kwani siyo Masters? Mmeshaanza kuleta mambo yenu sasa. Kasome pale uone kama wanafundisha au hawafundishi, na ukishangaa watakudisco!

Kaka nimepitia mawazo ya watu na majibu yako na nimegundua y hupati kazi. Tatizo lako ni hizo passmark zako zinakufanya ujione exceptional na bado unawaza kishuleshule. Cku zote waajiri hawaangalii GPA na ucpende kuweka kwny CV yako but wanaangalia who u r. Do you have self confidence or ulikuwa bookworm tu kutafuta vyeti. Tatizo watu weliofaulu vizuri wanadhani wanajua kilakitu na hawashauriki na wana viburi kama wewe. Please change ur behavior na don't rely on ur GPA maana hy ni makaratasi tu

Unakuwaje na Master's degree kabla ya kupata matokeo ya dissertation? Je unafahamu baada ya kupata marks za hiyo dissertation hiyo GPA inaweza kupanda au kushuka? Pia ufahamu kuwa interview uanza kwenye shortlisting sasa kama kuandika kwako maombi kunaonesha walakini basi kupata kazi ni issue. Pia inawezekana wengine wengi wa calibre yako wamefaulu sana kuliko wewe yaani wana GPA 4.5 na kuendelea!!

Mimi nimesema so far ninayo hiyo GPA, hata desertation nikipata 3.8 bado nitakuwa above 4 kitu ambacho sitegemei kuwa dessertation itaniangusha kwa kuwa nimeandika vitu vya ukweli. Usinichulie poa kiivyo.
Inawezekana wenzangu wamenipita kwa GPA ndo mana siitwi. ndo mana nimeomba msaada na si kujikweza.

ordinary diploma ya accountancy IFM, mbona hiyo haikuwepo kabla! au unaongelea TIA? ok jaribu kuomba kwa Musasira nafasi ya kufundisha CPA
kwa pale kama umelamba CPA yako hawawezi kukutupa

Elimu ni ufunguo wa maisha
Elimu ni bahari
Elimu haina mwisho
Kazi ni kazi bora mkono uende kinywani...

Kwa sifa zako za elimu hustahili kulala huna kazi. Nachoweza kukushauri ajira kwa sasa ni gharama kwa mtu kama wewe ambaye huna uzoefu wowote maana utakuwa unahitaji mshahara mkubwa sana wakati uzalishaji wako (productivity) unaweza kuwa chini ya mtu mzoefu mwenye ATEC.

Nachokushauri tafuta audit firm ambayo iko busy uombe hata kukaa pale kama "Voluteer" wakikulipa kwa "assignment basis" baada ya miezi sita CV yako itapanda na utakuwa unatafutwa badala ya wewe kutafuta kazi. Kuna mtu alikuwa na tatizo kama lako nilikaa naye kama mwaka sasa hivi yuko kwenye chati na mara ya mwisho ilibidi aombe ushauri maana alipata zaidi ya kazi tatu kwa mara moja.

Kama uko Arusha unaweza jaribu Welcome to Facebook - Log In, Sign Up or Learn More

Watanzania tuna uwezo mkubwa sana wa kukatishana tamaa.........mpeni moyo dogo na ma GPA yake

ordinary diploma ya accountancy IFM, mbona hiyo haikuwepo kabla!

Inabidi kijana atoe ufafanuzi la sivyo atakuwa hajatudanganya ila kasema uongo ,

sorry let me look it in a differnt way, first, what was your target by so studying?
secondly, by the level of education you have, you are not suppose to look for a job, you should be a job creater,
lastly, it be very difficult for you to get a job
conclusion, to all people who are studying they should set clear vission of what their studying and why

Kaka Hongera kwa vyeti ulivyonavyo kama ni ukweli, but kama walivyosema baadhi ya wadau GPA peke yake sio kigezo cha kuwa mtendaji mzuri, So usichague sana kazi kama vipi jitolee tu hata kwenye firms ndogo ndogo,

Pia jitahidi uwe na good communication skills hasa za lugha ya wenzetu sababu post za finance managers au zozote kubwa kubwa zinahitaji strong communication skills, pia elimu unayo nzuri but ya vyuo vyetu locally, kwa kipindi hiki cha competitive labour market exposure and international experience + practical experience inahusika kwenye post za kueleweka sio vyeti tu vya shule zetu za madesa za kibongo,

So usiwe na kiburi sana kwa hizo Gpa za 4 za kibongo kwenye labour market ya post kubwa, wenzako wana degree 1 tu ya university of Manchester kaipiga "Downtown manchester " nyuma ya OLD TRAFFOLD kona ya kwenda kwa "Rooney" plus ACCA na intership ya KPMG hata kama ana GPA 2.0 unafikiri watamuacha wakuchukue wewe wa this and that you know my gpa is big...

