sifongo
JF-Expert Member
- Jun 5, 2011
- 4,896
- 5,302
Habari wanajamvi, naomba nikiri na kujutia dhambi niliyofanya mimi na mwenzangu (aliyekuwa girlfriend wangu). Miaka kadhaa nyuma nilikuwa na girlfriend nilimpenda naye alinipenda japo nilikuwa najua ananichiti coz sikuwa na hela ya kutosheleza mahitaji yake, kiukweli alikuwa anapenda maisha juu.
Tulidumu kwa miaka 4 katika uhusiano wetu na katika dhambi kubwa tuliyofanya ni kuwa tulitoa mimba 3, mbili niliridhia na ilipokuja ya 3 nilimuambia tuzae kwani tatizo ni nini, nyumba ya kukaa bure ipo, yeye anafanya kazi na mimi namaliza masomo muda si mrefu nitakuwa na ajira ya kudumu kwani hapo mwanzo nilikuwa naunga unga kazi, huyu binti alikataa kata kata tuzae na akaja kuitoa hiyo mimba.
Siku moja akanimbia wanakwenda kwenye sherehe ya kiofisi hivyo hatutakuwa wote wikiend hiyo nikamuambia poa, na mimi nikamtafuta mshikaji wangu mmoja nikijua wikiend nyingi anakuwaga na kazi za shooting kwenye maharusi, japo nikampe tafu hata ya kuvuta waya wa taa na ikawa hivyo, ishu ilikuwa ni ISTANA pale victoria.
Sitaisahau hii siku, mmoja wa waalikwa katika hiyo harusi ni demu wangu na alikuwa na mshikaji mwenye hadhi ya juu si kama mimi nakiri hivyo, tukaonana uso kwa uso akaduwaa nikajitahidi kumpotezea nikiogopa nisije kutambulishwa kama kaka mtu, jamaa yangu aliona mchezo wote akajua kabisa siwezi kumudu kukaa pale na ilikuwa hivyo, nikatoka nikaenda home, nilipata uchungu wa ajabu lakini sikuwa na jinsi, nilijaribu kupiga simu iliita na kukatwa kisha ikazimwa na ukawa ndio mwisho wa uhusiano wetu.
Miaka imepita nina mke na binti wa miaka miwili na yeye bado hajaolewa, maisha yanasogea ni juzi tu nimekutana na rafiki yake pale jojis akaniuliza kama bado nawasiliana na shoga yake nikamuambia sio sana, japo kuna muda tunasalimiana kwa simu, basi katika maongezi ndio akaniambia kuwa hata jana yake walikuwa wote hospital kwani ana matatizo ya kutopata mimba, amejaribu mara kadhaa na ishu imekataa kabisa, roho iliniuma nikikumbuka tuliyofanya huko nyuma yeye hajaniambia hilo tatizo ila natamani kumpigia nisikie toka kwake.......nisaidieni wanajamvi kufanya maamuzi, nimpigie au nitulie nisijeonekana mwanga.