Nimfanyaje huyu: Mimba zote zinaharibika.

Muombe Mungu wakati wake ukifika atawapatia, nendeni pia Hospitali kubwa ili kujua tatizo.
 
Uzazi una mambo mengi, complications nyingi sana. Zamani na hata sasa wengi wapo na notion kuwa miscarriage nyingi ni matokeo ya utoaji mimba, lakini wala sio kweli, hiyo yaweza kuwa moja ya sababu nyingi mno.

Nendeni wote hospital, huenda tatizo liko kwako mwanaume.
 
Kitaalamu inaitwa "recurrent abortions/ miscarriages, yaani mimba kutoka au kuharibika kwa mara tatu au Zaidi.

Sababu:
1, Matatizo ya kromosumu (3-5%) (chromosomal abnormalities)
2, Matatizo ya nyumba ya uzazi( uterine abnormalities)
3, Maambukizi (Infection): bacterial vaginosis,
4, Magonjwa sugu na ya kudumu: Kaswende, kisukari, tezi ya shingo, magonjwa ya figo.
5, Ulegevu wa shingo ya tumbo la uzazi (cervical incompetence).
6, Polycystic Ovarian Syndrome (Viroba/ uvimbe kwenye ovary) hii inawagusa asilimia 58.
7, Uvutaji wa sigara.
8, Kufakamika pombe kulikopitiliza.
9, Hakuna sababu itakayopatikana (Idiopathic).

Mtafute bingwa mtaalamu aliyeboboe katika magonjwa ya wajawazito na wanawake (Obstetrician and Gynaecologist) ili ampime shemeji yetu. Kila la kheri.
 
Amani ya bwana iwe nanyi.

Wakuu nimekuja kwenu nikiwa na jakamoyo, nalo ni baada ya kuwahi kuleta malalamiko hapa kuhusiana na shem wenu ambaye ameshaharibikiwa mara mbili , nilikua natarajia lolote mwaka huu lakini nayo imeharibika, hii ni ya tatu sasa wakuu.

Sijali gharama ninazo/nilizoingia kumhudumia as it is part of the bargain, lakini nahisi kama si mti unaozaa matunda.

Nimeamua sasa kutafuta kwingine. Nimekosea????
ni mkeo au mchumba? vyovyote itakavyokuwa, utamwacha alafu utakuta kaolewa na mwingine anapata tu mapacha, hapo ndio utajifunza uvumilivu kwa mtu unayempenda. pia, ndoa sio watoto t u ,pamoja na kwamba watoto ni wa muhimu na wanaongeza kitu. kuna watu wamepata watoto hata watano ajali ikatokea wakafa wote akabaki kama mwanzo...hao utawatofautishaje na wewe? nilifikiri utajitahidi kutafuta suluhu ya tatizo ili uishi maisha yasiyo na malawama.
 
Amani ya bwana iwe nanyi.

Wakuu nimekuja kwenu nikiwa na jakamoyo, nalo ni baada ya kuwahi kuleta malalamiko hapa kuhusiana na shem wenu ambaye ameshaharibikiwa mara mbili , nilikua natarajia lolote mwaka huu lakini nayo imeharibika, hii ni ya tatu sasa wakuu.

Sijali gharama ninazo/nilizoingia kumhudumia as it is part of the bargain, lakini nahisi kama si mti unaozaa matunda.

Nimeamua sasa kutafuta kwingine. Nimekosea????
Hujakosea mkuu ukiona na huko pia mambo ni hayohayo then utakuwa na hakika kwamba mwenye kasoro ni wewe!!!
 
Amani ya bwana iwe nanyi.

Wakuu nimekuja kwenu nikiwa na jakamoyo, nalo ni baada ya kuwahi kuleta malalamiko hapa kuhusiana na shem wenu ambaye ameshaharibikiwa mara mbili , nilikua natarajia lolote mwaka huu lakini nayo imeharibika, hii ni ya tatu sasa wakuu.

Sijali gharama ninazo/nilizoingia kumhudumia as it is part of the bargain, lakini nahisi kama si mti unaozaa matunda.

Nimeamua sasa kutafuta kwingine. Nimekosea????
Nop usifanye ivo,,, mpe ujauzito akikaribia kujifungua muhamishe mji akajifungulie mji mwingine au mkoa mwingine,,,

Usimfadhaishe mshike mkono wa maisha, imagine ww ndo ungekuw yeye ungefanyaje,,
 
Nop usifanye ivo,,, mpe ujauzito akikaribia kujifungua muhamishe mji akajifungulie mji mwingine au mkoa mwingine,,,

Usimfadhaishe mshike mkono wa maisha, imagine ww ndo ungekuw yeye ungefanyaje,,
Maumivu ninayoyapata hayaelezeki. Alihama mtaa kabisa ila haikusaidia.
 
unaona rahisi eeehh.... beba mimba na wewe tuone.....nenda hosptal mkacheki blood group
 
Pole sana ndugu, ila nakuomba usimfanyie hivyo mtoto wa mwenzio bado mapema sana.
Nendeni hosptali utapata muafaka wa tatizo lenu. Nenda Muhimbili utapata ufumbuzi wa tatizo lenu
 
Amani ya bwana iwe nanyi.

Wakuu nimekuja kwenu nikiwa na jakamoyo, nalo ni baada ya kuwahi kuleta malalamiko hapa kuhusiana na shem wenu ambaye ameshaharibikiwa mara mbili , nilikua natarajia lolote mwaka huu lakini nayo imeharibika, hii ni ya tatu sasa wakuu.

Sijali gharama ninazo/nilizoingia kumhudumia as it is part of the bargain, lakini nahisi kama si mti unaozaa matunda.

Nimeamua sasa kutafuta kwingine. Nimekosea????
Ndio umekosea kwa maana bado hujatibu tatizo kwani kwa hilo tatizo naamni linatatulika /linatibika hasa kwa kuwa concert wataalam hata mimi ndugu yangu wa karibu sana mimba tatu zilitoka kabla ya juzi kupata naby boy...
 
Jamaa ana tatizo gani wakati mimba inaingia ila baadae ndio inaharibika??
Sio kuwa demu hashiki mimba, anashika ila baadae miscarriage.

Mambo ya blood group ndugu, mimi si mtaalamu sana ila naamini MDs na Pro wengine wa afya wapo humu wanaweza weka clear zaidi.

Zile blood group si zina positive na negative zake? Sasa hizo zikiwa hazishabihiani vyema sahau kuhusu mtoto ata akizaliwa atafariki mchanga au mdogo, kwani hujawai kuona mwanamke kila akijifungua watoto wanafariki wakiwa bado wadogo au wachanga? Wengi huzani mtu kalogwa kumbe walaa ni hayo mambo ya damu.

Natumaini umenielewa ki vipi jamaa nae anaweza kuwa chanzo cha hizo mimba kutoka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom