NIMR: Asilimia 45 ya watoto wachanga wakutwa na Virusi vya homa ya ZIKA Tanzania, asema Mwale Malecela

Kizazi kmejaa vilaza wa kumwaga bila ya Zika sijui Hali itakuaje Kama Baba Kilaza akipata Mtoto Mwenye Zika?
 
,
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu, NIMR imethibitisha kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Mwele Malecela,virusi hivyo vimepatikana mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania na Mkoani Geita, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Utafiti huo ulifanyika kutokana na uhalisia kuwa kuna mazingira yanayowezesha kuzaliana kwa mbu wanaoeneza virusi hivyo.

Dkt Mwele Malecela alizungumza na BBC na anafafanua kugundulika kwa virusi hivyo.

Chanzo: BBC
hicho kirusi kilirukarukaje, toka brasil hadi east africa tz bila kuripotiwa nchi nyingine za africa? basi wange tupatia na picha za walio azilika na zika morogoro, ili tuamini
 
Hivi kwa hili janga kama kweli morogoro na geita lipo#mpango wa uzazi unahusika sana maeneo hayo wana JF ase
 
Kama ni kweli, wabongo tumeisha. Sasa hivi hospitali hamna dawa ndio ZIKA inaingia ! Kweli tuta-zika wengi. Na hali ilivyo ngumu hata hela za vidonge vya kutuliza maumivu hakuna. Na kama ZIKA ipo, watalii ndio bye bye! Uchumi utazidi kudorora. Tena ukame ndio huo, na pale ambapo hakuna ukame kuna mvua za ghafla zinazobomoa majengo. Tutaishije?
 
Hakuna zika kirusi,, huyo ni zika wa kusahaulisha yalipo. OVER!
 
ASILIMIA 43 YA WATOTO WACHANGA WAKUTWA NA HOMA YA ZIKA

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

ASILIMIA 43.8 ya watoto wachanga 80 kati ya watu 533 ambao walichukuliwa sampuli na kupimwa, wamegundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya homa ya Zika, imeelezwa.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki Bugando hivi karibuni, umethibitishwa kuwapo tatizo hilo.

Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela, alitoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya taasisi hiyo kwa mwaka 2016.

Alisema utafiti huo ulilenga kuainisha uwapo wa maambukizi ya virusi vya Zika katika jamii ya Watanzania na kuangalia athari ya maambukizi katika kusababisha watoto wanaozaliwa na ulemavu.

“Tulipima sampuli za damu kutoka kwa watu 533. Kati yao, watoto wachanga 80 walizaliwa na ulemavu wa viungo mbalimbali. Kati ya waliopimwa asilimia 15.6 waligundulika wameambukizwa virusi vya Zika.

“Kati ya wale watoto wachanga 80 waliozaliwa na ulemavu, asilimia 43.8 walikuwa wameambukizwa virusi vya Zika. Utafiti unaendelea kujua ukubwa wa tatizo hili,” alisema.

Alisema kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi miaka michache iliyopita, NIMR kwa kushirikiana na Kampuni ya dawa ya Janssen & Jansen, ilifanya majaribio ya awali ya chanjo ya Ebola (Ebovac) katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria.

“Tulihusisha watu 25 na wote walimaliza dozi ya chanjo kama inavyotakia. Matokeo yameonyesha chanjo hii (Ebovac) ni salama kwa binadamu na ina uwezo wa kujenga kinga dhidi ya virusi vya Ebola, tunaendelea na ufuatiliaji kutathmini athari za muda mrefu za chanjo hiyo,” alisema.

Mbali na ugonjwa huo, Dk. Malecela alisema taasisi yake ilifanya pia utafiti kwa kundi la vijana waoendesha pikipiki maarufu bodaboda Agosti, mwaka huu kwa lengo la kutathmini viashiria vya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Utafiti huo umeonyesha kiwango cha maambukizi ya VVU kwa waendesha bodaboda ni kidogo kwa asilimia 2.5, vijana wengi wameonekana kuwa na tabia hatarishi zinazoweza kuwafanya wapate VVU.

“Tabia hizo ni kama vile kuwa na wapenzi wengi, baadhi kutotumia kondomu na kutofuatilia ili kupata huduma ya ushauri nasaha na vipimo,” alisema.

Dk. Malecela alisema taasisi inapendekeza kufanyika utafiti huo katika maeneo mengine kwa kujumuisha makundi mengine ambayo yako hatarini kuambukizwa.

Alisema pia wameanza majaribio ya chanjo chini ya mkakati mpya kupitia mradi wa P5.

“Majaribio haya yanafanyika, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji, Zambia, Malawi, na Kenya. Chini ya mpango huu, washiriki wenye umri kati ya miaka 15-50, wasio na maambukizi ya VVU na magonjwa sugu wanashiriki katika awamu mbalimbali za utafiti.

“Tanzania inashiriki majaribio haya kwa kushirikiana na washirika wake, Mpango wa Utafiti wa Jeshi la Marekani na Mtandao wa Tafiti za Ukimwi Duniani. Mpaka sasa taasisi imesajili washiriki 17 kati ya 28 wanaotegemea kusajiliwa kwenye mojawapo ya tafiti hizi za chanjo,” alisema.

Alisema NIMR imeanza kufanya utafiti wa kufuatilia usugu katika dawa za kurefusha maisha (ARV) kwa watu wanaotumia.

“Tulifanya pia tafiti za VVU na Ukimwi na kutathmini utekelezaji wa mpango wa kupima watoto wachanga, tumebaini bado kuna changamoto kadhaa."

CHANZO. Gazeti la Mtanzania.
16/12/2016
 
Ni shida,ugonjwa mbaya sana watoto wanazaliwa na ulemavu,ila nasikia kuwa wazungu wamemtengeza huyu mdudu ili wao wauze dawa
 
wp_ss_20161216_0004.png

Virusi vya Zika vyagunduliwa nchini Tanzania - BBC Swahili
 
Mkuu hiyo habari wameshaikanusha sasa hivi kupitia hao hao BBC. Wanadai wizara bado haijathibitisha hilo jambo.
 
BBC SWAHILI (USO WA MBELE) wamechapisha habari hii. wizara ya afya nchini humo IMEKANUSHA kupatikana kwa virusi hivyo.
 
Mkurugenzi wa NIMRI dk Mwele Malicela anasema wamefanya uchunguzi na kugundua ugonjwa huo upo Tanzania,Ummy Mwalimu na Hamis Kigwangala wanasema haupo.Ni nani yuko sahihi?
 
Kama Malaria tumeshindwa kuitokomeza, hivi virusi vya Zika hatutaweza ukizingatia hata chanjo hamna, miaka 30 ijayo naliona Taifa la Tanzania likiwa na vijana wenye vichwa vidogo, tena wakiwa Saresare, sasa fikiria mtu mwenye chogo hafu akose Komwe!!
 
Tanzania ina serikali ya kipekee.
NIMR,Taasisi ya serikali ya utafiti imefanya kazi yake na kuijuza nchi,kuwa virus vya ZIKA vipo.
Ghafla Naibu waziri,Dr.Kigwangala anatoka hadharani na kupinga ripoti ya NIMR!!!!Just one day bila hata ya site visit,!!!!
A failed system !!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom