Habari wanaJF,
Siku mbili zilizopita kumekuwa na purukushani ndani ya Bunge Tukufu la Tanzania.
Kilichofanyika wengi wetu tumekishuhudia na pia tumepata kutolea maoni sehemu mbalimbali.
kwa upande wangu namtazama spika wa Bunge, Mama Anne Makinda kwa sura ya huruma, Kilichotokea hakika naweza kukitafsiri kama hakuwa na jinsi!
Kifupi alionekana kuwa hakuwa na namna nyingine yoyote ile ya kuwezesha miswada hiyo kubarikiwa na "viti" vilivyomo ndani ya jengo la Bunge isipokuwa kwa kuwatoa nje walio kalia viti hivyo ili "viti" vibaki vikipitisha miswada hiyo.
Kwanini? jibu ni rahisi sana; WAKUBWA wameshaamua iwe hivyo! Siku zote hakuna wakumpinga BWANA MKUBWA! Ni nani ana ubavu huo!? yuko wapi ajitokeze!
Anne Makinda alijaribu kuwazuia walipotaka kulizima sakata la ESCROW; akapigana "ki uwoga uwoga" huku akitegemea zaidi sapoti ya wabunge wa pande zote mbili hatimaye kwa kupitia kwa Naibu spika kupitia kwa alichokiita kuomba ushauri wa wabunge, hatimaye sakata likafumuliwa na baadhi ya viongozi wakalipuka.
Hata hivyo kuna minong'onong'o isiyo rasimi kuwa naibu wa spika alipigwa adhabu kwa kuruhusu bomu hilo kulipuka wakati alikuwa na uwezo kulizuia! Angezuiaje wakati wabunge wa pande zote mbili walilishadadia?
Asingeweza kutofautia na wabunge wenzake wa upande wake! Sasa hili la miswada ya gesi na Petroli, Anne Makinda kakosa sapoti ya wabunge wa upande wake!
Waliolivalia njuga si wenzao, sasa angepitia wapi kutofautiana na WAKUBWA wakati WAKUBWA walisha viteka viti vyote vya BUNGENI! Viti vyote vimeshatekwa, sasa unadhani yeye angefanyaje? Jibu ni rahisi tu; Kuwatoa nje wale wote wanaong'ang'ania kukalia viti wakati viti vyote vimeshabukiwa na WAKUBWA na wanawakalisha hapo wanao wataka wao!?
Yamkini Wangejitokeza hata wabunge wa Upande wake watatu tu wa kuungana na hawa wengine wa upinzani, huenda Mama ANNE angejitutumua kusema neno kwani angepata la kujitetea kuwa "nilikuwa na wenzangu"! Sasa woooote, wanasema: Ndioooooooooooooooo!! Yeye ni nani aseme HAPANA!
Wananchi tumeliona hilo,wenye akili wamesha-note,walioruhusu mabwana wakubwa kugawana Gesi na Mafuta tena kama walivyogawana madini.
Zigo hiloo uliliweka mwenyewe madarakani kwa kulipigia kura au kwa kutoenda kupiga kura,sasa limejidhirisha muda mwafaka.
Sio mbali ni mwezi wa 10 tu unao uwezo kwenda kuliondoa...Umejiandikisha?
Usiendelee kulalamika,hayo yana mwisho mwezi wa 10 nenda kalitue zigo unalohisi limekulemea.