NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu

Nilidhani una hoja kumbe una chuki. Ungeliuliza ukapata ufafanuzi wa hizo points. You should not attack them seek clarification... wapo humu wangelikupa clarification. Mfano point na. 1. Research yote ilikuwa undertaken na NIMR staff and publication on this is wholly acredited to NIMR as first authors and last authors.
Basi nakuacha
Ok, clarify.
Kwahiyo hizo ndizo kazi NIMR imefanya tangu 1980?
  1. Hakuna tangible product waliyogundua ikaingia kwenye soko la tiba
  2. Hakuna medical procedure mpya waliyoigundua ikaingia kwenye mfumo wa tiba kwenye mahospitali yetu
  3. Hakuna changamoto ya tiba waliyotatua, wanazunguka tu kugawa dawa za matende na mabusha zilizofanyiwa utafiti nchi nyingine tangu zamani za kale
  4. Hakuna ujuzi mpya waliogundua usaidie madaktari na manesi wetu katika kazi zao. Hivi katika vyuo vya madaktari, manesi na wafamasia vilivyoko nchini, kuna kitu gani angalao hata mada moja tu wanayofundishwa ambayo imegunduliwa NIMR? Watu mko busy kugawana perdiems halafu mnaita "capacity building", feki tu.
Jibu hoja kwa hoja, acha kulalama
 
Wewe kweli nutcase, unafikiri Marekani ni wazungu tu! Mmekaririshwa propoganda mpaka vichwa vimebaki kama mifuko ya kubeba meno tu.
Haya waangalie Mugabe, Kagame, M7 ,Gaddafi na Kinjikitile.
Hizo Styles zenu za wakina Kinjekitile zingekuwa zinawachanganya maadui mngebaki mafukara miaka 60 baada ya uhuru huku hao "wazungu" wakijichotea mali tu.
Halafu some people bana, yaani kidooogo tu!! plus kila kitu ''angalia Wazungu'' hao wazungu waliwapa nini huko matakoni zenu??, bila hata aibu, afadhali ungesema niangalie serikali ya Mugabe, Nyerere, Mwana Marundi, Mkwawa, Faraoh!, Moi!!

hao wazungu ni wao na sisi tuna style zetu!! yaani popote TISS unakomaa mtu! ili kuwachanganya maadui! ndo mipango na style yetu!! yaani style ambayo haipo Duniani sasa.
jinga km wewe unaona CIA ndo bora? mpyuukfuuu!
unatamani kuiga sababu ni wazungu!!! ungekuwa karibu ningekupiga kofi ukanye! umuonyeshee mke wako vizuri nilivo kuchapa kenge kabisa!
 
1. Miaka yote zaidi ya 40 ya uwepo wa NIMR, wameongeza nini katika ufahamu wa mambo ya tiba Tanzania? Ni utafiti gani waliowahi kuufanya ukaleta tija katika kupunguza au kuondoa tatizo lolote la kiafya? Jibu ni zero.

2. Hivi kuna dawa yoyote sokoni (dawa ya maana yenye viwango stahiki, na siyo ile michanganyiko ya pilipili kichaa na tangawizi waliyoiga kutoka kwa waganga wa kienyeji) au vifaatiba hospitalini au maarifa mapya yoyote ya tiba yaliyowahi kugunduliwa na NIMR? Jibu ni hakuna.

3. Nina jamaa zangu nimesoma nao History na English pale Mlimani, eti nao wanafanya kazi NIMR wananiambia wanaitwa "Research Scientist". Hiki ni kituko! Scientist wa history, English, Kiswahili, sociology na Political Science anafanya nini kwenye MEDICAL research? Ingekuwa HEALTH research ningewaelewa kwa kuwa afya ni suala mtambuka lenye mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayoathiri afya, lakini medical research ni mambo ya maabara, madawa, mawodini huko wanakotibiwa wagonjwa, operations mpya mpya kama hizi za moyo na figo nk. Tunasikia huko Jakaya Kikwete institute, Benjamin Mkapa Hospital na hata MOI wakifanya innovations mpya mpya, lakini mchango wa NIMR kwenye hizi innovations uko wapi?

4. Mkurugenzi wa NIMR ni profesa wa Marine Biology. Hii ndiyo medical research? Hakuna medical researcher nchi hii mwenye sifa ya kuwa mkurugenzi wa NIMR? Sasa marine biologist na medical research wapi na wapi? Ndio chanzo cha kwenda kudesa michanganyiko ya waganga wa kienyeji na kutuambia ni dawa za korona!

