Nimewaona,nimemshukuru Mungu

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Mara nyingi tunaangalia mbele na kusema "sijafanya chochote maana ninapo enda ni mbali sana"

Week iliyopita nilikutana na class mates wangu tulio maliza wote darasa la saba (LY,haha)
Nikakumbuka,katika darasa lile,tulimaliza watu 68 mwaka huo ila:-
*ni watu wa nane (8) tu tulio chaguliwa kuingia kidato cha kwanza.
*katika hao wanane,ni watu 6 tu tulio maliza form four
*katika hao 6,ni wawili tu tulio ingia advance.
*katika hao wawili,tuliingia wote chuo.

Nikafikiria,hao wengine 66 wako wapi?
Ofcourse,wengine hawakusoma lakini wana maisha mazuri tu,ni kama wa3 kati ya wote
ninao wafahamu.

Nilitokwa na machozi kwani hii ilikua sababu tosha kwangu
kumshukuru Mungu kwani alipo nitoa ni mbali haijalishi naenda wapi.

Unawakumbuka watu ulio maliza nao darasa la 7(maana hawa ndio mlikua wote utotoni)?
wako wapi na wana hali gani?
 
Mhhh ngoja nikumbuke
Wengine waliishia pale pale std seven wakaja kuwa mafundi magari au carpenter
Mmoja ni dr kwa sasa ana maisha yake na familia yake
Mwingine was my friend yuko African Court of human and peoples right wengine ni wafanyabiashara japo hawakuendelea na shule
Duh ni great moment sana unapokutana na mtu mliyemaliza nae la saba
 
Sure,maana hawa ndo watu ambao wana kufahamu toka
enzi hujui kujipangusa vizuri makamasi hadi mda huu.
Too bad marafiki wengi tunao kuwa nao ukubwani na hata
washiriki wetu kibiashara ni wale tunao kutana nao
kwa mda mfupi sana na hatuwafahamu vyema
 
True mkuu hao ni watu ambao wanatufaham vyema na wanafahamu mambo yetu mengi. Marafiki wengi wa ukubwani ni wanafiki wengi na hawana real love kabisa
 
mmm nimekumbuka mbali sana.Sisi tulifaulu wawili tu kati ya 65.Mimi nikaenda sec wa pili mdada akaenda wakati huo ualimu grade B..Enzi hizo usafiri kwa train na mabasi ya TRC natunatumia warrant..na tunapewa masurufu ya njiani wewe...Basi bwana
 
baada ya form four karibu wote wako kijijini wanne tu waliendelea na shule, na mie ndio neema imefunguka kwa sasa nipo chuo, ...naomba Mungu anipe moyo wa ujasiri nisome nifaulu... ukifikiria ni ngumu kuamini, maisha magumu sana ndugu yangu
 
Long tym man!
Hahaaaa! Tulifaulu 3 kati ya 44, wawili waliishia form four, mmoja anafanya PhD sasa hivi, wengine wana wajukuu, kuna lidada limoja lilikuwa libabe ile mbaya, sasa hivi lina wajukuu watatu! Choka mbaya, nyumba inataka kumuangukia huko kijijini,.....pamoja na ubabe wake wakati ule, sijisikii vibaya kuwasaidia wajukuu zake ili wasiishie alikoishia bibi yao.
 
Mbona kila anaechangia hakuna asemae kuwa alifeli? Au ndio kama zile za baba kujisifu kuwa alikuwa namba moja darasani lakini akaishia la saba.
 
mmm nimekumbuka mbali sana.Sisi tulifaulu wawili tu kati ya 65.Mimi nikaenda sec wa pili mdada akaenda wakati huo ualimu grade B..Enzi hizo usafiri kwa train na mabasi ya TRC natunatumia warrant..na tunapewa masurufu ya njiani wewe...Basi bwana

Dah,we wa zamani kweli aisee.
Hongera
 
Long tym man!
Hahaaaa! Tulifaulu 3 kati ya 44, wawili waliishia form four, mmoja anafanya PhD sasa hivi, wengine wana wajukuu, kuna lidada limoja lilikuwa libabe ile mbaya, sasa hivi lina wajukuu watatu! Choka mbaya, nyumba inataka kumuangukia huko kijijini,.....pamoja na ubabe wake wakati ule, sijisikii vibaya kuwasaidia wajukuu zake ili wasiishie alikoishia bibi yao.

