le madame
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 476
- 263
Natambua uwepo wako humu ndani ya JF,
Soma tuu maana hamna jinsi asome!
Tumekuwa nae kwenye uhusiano hadi kufikia kutambulishana kwa wazazi, Mungu si athumani akapata ufadhili nchi za wenzetu kusoma huku nyuma akiniacha mjamzito, kitu ambacho alikifurahia sana kwa kuwa age imeenda sana na hakuwa na mtoto, tumewasiliana vizuri nikalea mimba kufika miezi 5 vitimbwi vikaanza ikiwamo kunipa shughuli nzito zilizopelekea mimi kusumbuka sana na ujauzito.
Tulikubaliana aliahidi pia kutuma vitu vya mtoto mapema! Lakini haukuwa hivyo, kuna mzigo aliagiza toka huko kuuzwa hapa Dar, nikaona bora nichukue pesa yake kwa maandalizi ya mtoto kwa kuwa nilishaona zengwe.
Kufikia miezi 7 akakata mawasiliano kabisa hadi nikamsahau, Mungu kanijalia nimejifungua salama sasa anarudi kutaka ita mwanangu! Je nimchukulieje huyu mtu?Huko aliko ana mambo chungu mzima nilipomuuliza hatukuongea na nikaachana nayo, akirejea anakujafunga ndoa na mwanamke mwingine huku akiacha maswali mengi kwa ndugu na jamaa zake, sasa, sioni umuhimu wake kwetu mimi na mwanangu na hata uwajibikaji japo salam tu ni zero.
Nisaidieni mawazo wanajamii.