5. Kwa ujumla NIMR ni kimeo, haina faida kwa nchi, ifutwe tu.

Institute Profile​

Establishment and Mandate

The National Institute for Medical Research (NIMR) is a parastatal organization under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children (MoHCDGEC). NIMR was established by the Parliament Act No. 23 of 1979 and became operational in 1980; holding the following mandates:
    • To carry out and promote the carrying out of health research designed to alleviate disease among the people of Tanzania;
    • To carry out, and promote the carrying out of, medical research into various aspects of local traditional medical practices for the purpose of facilitating the development and application of herbal medicine;
    • In co-operation with the Government or any other person or body of persons, to promote, or provide facilities for, the training of local personnel for carrying out scientific research into medical problems;
    • To monitor, control and coordinate medical research carried out within Tanzania, or elsewhere, on behalf of or for the benefit of the Government of Tanzania, and to evaluate the findings of that research;
    • To establish a system of the registration of, and to register, the findings of medical research carried out within Tanzania, and promote the practical application of those findings for the purposes of improving or advancing the health and general welfare of the people of Tanzania;
    • To establish and operate systems of documentation and dissemination of information on any aspect of the medical research carried out by or on behalf of the institute;
    • Carry out, and promote the carrying out of, research and investigation into the causes and the ways of controlling and preventing the occurrence in Tanzania of particular diseases or a category of them;
    • In co-operation with the Government or any person or body of persons, carry out and promote the carrying out of, basic, applied, and operational research designated to provide effective measures for the control of diseases endemic in Tanzania.
Institute Profile – NIMR Tanzania
 

Institute Profile​

Establishment and Mandate

The National Institute for Medical Research (NIMR) is a parastatal organization under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children (MoHCDGEC). NIMR was established by the Parliament Act No. 23 of 1979 and became operational in 1980; holding the following mandates:
    • To carry out and promote the carrying out of health research designed to alleviate disease among the people of Tanzania;
    • To carry out, and promote the carrying out of, medical research into various aspects of local traditional medical practices for the purpose of facilitating the development and application of herbal medicine;
    • In co-operation with the Government or any other person or body of persons, to promote, or provide facilities for, the training of local personnel for carrying out scientific research into medical problems;
    • To monitor, control and coordinate medical research carried out within Tanzania, or elsewhere, on behalf of or for the benefit of the Government of Tanzania, and to evaluate the findings of that research;
    • To establish a system of the registration of, and to register, the findings of medical research carried out within Tanzania, and promote the practical application of those findings for the purposes of improving or advancing the health and general welfare of the people of Tanzania;
    • To establish and operate systems of documentation and dissemination of information on any aspect of the medical research carried out by or on behalf of the institute;
    • Carry out, and promote the carrying out of, research and investigation into the causes and the ways of controlling and preventing the occurrence in Tanzania of particular diseases or a category of them;
    • In co-operation with the Government or any person or body of persons, carry out and promote the carrying out of, basic, applied, and operational research designated to provide effective measures for the control of diseases endemic in Tanzania.
Institute Profile – NIMR Tanzania
Katika haya yaliyoorodheshwa NIMR imefanya yepi na products zake zinatumika wapi? Tutajie katika kila lengo lililoorodheshwa hapo nini kimefanyika na sio zile blah blah za kudesa
 
Nina jamaa zangu nimesoma nao History na English pale Mlimani, eti nao wanafanya kazi NIMR wananiambia wanaitwa "Research Scientist". Hiki ni kituko! Scientist wa history, English, Kiswahili, sociology na Political Science anafanya nini kwenye MEDICAL research? Ingekuwa HEALTH research ningewaelewa kwa kuwa afya ni suala mtambuka lenye mambo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayoathiri afya, lakini medical research ni mambo ya maabara, madawa, mawodini huko wanakotibiwa wagonjwa, operations mpya mpya kama hizi za moyo na figo nk.
Hiki kweli ni kituko, Ni Tanzania pekee
 
Naona kuna ligi mbili hapa ... Yangu macho .. ila si sahihi kuifuta hii taasisi badala yake waweke watu sahihi .. (Medical Research ) inahitaji medical people sio sociologists waliojazana pale ...
 
