Nimeyakumbuka maisha yangu ya uyatima; Uyatima ni noma sana ndugu zangu

Hapo kwenye kinyesi me mwenyewe ilinitokeaga
Nilijisaidia kwenye shamba la jamaa ambaye pale kijijini alikuwa anaogopeka Sana
Basi Kumbe jamaa alikuwepo mle shambani kalala na aliniona
Akaniacha nimalize baada ya dk kadhaa nashangaa jamaa yupo nyuma yangu kashika panga
Akaniambia zoa hayo mavi na mkono
Nilichofanya nikachota kuanzia chini ya udongo kwani udongo ulikuwa mlaini nikaenda kutupa mtoni.
Aisee Kuna watu wanaroho ngumu Sana.
Ana roho ngumu, ulitaka azoe yeye..... ungekuwa wewe mwenye shamba ungemchekea?
 
Pole sana. Naelewa sana hali uliyoipitia. Naelewa vizuri sana kwa kuwa mimi pia ndio njia hiyo niliyopitia japo kwa namna ya tofauti kidogo. Ila amini kwamba nakuelewa vizuri.
Hongera kwa kutoboa
 
Pole sana Mungu atakusaidia kufuta maumivu yote, wewe wasamehe tu japo si rahisi kihivyo bila msaada wa Mungu huwezi, hata kama huwezi watafuta ila moyo wako uwe radhi kuyaachilia hayo ili moyo upone, nasema tena pole sana.
 
Jana (Ijumaa) nikiwa kazini Kuna saa nilikosa Kazi (zilikua zimeisha). Nikawazaa, ghafla mawazo ya maisha ya UYATIMA niliyopitia yalinijia.

Ni ndefu sanaa we somaa.!

Japo siwezi kuyaandika yotee, maana UYATIMA wangu ulinipitisha kwenye makubwa sanaa..!!

Nilizaliwa kwenye familia ya watoto 3 tukiwa na baba na mama.
Baba alifariki kwa ku palaryze nikiwa mdogo sanaa.

Baba alikuwa ni mfanyabiashara mwenye mali nyingi ila mama alikua ni mama wa nyumbani.

Kwasababu ya kumkosa mumewe, baada ya baba kufariki mama alikuwa anaumwa umwa Sana.

Hii ilisababisha Mali nyingi kuuzwa na bila kusahau nyengine zilidhulumiwa na ndugu.

Ndugu na marafiki wa baba waligawana mali nyingi sanaa tukaachwa na nyumba tu ya kuishi.

Mama alikua anateseka Sana na mawazo ya kumpoteza mpendwa wake, hii ilisababisha kudhoofisha Kinga ya mwili na hatimae malaria kali ilimjia na kumchukua.

Ilikua ni siku ya jumapili nilipoletewa habari kuwa "Mama yako amefariki".
Aisee Ile siku ilikua nomaa, Mimi na mama tulikua na kijiwe chetu..!! Pale nyumbani (Kona ya barazani kwenye ua alilokuwa analipenda).

Aisee nilikaa pale na kulia sanaa, nilikumbuka ule usia wake, vicheko vyake, sura yake, harufu yake, kifupi niliona dunia imefika mwisho.

Wakati huo nikiwa mdogo sanaa (darasa la 4) ila huwezi amini NAKUMBUKA KILA KITU MPAKA LEO.

Nakuonya mwana JF "Usimfanyie mtoto ubaya" kwamaana "Hawezi sahau".
Mimi japo nilifanyiwa ubaya na ndugu tena nikiwa mdogo ila nakumbuka majina, siku, location yaani kila kitu kwa jambo nililyofanyiwa na ndugu.

Siku ya msiba wa baba watu walijaa wengi na waliiba Mali za pale nyumbani na wezi wote nawakumbuka ""wakina Wajomba zangu""

Baba alikua Tajiri hivyo nyumbani kwetu kulijaa ndugu waliokuja kuomba Msaada.

Ila baada ya baba kufa walipungua sana na baada ya mama kufa ndio kabisaa sikuwaona.

Tulianza kulelewa na dada.

Maisha ya ushua yalipotea na kama upepo, tukaanza shida.

Dada majukumu yalimzidi tuka hamishwa kila mtu kwake.

Mimi nikabaki Dar, mdogo angu mkoani na dada angu akabaki nyumbani.

Huko nilikoenda nilienda kwa mshua mmoja hivi taita Dar pale (rafiki wa baba).

Ila huyu "Mkewe hakunipenda kabisa" sababu mpaka leo huwa siijui.
Nilikua sili Sana, nilifanya Sana Kazi na mengine ila sijui kwanini hakunipenda.

