Jamani wadau naomba msaada, mana nimeangaika hadi nimechoka kutafuta kazi. Nina Ordinary Diploma in Accountancy GPA 4, Advance Diploma in Accountancy GPA 4.2. zote nimepiga IFM. Nilipomaliza Advance mwaka 2009 niliunganisha kufanya masters ya Accounting and Finance toka Mzumbe University, and on the same time nikawa nafanya CPA. CPA nilipass zote at 1st sitting na June mwaka jana nikawa nimeipata. Masters nina GPA 4.1, bado kudefend thesis tu. lakini wadau nimetafuta kazi tangu nilivyopata hiyo CPA hadi leo hola! nisaidieni basi ndugu zangu!
Sasa wewe ndugu unasoma soma tuuu na GPA zako utadhani unatunga mtihani mwenyewe itakuwaje? Si ujisalimishe kwa Prof. Jairo pale IFM akupe nafasi za kutumia elimu yako ya darasani? Mwenye makosa zaidi ni yule aliyekuwa analipa ada mfululizo. Wenzio wanafanya hiyo Diploma ili watoke wapige first degree baada ya hapo inatatosha unaingia ofisini unafanya kazi, CPA unapiga ukiwa ofisini, na masters pia unless uwe umekwenda kusoma nje ya nchi, Masters ya Accounting and Finance - Mzumbe siyo lazima kufanya full time unless unataka GPA za mapambo kama za kwako au ni kilaza.