Kelvin Twissa Marketng manager wa Zain ana Degree 1 tu ya university ya kueleweka cheki wanavyomgombania Telecommunications company wakati kuna watu kibao Wanamaliza vyuo vyetu UDOM, UDSM, MZUMBE na vinginevyo hawapati hata nafasi ya kujivolunteer, na wengine wana experience ya hata 20 years lakini Hawaeleweki..

Sometimes kujilimbikizia mavyeti kibao ya kibongo sio dili sana, hiyo ilikuwa Miaka ya zamani but dunia ya kisasa ni ufanisi sio vyeti ndo maana most of successful people in the world Sio ma Proffessor...

Tatizo sio uzoefu, GPA wala nini. Tatizo ni attitude ambalo ni tatizo kubwa kwa vijana wengi wa Kitanzania wa sasa. Anadhani kuwa na MBA, CPA na GPA kali basi lazima aajiriwe. Huyu anashangaa kwanini na maganda yote aliyonavyo hapati kazi. Kwake vyeti equals kazi nzuri.

Mtu hatafuti kazi, ila kazi ndo inatafuta mtu. Kwa hiyo ukiendelea kutafuta kazi hutapata hata siku moja. Badilisha fikra, mtazamo. Nenda pale NBC or wherever, sema nina shida na CEO or whoever. Jitambulishe mweleze mimi ni young graduate nina skills hizi na hizi nataka kufanya kazi na shirika/ kampuni au taasisi yako. Ku prove kwamba nina hizo skills nitafanya kazi kama volunteer kama miezi mitatu. Kama utaridhika na utendaji wangu basi tutaongea.

Nakuambia hakuna mwajiri atakuacha, hata kama huna nafasi. Lakini mambo ya kusema nina MBA, CPA halafu za shule zenyewe hizo huwezi kumshawishi mwajiri makini, maana watu wameshaona mtu ana MBA (finance) hajui hata stock exchange markets tatu duniani............

Usiweke vyeti vyote pamoja jaribu ,kuangalia kama kazi ni ya Proffessional weka (CPA+ADA)
kama kazi ni ya Academics i.e lectures etc weka (MBA+ADA)
jaribu na utafanikiwa Pia upangaji wa CV yako unaweza kuwa unakuangusha maana Skilled Managers akiangalia tu CV anajua huyu ni mtu mwenye vyeti au ni mtu mwenye uwezo.

Bwana mdogo kwanza hongera sana kwa kupata magamba yote hayo,mimi ushauri wangu..fikiria kujiari zaidi kuliko kutafuta kazi,kama vile kuwatengenezea watu business plan,tax returns,financial statements...na mambo mengine utatoka tu kijana

Kuna siku niliishawahi kuweka post hapa nikasema tunataka finance manager.. watu wengi sana walileta CV zao wenye MBA+CPA tulipowaita kwenye interview tulishangaa sana mtu hata Payroll hawezi tengeneza, tunamuuliza ategeneze management report ya mwezi hajui,...kwa hiyo suala la CPA+Msc/MBA-finance halafu experience 0 haina maana kwa sasa. nakushauri chukua cheti chako cha ADA tafuta kazi ukiwa pale tafuta dili zingine tena kwa vyetu vyako vyote then utafanikiwa.

Kuna siku niliishawahi kuweka post hapa nikasema tunataka finance manager.. watu wengi sana walileta CV zao wenye MBA+CPA tulipowaita kwenye interview tulishangaa sana mtu hata Payroll hawezi tengeneza, tunamuuliza ategeneze management report ya mwezi hajui,...kwa hiyo suala la CPA+Msc/MBA-finance halafu experience 0 haina maana kwa sasa. nakushauri chukua cheti chako cha ADA tafuta kazi ukiwa pale tafuta dili zingine tena kwa vyetu vyako vyote then utafanikiwa.
off topic: plz badilisha hii avatar maana haiendani na status yako.

Kaka mie nlitafuta kaz mpaka nikaisi nimelogwa,baadae nkapata kaz ila kwa sababu nilikuwa na qualification kubwa mshahara laki tano gross i was so down mana nahisi wananionea ila nimeamua kujizila tu nile lakikadhaa nipate experience niondoke zang.

yaani watu kama nyie ndio vimeo kama nini? wabishi kwenye kazi hamfundishiki much know sana! bora kuajiri under graduate ukamuendeleza kuliko kuajiri watu dizaini hiyo!!! Master unatakiwa usome baada ya kufanya kazi at least one year same apply to CPA, ur qualification unatakiwa uombe Managers post sasa nani yupo tayari kuajiri manager ambaye amejaa theory kichwani?

Ndachuwa umesema yote,mkuu soma post zote za Ndachuwa zitakusaidia.bado kuna upungufu mkubwa wa CPA kimahitaji ya soko.NBAA pia wanatafutia kazi graduate wake nenda pale utaambiwa cha kufanya mkuu.

Back
Top Bottom