Nilikaa pale miaka miwili, mama akaanda staili moja ili niondoke kwake.

Lile zegwe hausi geli alilijua.
Akanitahadharisha.

Nikamuhadithia shangazi
Shangazi alikuja kunichukua fasta.

Shangazi yangu hakua na maisha mazuri ila nilikomaa hivyohivyo.

Nilikomaa sanaa, chakula hakitoshi, Shule kwenda na miguu tena Dar es salaam, halafu mbali sanaa.
Mwaka mzima hununuliwi nguo mpya..!! Unavaa nguo za kushindia hizohizo mpaka mtaa una kukariri.

Ila nilikomaa.

Shangazi yangu hakuwa na room kwa watoto wa kiume, kwahiyo sometimes nilikua nalala kwenye korido na sometimes nje ya nyumba.

Yaani nje kabisa, milango inafungwa mi nafunga net kibarazani nalala.

Hakua ananitesa na nilikua nina amani.

Kwakuwa chakula kilikuwa hakitoshi nilianza kufanya Kazi kwenye nyumba za watu.

Maisha ya zamani ilikua mwenye hela ndio anabomba la maji la Dawasco.

Hivyo mi nilikua nachotea watu maji wananilipa ndoo moja 50.

Hapo nikawa napata nauli ya kwenda Shule (kipindi hicho mwanafunzi nauli 50).

Na nyengine kabla sijala nyumbani nilikua natanguliza kwanza sambusa, hivyo na kile kidogo cha nyumba nakua nashibaa.

Maisha yalienda mara la 7 nikafaulu.

Miaka ile kufaulu la Saba ilikua dili hasaaa.

Shuleni kwetu tulienda secondary Wa3 tu, yaani tulifaulu Wa3 tu..!!!

Mtaa mzima hongera...!!!

Kufika Shule nikaanza kucheza kamali ili nipate pesa ya kujikimu..!!

Nilikua nawala hasa.

200 inazalisha 3000 mpaka 5000.

Bwana eeeh Kuna siku ikapitishwa karatasi waandikwe majina ya wacheza kamali, na Mimi ndani...!!!

Tulipigwa sanaa siku ile, fimbo kama 100 hivi.
Enzi zile tulikua tunapigwa hasaaa.
Unashika chini huku umebongoa, walimu wanapita na fimbo, ukiishika Tako umefutaa.!!!

Tulipigwa sanaa.

Ila Sasa hata nikiacha kucheza nitapata wapi hela ya kujikimu shule..!!
Shangazi ya kunipa hana, hana uwezo wa kunipa nauli, je madaftari na vitabu atanunua?

Dah maisha yaliendelea, tukawa tunacheza nje ya Shule.

Kufika form 2 nikaongoza wastani kwa Shule nzima.

Ikabidi mwalimu wa darasa aniite "wewe una akili sanaa, kwanini unakua mtundu?"

Nikamuhadithia nayopitia nyumbani, huyu mwalimu niliona kabisa machozi yana mlenga.

Tokea siku hiyo alianza kunichukulia tofauti sanaa.

Form 4 nikaongoza kwa kupata Division 1 Kali sanaaa.

Taarifa zikaenea kwa ndugu na jamaaa + mtaani.

Hongera na masifa kama yoteee.

Ila nyumbani hali ilikua tofauti..!!

Binadamu yangu ye alipata 4 Mimi 1.

Mama ake ikawa kila jambo ananipendelea Mimi..!!

Binamu yangu alini mind sanaaa.

Akawa anatanitaka nitoke kwao, hii "Toka kwetu" mwanzo niliiona ya kawaida sanaa ili kufika form 5 ilikolea sanaa.

Kuna siku nilirudi nyumbani nikafungasha nguo na kusepa gheto la masela wapiga misuli.

Shangazi alimind sanaa.

Akaniita tukaongea na kuahidi kila jumapili nikachukue elfu 5 ya matumizi ya wiki.

Yaani kwa wiki utumie elfu 5..!!
Kula mchana, asubuhi, usiku na hela ya pindi mchikichini..!!

Nilikonda hasaa, maana kila siku nashindia miogo ya Shule.
Maana kila siku natakiwa kutumia buku..!!

Maisha yaliendelea taarifa zikamfikia baba mdogo.

Akaniomba niwe naenda kwake kuchukua misaada.

Nilienda kama wiki 4 mfululizo (kila jumamosi).

Nakumbuka Kuna jumamosi nilienda nikamkuta mkewe na baba mdogo hayupo.

Sasa bana Mimi Nina aibu ya kuomba Msaada kwahiyo muda wa kuondoka nikaaga ili niondoke kimya kimya.

