Nimrod Mkono kakisusia kijiji, JF okoeni kijiji hiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimrod Mkono kakisusia kijiji, JF okoeni kijiji hiki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wiseboy, Jul 14, 2012.

 1. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,705
  Likes Received: 1,886
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mkazi wa kijiji cha ujamaa Bumangi kilichopo wilaya ya musoma vijijini, ambalo ni jimbo la nimrod mkono na ni kijiji cha tatu toka nyumbani kwa mbunge wangu nimrod mkono.
  Nimezaliwa, nimekulia na kupata elimu ya msingi na upili hapo kijijini kwetu ,kabla ya kukiacha kwa kwenda kujiunga na masomo ya advance na badae chuo kikuu mikoa mingine.
  Niende moja kwa moja kwenye mada
  toka nikiwa mdogo kijiji changu kinakabiliwa na ukosefu mkubwa wa maji, japokuwa ukiwa kijijini kwetu ukinyanyua macho upande wa kaskazini utaona maji ya mto mara yakitiririka kuingia ziwa victoria, nikikumbuka siku moja tulitolewa darasani nikiwa kidato cha tatu, huko kisimani kulitokea ugomvi wa maji ya kwenye vidimbwi kati yetu wanafunzi na wanakijiji, nakumbuka nilimwagiwa tope shati langu la shule.......nikikumbuka adha hii ya maji kwa sasa natokwa machozi.
  juhudi nilizofanya binafsi kulitatua tatizo hili
  1
  :nikiwa mwaka wa kwanza nilifika kwa mkono jijini dar es salaam ili nimuone na kumfikishia kilio hiki cha shida ya maji wanayopata wazazi, ndugu, na wanajamii kwa ujumla pale kijijini lakini kwa bahati mbaya walinzi hawakuniruhusu niingie pale kwake, na hata nilipojaribu kumsubiri nje ya geti, alinipita bila kusimama akiwa ndani ya gari lake.

  2.
  nikiwa mwaka wa pili nilijaribu kutafuta ushauri kwa baadhi ya maprofesa pale chuoni kuona kama nitapata msaada wa kupata wadhamini wa kusambaza maji kijijni kwetu, japo sikufanikiwa kwani walinishauri niconcetrate na masomo kwanza there after ndo nideal na hili suala
  facilities zilizopo kijijini kwetu
  miaka ya huko nyuma kulikuwa na huduma ya maji, japo miundo mbinu haikufanyiwa matengenezo hivyo kushindwa kufanya kazi......kwa kigezo hicho kijijini kwetu kuna matank makubwa ya kuhifadhi maji, na pia kuna steel pipeline ambazo bado zipo connected, na pia umbali wa kilomita 20 kuna chemi chemi yenye maji mengi yanaweza kuvunwa na kujazwa kwenye matank.
  DHUMUNI LA KULETA HII MADA HAPA
  1.
  Kama kuna mtu ana email ya nimrod mkono humu naomba amforwadie hii thread yangu
  2:sitaki kukata tamaa, naomba wana jf kama kuna mtu anajua funders wanaoweza kudhamini mradi wa maji kijini anisaidie link yao
  3:kama kuna mtu ana proposal format ya jinsi ya kuandika project proposal juu ya maji, please anitumie kupitia
  mmattuh@gmail.com
  please toka moyo mwangu naumia sana na hili tatizo la kijiji changu, naombeni mawazo yenu na msaada wenu kulifanikisha hili suala, nifanyeje? karibuni wakuu
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Taarifa zimefika mahali pake mkuu, subiri hoja za jukwaa kuhusu kitu gani kifanyike.
   
 3. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  du ndgu hao watakuona muhimu kipindi cha kampeni, kuhusu hilo tatzo lako kuna tym TBL walikuwa na programu ya bila maji hakuna uhai cjui imeishia wp, cheki hyo wana fomu itakayojazwa na kijiji.
   
