Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,854
natoa shukrani kwa michango yenu yote na ningejaribu kumjibu mmoja mmoja lakini kama mnavyojua ttcl yetu hii na mitandao ya kudandia.
Naomba niseme tatizo si fedha zake kwani na mimi nina za kwangu na nina uwezo wa kuishi vizuri tu. Mwanzoni nilifikiri ni mtu wa urafiki tu lakini aliponipa hizo za kunidondokea ndio nimepata na utata. Hivi nikiamua kuanza kumchunia si atanielewa vibaya na anaweza kuanza kudai "yote aliyonifanyia" mimi na mwanangu?
Au niamue kumlipa "kiaina" yaishe huku nikijua siwezi kuwa naye? Lakini pia maisha ya kuishi single muda mrefu nayo si mazuri kwani Mungu alituumba wawili wawili.
Nimeuliza hapa si mimi tu kuna mabinti wengine ambao wao hawana hata watoto lakini wanajikuta na utata huu wa kutembea na waume za watu hasa hawa waheshimiwa wetu. Au na sisi tuingie kwenye haya ya kuwakamua tu na kuwachuna?
nadhani nitafikia uamuzi na asanteni sana. Bimkubwa, nashukuru kwa ushauri wako. Umenisaidia sana.
Asanteni.
Kama walivyosema wengi jibu unalijua. Wewe ulishafanyiwa na unajua chungu yake sasa kwa nini unataka kujiingiza huko? Hauna haja ya kumchunia wala kumchukia maana yeye kama mwanaume yeyote katupa ndoana yake na kuna kupata na kukosa. Ukimtema, mteme kiungwana na kama ni muungwana kweli basi uhusiano wenu utakomaa zaidi maana mipaka itakuwa inajulikana kwa wote. Hawezi kukudai chochote maana alifanya yote kwa mapenzi yake. Na kudai kunaweza kumlipukia maana haitakuwa siri tena kuwa alitoa kwa malengo gani.
Ukiamua kumshukuru kiaina, ufanye ukijua kuwa na wewe utajulikana tu. Kama vile wewe ulivyomstukia mwenzio (au tatizo lilikuwa ni yeye kuzaa na sio kuwa na uhusiano nje?). Upete ukijua kuwa kama itatokea siku akatokea anayekutaka na yuko huru patakuwa na kazi! Jamaa dizaini hii ni ving'ang'anizi ile mbaya.
Lakini nina wasiwasi. Is this for real? Maana kwa simulizi zako kama jamaa anapitia humu atakuwa ameishajijua!
Asante.