Mama mdogo aliniita akanipa maneno makali "Unasababisha sisi tuishi maisha magumu kisa wewe....." aliongea mengi ila mwisho wa siku alinikataza kwenda kwake kuchukua misaada.

Na kama baba mdogo alijua maana hakuwahi kuniuliza lolote juu ya lile jambo.

Nilifika nyumbani siku hiyo nililia sanaa, nilikumbuka maisha ya baba yupo na mama.
Nililia balaaa.

Ghafla mama mdogo (ndugu wa mama) akaniambia niwe naenda kwake.

Huyu nae alinisaidia mara sijui 6 ya 7 nae akanipa dongo "Kwani wengine hawapo" nilibaki mdomo wazi.

Nikarudi gheto nikajisemea "Sitaki tena msaada nitakomaa mpaka nafia humu"

Ile elfu 20 ya mwisho niliyopewa Msaada nikafanya mtaji wa kuuza vitu vidogo vidogo Shule na mitaani.

Nikaacha kwenda mchikichini (tution) NECTA form 6 sikufaulu vizuriiiiii, ila nilipata credit za Degree.

Nilisoma PCB ila nilipenda sanaa mambo ya biashara.
Afya sikuiwaza kabisaa na Wala sikuipenda.

Sasa bana kuomba mkopo na post, post zinatoka chuo UDSM halafu bodi ya mkopo "NO LOAN".

Nani atanisomesha sasa??..!!!!!

Dah nikawazaa, kumbe shangazi yangu anahangaika.

Akanitafutia ufadhili mmoja wa ada.
Chuoni nikawa nalipa 240,000/= ya mambo mengine ya chuo ila ni Diploma.

Nikajisemea "yaani hizi C zangu za PCB naenda kusoma diploma, huku wenye E na D wanaenda degree"
Maisha gani haya...!!!

Nikabeba begi kwenda chuo.

Chuoni sikua na raha Wala amani, nilipenda masomo ya biashara ila nikawa nasomo visivyojulikana na moyo wangu..!!

Nikiwa Diploma 2 mdogo angu akamaliza form 4, akapata ufaulu wa kawaida ila sio wa kwenda advance..!!

Wakumsomesha HAKUNA..!!

UYATIMA nyie, Achana nao kabisaa...!!

Ikabidi nimpe ahadi ya kwamba anisubiri mi mwaka mmoja nimalize Diploma halafu yeye ataingia kwa ada yangu mi nitaishia hapo..!!

Ila kabla ya hapo nikiwa form 4 na 6 nasubiri matokea na post zakuendelea kusoma nilishawahi fanya sehemu tempo.

Kwahiyo lengo langu lilikua ni kumaliza Diploma halafu niende pale kujishikiza, then mdogo angu aingie chuo.

Nikamaliza diploma kufika ile ofisi kuongea na bosi akakubali. Kunipa Kazi.

Nikawa mpiga Kazi pale.

Nilikomaa kuishi maisha magumu hasaa ili tu mdogo angu aingie chuo.

Aisee ni mengi aiseee.

Ile dogo kumaliza Certificate nikamshikiza pale job na kikazi fulani hivi.
Huku Mimi nika apply Kazi serikalini nikapata Mkoani.
Dah hapo ndio ikawa kama nafuu imeanza kuja.

Maisha yalienda, serikalini kazini nikaomba ruhusa ya kwenda Shule kupiga Bachelor nikaunga Masters.

Sikuacha ndoto zangu zife, nilienda kusoma masomo ya biashara.
Ghafla zile ndoto zilizozimwa kisa yatima kakosa ada zikatimia.

Na mwaka huu naingia darasani kusoma PhD yangu..!!!

Na mdogo wangu aliendelea mpaka akapata CPA..!! Na mwaka huu anaingia darasani kusoma Masters.

Mama yetu alikua anatuambia "baba yenu alitaka na kutamani sanaa msome".

Angalau sasa hata tukifa tunaenda kuwaambia wazazi wetu "Tumemaliza yale mlioyatamani kutupa"

Dada yetu yupo na ameolewa na yeye ndio mama yetu.

Huwa tunamlea vizuri ""Japo tunampaga pesa kimya kimya ili shemeji asijue..!!!""

Aisee ni mengi aisee na siwezi kuyaandika yoteee.

Maana pia nilishawahi fukuzwa na shemeji (mke wa kaka - kaka mtoto wa baba mkubwa) bila kujua sababu..!!
Nilikua naendaga kuwasalimia, mkewe sijui akanichoka na kunifukuza ..!!!

Kifupi ndugu walikua wanadhani na hasa wake wa ndugu zangu walikua wanadhani sijui naenda kumaliza hela za waume zao.

