nsee a muro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2012
- 241
- 124
heshima mbele wakuu. baada ya kushiriki humu jamvini kama mgeni leo nimeona nijiunge kisha nipatiwe ufumbuzi wa tatizo langu kutoka kwenu.
Mimi ni kijana ambaye elimu yangu ni ya msingi tu, kwakulitambua hilo ilinipasa kutumia kazi ya ziada kujiendeleza kimaisha kwani nilijua kusoma kushanitupa mkono. ukweli nilijiingiza katika kazi za ujenzi kama fundi mwashi ambaye nilishinda site na mafundi waliozoea hadi nikatoka na ujuzi ambao leo hii nautumia. sina hali mbaya kimaisha kwani kazi zangu za ujenzi zinanipa shavu nene na hasa ukizingatia kwamba nilibahatika kuwa mtundu sana wa kutengeneza building materials na kuuza hasa tofali, miguu ya tembo, urembo wa fensi, vyungu vya maua na vitofali vya uani.
kwa bahati mbaya sana niliwah kupata ajali mbaya wakati najenga nyumba moja(kupaua) nilidondoka na kupooza mguu wa kushoto hivyo nikaishia kuwa mlemavu wa mguu. lakin hali hii haiku nikatisha tamaa sana kwa msaada wa marafiki niliikubali na kufikiri nawezaje kujiendeleza kimaisha manake kama ni kilema tayari ninacho ila mguu upo na unatembea ingawa kwa kuuvuta.
kutokana na hali hii nilikuwa bize sana na kazi, na nafurah kuona ubize ule ulinisaidia sana sana kiuchumi kiasi kwamba sijutii wala kulaumu.lakin kama mjuavyo wapendwa moyo wa kupenda kuwa na mwenza huwa hauchagui aina ya mtu wala elimu wala kazi, hivyo nikjikuta nimeanguia kumpenda binti mmoja wa kizaramo. binti huyu tulikutana maeneo ya jirani ambako kulikuwa na site nasimamia ujenzi sasa yeye alikuwa mpishi wetu. kiukweli kwa macho ya kiume binti alinivutia sana sana, hivyo ikabidi nimweleze langu la rohoni.
Binti alikubali kuwa rafiki yangu na tulielezana mambo mengi ya tulikotoka. kwa uzuri binti alaikuwa muwaz akaniambia ana mtoto mdogo wa miaka 4 wa kike nikakubali mie kumlea mtoto huyo na ukweli nilimpenda sana binti hivyo sikuona tabu kumlea huyu mtoto. na hata kumsomesha. kwasasa binti yuko darasa la pili.
kama mjuavyo mapenzi yakikaa muda mrefu basi mtu hutamani ndoa, ndivyo ilivyokuwa kwangu, nikatamani nifunge ndoa niishi na binti, nikaanza taratibu za posa kulingana na desturi zao. bahati mbaya sana binti akawa mjamzito, aliponiambia nikamwambia basi usijali kwa vile tumeshaanza taratibu za ndoa tuilee mimba. kwangu mm ilikuwa kama baraka manake sikujua kama ningeweza kuzaa kutokana na ajali niliyoipataa so aliponiambia nilifurah sana sana.
tukiwa katikati ya taratibu ili tukabariki ndoa binti alianza kelele kwamba anataka kuolewa akiwa binti( hana mimba ) hivyo anahitaji hela aende akatoea ujauzito huo. nilikataa kabisa na kumwambia kwamba kama akiitoa basi ndoa hatakuwepo tena. nilifikiri ni utani mwezi uliopita binti alitoa ile mimba kienyeji. nilifwata na mtu akaniambia kwamba binti anaumwa, nikaenda pale nikamchukua kupeleka hosp kufika dr kumpima akasema katoa mimba sasa tumbo bado halijasafishika vizuri. nikaingia mfukoni nikamgharamia kwa dawa za sindano na vindonge na huduma za kusafishwa. kisha akarudi nyumban.
kwa hasira niliyoipata sikuweza kurudi kwao baada ya kumrudisha kutoka hosp. wiki iliyopita nimepata habari kwamba yule binti analiwa kipara na wajanja kwa buku maisha yake ni magumu. kiukweli haya mambo yamenichanganya sana sana kiasi kwamba naanza kuharibu kazini. naombeni msaada wenu je nifanyeje juu ya hali hii??
najua sieleweki kimaandishi lakini wachache mtaweza kunisaidia niondokane na msongo wa mawazo jamani. sikuwahi kupenda mtu zaid ya huyu binti na sijui kama kuna mtu anaweza kunipenda tena ama sitakiwi kupenda? je kwanini binti aharibu mimba inawezekana kweli isiwe ya kwangu ama ni kwamba hataki kuzaa?