Hahaha,"hilo lidada" lilikutosa nini?
me nilio maliza nao darasa la 7 wengine nikiwa form 1 walikua na watoto tayari
namaliza form4 wana watoto wa2,...sijui saivi watakua na team gani huko.
 
Huu uzi umenikumbusha mbali sana...mie ninajua walipo wawili kati ya darasa zima tuliomaliza nao std 7 enzi hizo.
Inauma sana kuona kuna wengin wamepoteza mwelekeo siku nyingi zilizopita.
 
baada ya form four karibu wote wako kijijini wanne tu waliendelea na shule, na mie ndio neema imefunguka kwa sasa nipo chuo, ...naomba Mungu anipe moyo wa ujasiri nisome nifaulu... ukifikiria ni ngumu kuamini, maisha magumu sana ndugu yangu

Sure,ni magumu sana.
Unajua nini kilinifanya nimshukuru Mungu zaidi?
sijawahi kua namba1 au 2 nafasi kubwa niliyo kwisha kamata darasani ni 3
tena nikiwa darasa la tano.
Lakini pia sijawahi kuondoka kwenye top 10,iwe primary,olevel,advance.

Na yule aliye kua anaongoza primary,toka
darasa la kwanza hadi la 7 alikua wa kwanza yeye na
alimaliza vigumu sana form 4 akapata div4.32.
(sio kwa sababu ya ugumu wa kifedha,nope,tulipotoka kijijini alikua mtu wa starehe sana)

Ila leo hii yupo anachukua diploma,alianza na certificate.
Namuombea apande juu zaidi
 
Huu uzi umenikumbusha mbali sana...mie ninajua walipo wawili kati ya darasa zima tuliomaliza nao std 7 enzi hizo.
Inauma sana kuona kuna wengin wamepoteza mwelekeo siku nyingi zilizopita.

Nilipo onana na hawa jamaa,
pamoja na furaha nyingi tulikua tunapiga story za wenzetu.
Ina sikitisha kwamba katika darasa la watu 68,watu 60 hawakuweza kujua hata
secondary iko vipi,ni wawili tu walienda veta na mmoja akaenda jeshini.
wengine wako vijijini wakiendelea kuifanya Tanzania kua jangwa (kwa kuchoma mkaa)
na kuuza maziwa mjini.
 
mimi huwa nafarijika ninapowaona wale waliokuwa hawana akili but wamefaulu maisha....

Sidhani kama kufeli mtihani au kufaulu mtihani ni kipimo cha akili.
Wengi ni wavivu tu kijishughulisha na kufanyia kazi akili zao,..
ila pale wanapo gundua wamechelewa ndipo wanaanza kutumia akili zao.

Na hapo ndipo unapo waona wakifaulu katika maisha kwa namna ya ajabu sana
 
Kuna rafiki yangu namkumbuka sana nilimaliza nae la 7, sijui alipo. Natamani siku moja tuonane tena.
 
Clemmy I am Proud of you... You've got Sooooo much LOVE in you...

I'm honoured by your compliment.
Thanks to my new "name" here,the old one was not me,it forced me to
wear the character of the name hahaha.
 
Kuna rafiki yangu namkumbuka sana nilimaliza nae la 7, sijui alipo. Natamani siku moja tuonane tena.

Mtakutana tu,hadi kukutana na hawa jamaa nakumbuka
nilianza kwa kukutana na mmoja ubungo mataa nikiwa na haraka kweli.
Tukabadilishana namba,akanambia kuhusu wengine na tuka kutana for fun.

Ilikua wonderful, yaani unakumbuka your real original life.
Life ya sasa nimegundua na fake mambo mengi sana,that was the life and
am going for it.
 
I'm honoured by your compliment.
Thanks to my new "name" here,the old one was not me,it forced me to
wear the character of the name hahaha.

I had a funny feeling... which is no mo'....lol

Enways.. the way umekuja... umekuja perfectly... Your Avatar is engaged to your signature and married to your posts.. Keep it up.
 
Back
Top Bottom