Hapo namba 3 utakuwa unakosea sana.Kwa Tanzania mtu bora ni yule mwenye elimu kubwa mfano PhD. Huyu anaweza kufanya chochote bila kuhojiwa.

Hata kama kazi ya kukamua maziwa ingekuwa na mshahara mkubwa sana,angetakiwa kufanya mtu mwenye PhD.Sasa watashindwa nini kufanya kazi NIMR
 
hamna kitu kama hiko. research huwa inaanzishwa na taasis yenyewe. halaf wanatafuta wadau wa ku support.
wale ni support tu, sio ku control nn wafanye.

Ni taasis yenyewe haiko vizuri ndio maana.
Inaelekea haujui kitu eneo hilo
 
Hapo ndio umeandika nini?

Kwahiyo wewe ni miongoni mwa wale wasiokuwa na taaluma ya tiba mliojazana NIMR na kuigeuza kuwa genge la wadesaji na wapiga dili? Kafanye kazi ya taaluma yako kama tunavyofanya sisi wengine, utaheshimika. Hebu ona mlivyodharaulisha NIMR sasa imekuwa kikosi cha wachekeshaji wanaowaambia watu kuwa juice ya tangawizi na pilipili kichaa inatibu corona!

Wewe uliyejiongeza na kuvamia ajira za kudandia huko NIMR umechangia nini kwenye medical research? Wewe ni "research scientist" wa kitu gani, una taaluma gani?

Wataalam wa Muhimbili, Jakaya Kikwete, MOI na ile hospitali ya Dodoma ya Benjamin Mkapa wanafanya operesheni kubwakubwa za moyo na figo, na sasa wamechangia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje kwa shida hizo. Wewe huko NIMR na sociology yako uliyojiongeza umechangia nini zaidi ya ufujaji tu wa fedha za umma kwenye tafiti zisizokuwa na tija? Medical Research gani mlizofanya, hebu orodhesha hapa na faida zake kwa nchi.
Wataalam wa Muhimbili wangepata dawa ya korona?
 
Hapo umekuja vizuri.
  1. Kama NIMR haipewi hizo 6%, inapewa % ngapi? Imefanyia nini hicho ilichopewa miaka yote hii? Imeleta majibu ya changamoto zipi katika masuala ya tiba?
  2. Tanzania pia kuna sekta binafsi. Je, NIMR haizioni hizo sekta binafsi ikaziendea for funding, au inakatazwa?
Nisome kwa utulivu, pesa inayotengwa kwa ajili ya utafiti hairidhishi, nenda COSTECH kawaulize kama wamepata pesa kiasi gani kwa ajili ya shughuli za utafiti. Medical research zinahitaji pesa nyingi na miaka mingi zimekuwa zinapata support ya wazungu ambao na wenyewe wana agenda zao hasa kupata sampuli/takwimu. Innovative medical researches mara nyingi zinafanyika kwenye maabara za mabeberu. Jambo lingine medical research inaweza isije na matokeo tarajiwa ndo maana zinahitaji muda, pesa nyingi na commitment, hadi ku-pin down technological innovation au kutengeneza aina mpya ya dawa, aina mpya ya chanjo na vifaa tiba inahusisha ku-review kazi za researchers wengine waliofanya kitu kinachofanana na huo utafiti na inaweza kuchukua miaka mingi, hata 30 kupata breakthrough.......

Sekta binafsi ku-drive research wao ndo wanajua wanahitaji kitu gani, mfano labda wanahitaji aina mpya ya dawa ya kutibu kansa, wao ndo watapeleka hilo wazo kwenye taasisi husika na pesa ambayo wapo tayari kugharamia ili huo utafiti ufanyike kwa mafanikio, then taasisi itatangaza kwa watafiti waweze kuandika proposal zao kufuatana na malengo ya kampuni inayogharamia huo utafiti. Kuna jamaa anawaponda medical researchers wa NIMR eti wanafanya simple surveys, unataka wafanye complex medical researches kwa vibajeti vya milion 10.