 4. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  pole sana ndugu kwa adha wanayopata ndugu uliowaacha huko kijijini..binafsi napafahamu bumangi japo si mwenyeji wa kijiji hicho..nackitika sana nkickia hivyo kwan huyu jamaa anachojua ni kununua watu wanaompinga..kwa sasa amekuwa mzigo kwa jimbo la musoma vijijini...hapa ni sehemu husika na atapita kuona ujumbe..inasikitisha kwan bumangi ni jiran kabisa na,butiama,busegwa!!
   
 5. mwitaz

  mwitaz JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Nenda Musoma Mjini ukamuone jamaa mmoja anaitwa Dr. Kayombo yeye ni mwajiriwa wa taasisi moja ya kanisa la Anglikan inayojihusisha na utoaji misaada katika miradi kama hiyo ya maji huko Mkoani Mara. Zamani wakati niko kijana niliwahi kwenda huko mkoani Mara nikakutana na mradi wa maji safi ukiitwa HESAWA vipi haupo haukuwafikia?

  Halafu mkuu kama kuna steel pipes (huwa zinaoza hizi) tatizo ni nini sasa manake inaonekana kuna miundombinu au mnakosa mashine ya kusukuma maji au mabomba yameoza?
   
 7. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  jwhq fjrh3g cx
   
 8. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Utasikia yale majibu yao tu....
  Tume sikia,tupo kwenye upembuzi yakinifu....
   
 9. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Acha Bumangi tu, hata pande hii ya Wajita, Waruri na Wakwaya, hana Muda kabisa, ukienda Mugango, Majita nk nk ni aibu tupu. Hili jimbo kwanza ninabidi ligawanywe, pamoja na kujenga zile shule, kazijenga upande mmoja tu wa Wazanaki na Wakurya! Huyu mzee inabidi atoke awaachie watu wapige mzigo. Haingii akilini Sehemu kama Bumangi, Majita, Mugango kuna vyanzo vingi tu vya maji, halafu watu hawana maji, hii ni dharau sana!
   
 10. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapo kwenye red umefanya nimecheka sana
   
 11. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Bumangi na Zanaki kwa ujumla ina human resource kubwa sana, wengi wako hapo Dar, nadhani hawana utashi wa kuendeleza kijiji chao vingine wangeshatatua hiyo shida siku nyingi. Jaribu kuongea na watu hapo Dar utaelewa ninachosema.
  Ushauri wangu ni kuwashawishi WAMANGI waliopiga hatua kubwa za kimaendeleo kukumbuka nyumbani. Achana na Mko huyo hana sera.
   
 12. b

  bdo JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280

  Ila nasikia nyie wa upande wa Zanaki (Bumangi, Makutano, Buhemba, Butiama, Butuguri, Kyarano, Lwamkoma, Bisyare, na wote along Musoma - Bunda road) hampendi huyo mbuge wenu, tofauti na watu wa upande wa ziwani, I mean Majita, that is why huyo mzee anawashiti sana, alichofanya amewajengea tu shule za sekondari nzuri na nyingi tu ili msome na muelimike - na ukizingatia mnamdharau kwa kuwa ni mzanaki mwenzenu na hamkumuona wakati mwl.akiwa hai (infact mnamsema kama mwl angekuwa hai wala asingekuwa mbuge kwa mnajua ni fisadi), wakati wenzenu wa ziwani wanakula maisha na wanamuona ni mkombozi na baba yao..and mind you huyo mzee alikubali jimbo lake liwe wilaya mbili Butiama na Musoma vijijini, ila hataki kuwe na majimbo mawili (musoma vijijini na Butiama) akiogopa nyie wazanaki mtamnyima kura kama atagombea jimbo la Butiama na wakati huo hawezi kwenda ziwani wakati yeye si asili ya huko..ushauri wangu, ombeni muwe na jimbo lenu la Butiama ili mtoe hukumu ya haki kwake, Ombeni kikao naye si cha kussurrender ila cha kumwambia ukweli kwamba tumekuchoka.
   