Kifupi hakuna aliyenisaidia bila kulalamika, na kunisimanga.
Na wotee waliona Bora kunitimua ili nisiwaletee shida makwao.

Kifupi mpaka leo ndugu huwa siwaelewi.
Huwa wanapiga simu na kiukweli si "save" namba zao.
Na kesho wakipiga Tena na nikiwauliza "nani mwenzangu" huwa wanakata simu na kusema "huyu siku hizi yupo serikalini na kasoma basi anajidai sanaaa"

Na huwa hawaniambii direct ila Wana mwambia dada au shangazi.

Cha ajabu WAMESAHAU YOTEE WALIYOTENDA..!!!

Kifupi sina swaga yoyotee na ndugu YOYOTE.

Siwachukii ila SINA MPANGO NAO KABISAAA.

Ila mdogo angu anamsemo wake "Atavuna aliyepanda kwenye maisha yangu tu, kwani wakati hatuna wazazi na tunateseka walikua wapi"

Kifupi hatuna connection na ndugu wa upande wa mama woteeeeee yaani hata mmoja sijui yuko wapi.

Ila Kwa baba ni shangazi yangu ndio aliyepambana tukafika hapa..!!!
Tupo nae karibu na tunampenda sanaaa.

Baba yangu kwao walizaliwa Wa2 tu.
Yeye na dada ake ambae alitulea.

Nampenda sanaa shangazi yangu na namuheshimu sanaa.

Siwezi kufika Dar bila kumuona Wala kumletea Zawadi ni Mungu wangu aisee hapa duniani.

Ila ndugu wa mama HAPANA KWA KWELI.

Siwachukii ila HATA SIJUI WAKO WAPI NA SINA MPANGO NAO KABISAAA.
Waliamua kunitupa na Mimi nimejitupa mazima.

Dah tuishie hapo.....

YANAYONITAWALA KICHWANI.

1. Natamani kumuuliza yule mama wa mshua, kwanini alipanga kunifanyia lile tukio ili mumewe anifukuze?

2. Natamani kuwauliza wajomba zangu, kwanini mliamua kutudhulumu mali zetu?

3. Natamani kuwauliza mama wadogo, kwanini mliamua kumuacha dada yao (mama yetu) atulee kwa shida wakati wao walikua wanakuja kwake kulia shida?

Kifupi natamani tu nikae na walionifukuza halafu niwahojii kwanini walinifanyia vile.
Yaani tuhojianee weee mpaka moyo ukaridhika.

Natamani nikae na walionipitisha kwenye shida niwahojiiii mpaka niridhike.

KITU NILICHOSHINDWA NI KUWATAFUTA NA KUONGEA NAO.
Najua watakua wanamiliki simu ila hata kutafuta namba zao NIMESHINDWA ..

Na nimepitia mengi siwezi kuyaandika yoteee mengine yanauma na kuumiza.

Tuishie hapa.

Miss you Daddy and Mammy.

UYATIMA ni nyokooooo sanaaaa.
Uyatima unauma sana mm kuna matukio sijawah kuyasahau
 
Ghafla nimekumbuka sinema ya bite na lamoza,enzi hizo ikiwa inaonyeshwa mashuleni

Jinsi wale watoto walivyokuwa wanateseka,nakumbuka mwalimu wangu alikuwa anapewa leso ya kujifutia machozi..uyatima mbaya sana
Hii movie ilikua Kali sanaa, pamoja na Ile ya NEILA ya MAMA MJANE..

#YNWA
 
Leo ndio nimejua sababu ya wewe kutoka kuoa. Hujajifunza kwnye ndoa ya baba ako na mama ako
?
Nani amekwambia hilo?
Baba na mama walikua na maisha yao kwa uchaguzi wao, na Mimi Nina maisha yangu kwa uchaguzi wangu.

Kwani wale watoto mashoga, gays, na wezi ni kwamba wazazi wao walikua hivyo?

SIKIA DUNIA INA MAMBO MENGI SANAA na MUDA NI MCHACHE SANAA.

Narudia Tena:-
Nimeamua kufata njia ya KUSOMA na KUTAFUTA HELA hilo la KUOA NIWAACHIA NYIE.

#YNWA
 
Duh pole sana mkuu kwa yote uliyopitia, ila naamini kila jambo linapangwa na Mungu ili ufike somewhere, hizo shida na yote uliyopitia ni Mungu alikusudia ufike hapo ulipo,hatuna budi kushukuru na kusamehe tu.

Ila uoe sasa, achana na mambo ya ubachela bana, wanawake wenye tabia njema bado wapo
 
Unaweza ukatunga kitabu chako mkuu, umeupiga mwingi sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom