johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,840
- 141,765
Nimwwasikiliza wabunge wote wa Chadema waliohojiwa na vyombo vya habari baada ya kutoka kwenye mahojiano na maofisa wa Takukuru.
Kwanza nilimsikiliza Lijualikali aliyedai wabunge wa Chadema wamepanga njama za kuidanganya Takukuru.
Nikakaa mkao wa kuwasikiliza wabunge wengine ili nibaini hizo njama.
Nilichogundua baada ya kuwasikiliza ni kweli wabunge wamekiri kukatwa fedha zao kwa ajili ya ujenzi wa chama na hiyo ni kwa mujibu wa katiba ya Chadema
Pili, makato hayo hukatwa na ofisi ya bunge chini ya Baraka za mh Spika na kuwasilishwa kwa Katibu mkuu wa Chadema.
Tatu, matumizi ya chama husimamiwa na Katibu mkuu na fedha za chama hutunzwa na mhasibu mkuu wakati matumizi ya chama huamuliwa na kupitishwa na kamati kuu ya chama.
Suzan Lyimo kwa mfano alishangaa wao kuulizwa maswali yaliyopaswa kuelekezwa kwa mhasibu kwani wao kama wabunge katiba inawataka kuchangia ujenzi wa chama siyo kupanga matumizi.
Suzan Kiwanga amedai makato yao hubsrikiwa na mh Spika.
Naye mbunge Pareso anasema kanuni ya makato huelezwa kuanzia day one unapojaza fomu ya maombi ya ubunge hivyo ni uamuzi wako kama hutaki usigombee.
Katika mazingira haya ni wazi makato ya wabunge wa Chadema yako kikatiba na matumizi yake huidhinishwa na kamati kuu ya chama.
Labda ndio maana CAG aliwapa hati inayoridhisha
Nimalizie kwa kusema fedha yoyote ya taasisi huweza kubadilishiwa matumizi na hiyo siyo dhambi ndio maana hata fedha za bajeti zikifika serikalini zinaweza kubafilishiwa matumizi kwa nia njema tu ya kuleta maendeleo kwa haraka.
Nawatakia Dominica yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!