Tatizo lenu mangwini mnafikiri scientific researches ni sawa na kusoma story za mtemi mirambo na chifu mangungo wa msovero. Watafiti wanatakiwa kutumiwa kwa kuwapa bajeti ya kutosha ili waweze hata kulala maabara, siyo mnawalipa mshahara kiduchu hawana hili wala lile na wenyewe wanakata tamaa maana hawana motivations zozote, wanaona viongozi na wanasiasa ndo wananepeana mashavu kwa kula bata. Sasa magonjwa kama covid yakitokea ndo mnaanza kuwatafuta hao NIMR, pambaneni tu na hali zenu, nyie si mnakula vinono hamuwezi kuugua, utafiti gharama...na bado.
 
Tatzo la NIMR ni kutokukubali kuendana na wakati yani kwenye upigaji ndo wako vizuri hasa kwenya uendeshaji wa miradi ya malaria, kichocho, na matende hapo huwa ni kula hela tu, ila kwenye tafti ni blaa blaa tu

Hizo kazi za kuendesha miradi ya malaria, kichocho na matende zingeweza kufanywa na watu wa idara mojawapo pale wizara ya afya na kwenye halmashauri zetu, siyo na taasisi ya medical research. Hizo ni public health projects, na hazihitaji kuongozwa wala kusimamiwa na medical researchers, hizo hata watu waliosomea community development na sociology ndio kazi zao kupita kwenye jamii kuhimiza matumizi ya chandarua, matumizi ya choo bora nk. Tunaona hata huku mitaani watu wanaohimiza kwamba "Usichukulie Poa Nyumba ni Choo" ni akina Mrisho Mpoto na Shilole, wasanii wenye influence kwa hadhira.
Medical Researchers hawapaswi kuvamia kazi ambazo sio medical research. Wanapaswa wafanye tafiti za tiba walete majibu ya changamoto zilizoko katika tiba ya binadamu: dawa bora, vifaa tiba, mbinu bora za operesheni na mengine ya aina hiyo katika tiba.

Sasa hawa wenzetu huko NIMR baada ya kuona medical research imewashinda ndio tunawasikia kila siku wakiimba matende na mabusha na kugawa dawa za minyoo mashuleni. Dawa hizo zilitafitiwa zamani na kuthibitishwa ubora wake huko zilikotoka kwa mabeberu, hapa kwetu zimepata usajili na kuruhusiwa kutumika, eti NIMR wako busy kugawa dawa! Hiyo kazi hata ukimpa mwalimu wa shule ya msingi ukamwambia gawia kila mtoto kidonge kimoja anywe na glasi moja ya maji atashindwa?
Nijuavyo, programmatic activities za malaria zipo chini ya NMCP na hizo za matende na kichocho zipo chini ya NTDCP. Hivyo ni vitengo vya wizara ya Afya, na siyo NIMR. Hivyo kusema NIMR wanatuma pesa za miradi ya malaria na matende ni sababu ya kutofahamu ukweli. Yaani ni kama mtu kasimuliwa tu kama vile tunavyosikia mitandaoni kuwa barakoa za kutoka nje ya nchi zona virusi vya korona na sisi tukavalia njuga
 
Naona kuna ligi mbili hapa ... Yangu macho .. ila si sahihi kuifuta hii taasisi badala yake waweke watu sahihi .. (Medical Research ) inahitaji medical people sio sociologists waliojazana pale ...
Issue si watu sahihi. Watu sahihi naamini wapo, unless uwe na uhakika kuwa hawapo. Je, taasisi imewezeshwa kiasi gani kufanya tafiti zenye kuleta matokeo mnayoyataka? Je, mwenye taasisi yeye anataka matokeo gani na ameyagharamia kiasi gani? Matokeo makubwa hayawezi kuja kwa kuyatamani tu.
 
okay.. ww unaejua? nieleze we unajua nini?
Unaanzishaje research bila pesa? Wadau wa kusupport ninaamini unamaanisha funding agencies. Kama ni hao, basi wao hucirculate calls for funding opportunity, na zinakuwa zinasema wanataka kutoa pesa kwenye tafiti za uelekeo fulani. Ni jukumu lako kupima interests zako na competency individually au kitaasisi kisha kupambana na applicants wengine duniani au nchini au kwenye ukanda kulingana na scope. Kumbuka hapo idea ya proposal utakayoshindsnisha lazima iwiane na vigezo wenye fedha walivyotoa. Kama mkiona havifai, hamlazimishwi ku apply.

Kifupi, iambieni serikali na wadau wengine wawekeze kwenye tafiti za kipaumbele badala ya kutaka tu NIMR ifutwe.
 
Back
Top Bottom