Nimewahi kutangatanga makanisa yote nikamaliza mwisho nikaamua kwenda Kwa waganga tu!

Msemajiwao

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
638
1,531
Anayopitia Bashite sasa; Huenda ndiyo Yale niliyowahi kuyapitia;
Nimewahi pitia maisha magumu saana kiasi kwamba nilikuwa naweza kutembea njiani nikiwa naongea peke yangu;
Hali ilikuwa ngumu sana kiuchumi kwangu elfu kumi ilikuwa kama million!
Hapo ndipo nilipoanza kutanga tanga kutafta miujiza, ;
KKKT Nilikwenda nikaona si kitu;
Nikaenda katoriki haikunitosha;
Nikaenda Kwa Rwakatare kule nikakutana Bahasha nikakacha;
Nikaenda Kwa kakobe tena nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimevaa kadeti nikazuiwa kuingia hadi nikatafte suali ya kitambaa, nikaahirisha, wiki iliyofuata nikaenda Kwa mzee Wa upako, huko nako nikasali weee Hanna kitu, nikaenda Kwa katunzi nako nikaona sifanikiwi, wakati nikiwa natafakari kwenda ufufuo na uzima yule mtu aliyekuwa akinipa nauli juma pili akasafili nikawa mtu Wa kijiweni; maisha yalinipiga sana!
Kuna jamaa akanipeleka Kwa ndugu yake mganga...haloooh usiombe!
Nikapewa dawa ya kuoga na chale za ma***** yaani nilisumbuka sana!
Hadi nikaja kukutana na mwana saikolojia mmoja akaniambia!
Akanisihi ; akaniambia na yeye kapitia hali ngumu, akanikutanisha na watu waliopitia hali kama yangu akanifanyia Counselling!
Akaniambia neno moja tu" Niishi kama sina vyeti, nijichukulie elimu yangu ni sawa na darasa la saba, nisimwonee aibu mtu nifanye kazi kama vile niko chini ya ulinzi, nifanye kazi Kwa malengo, nisifikilie kushindwa Bali nijiwazie ushindi kila sehemu niendapo! n.k
Nikayachukua maneno Yale na kuyaishi!
ASIKWAMBIE MTU HADI LEO SIJAWAHI KUJUTIA, NIMETULIA NAKULA MAISHA YA KIYOYOZI MAISHA YANASONGA!
"Huku kutangatanga Kwa Bashite anakoelekea ni kwenda Kwa waganga Wa kienyeji"
 
Back
Top Bottom