 13. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu pamoja na uelewa wako wa maeneo hayo but u seem to miss something here, huko majita huyo jamaa hakuna kitu cha maana alichofanya hata sasa, zile shule amejenga kuenzi utemi wa watuguli na hana lolote, hebu taja shule moja nzuri aliyojenga huko Majita mkuu, vipi kuhusu Kyagata ambako hadharauliki kafanya nini cha maana huko?
   
 14. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kaka nafikiri ungejielekeza kwenye hoja kuliko kushambulia utu wa mtu. Jitahidi kuficha hisia zako kuhusu personality za watu.
   
 15. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,705
  Likes Received: 1,886
  Trophy Points: 280
  asanteni waungwana, ni kweli kabisa kijiji chetu kina watu maarufu na wenye fedha ila hatuna utamaduni wa kuangalia nyuma tulipotoka, mm nitaangalia nyuma daima, kama wapo hapa plz muone aibu na mnitafute tupeleke maji bumangi, tuache sifa za kurudi kijijin na kusifiwa fulan au ukoo wa fulan una hela bla kuleta tija kwenye jamii
   
 16. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,705
  Likes Received: 1,886
  Trophy Points: 280
  sure mkuu, ukitoka busegwe nyumbani kwa mheshimiwa unaingia muriaza, then bumangi ni nearby, anyway its ma hope kwamba nitafanikiwa one day katika safari yangu ya maisha katika uso huu wa sayari ya 3
   
 17. a

  admiral elect Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  inawezekana kabisa wapo wengi sana maana hat huyu prof.dr. mj. wa hapa kama unaenda tegeta si nilisikia naye ni wa huko? anyway ngoja nimpigie bridedia mts anipe ufafanuzi,vinginevyo kila la kheri
   
 18. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,705
  Likes Received: 1,886
  Trophy Points: 280
  asante mkuu, usemacho ni kweli kabisa, huu mradi wa hesawa ulikuwepo, na umesaidia kiukweli lakini tatizo ni kwamba walichimba visima na kusimika mabomba ya maji ya kupampu maeneo ya chemichemi ambayo yapo umbali na makazi ya watu yapata kilomita 15 na kuendelea mfano walisimika visima eneo la kisawakwe na kyawamang'we............kuhusu swali lako la steel pipe ni kwamba kuhusu suala zima la kuvuta maji toka chemichemi hasa toka maeneo ya 'nyabirango' kunahitajika facilities hasa pipes lakini kwa bahati nzuri hizi pipes bado zipo japo kwa vipande yaani sehemu na sehemu hivyo basi installation cost katika upande wa pipes unaweza kuwa chini kidogo so hii ni kama opportunities that we already have in hands..............thanks
   
 19. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Juzi nimekaona haka kazee kanarandaranda mitaa ya mlimani city,hakana mbele wala nyuma ilmradi tu anauza fuvu,kumbe jimboni kwake kuna shida ya maji hivyo. Shame on him,dhaifu.
   
 20. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada acha kulalamika Bumangi ni miongoni mwa vijiji vilivyosheheni wasomi wengi na wa kada mbalimbali. wasomi hao walipatikana wakati wa awmu ya kwanza na ya pili wakati Nyakiran'gani akiwa mwenyekiti wa scholarship board. wasomi wote mlio nao wameshindwaje kujimobilise mkapata maji na mbona usiwasemee watu wa Muriaza, Kizaru ambao kwanza hawwkupata upendeleo wa ndgu yako Nyakirang'ani.
  Hivi kweli akina Tom Nyanduga na wenzake wote wanashindwa kupata wafadhili.kwa hili usimlaumu mkona hawezi kufanya yote. mengine wananchi nguvu zetu zinatakiwa,ebu tupe kwa ufupi ni juhudi gani zimefanywa na nyini wanachi ili mbunge awasaidie.
   
Loading...