Nimewahi kupiga kura mara moja tu, na sitarudia tena- vyote ni haki yangu ya Kidemokrasia, na sababu ya msingi ninayo

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Mwaka 2010 nilipiga kura kwa mara ya kwanza, sio kwa sababu umri ulikuwa umefika, ila kwa sababu ya ku-test kinga ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika masuala ya Urais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ibara ya 74). Matokeo ya Urais hayahojiwi wala kuchunguzwa katika mahakama yoyote (ibara ya 74(12)) au chombo chochote (ibara za 41(7), 83(2)), na pia yanatangazwa na NEC tu (41(7)). Ushahidi wa kuwa NEC hukosea, ni baadhi ya kesi za uchaguzi za ubunge na udiwani za kupinga matokeo ushinda.

Je, ni kigezo/ sababu gani watanzania, kama kweli ndio waliotunga vifungu hivi vya katiba, walitumia kuilinda NEC namna hii na kuwa na kinga kali kuzidi hata wananchi wenyewe? Tume yenye hadhi ya 'Umungu'!

Basi sasa, kwa kuwa nina akili timamu, na kwa kuwa ninatakiwa kuitendea haki elimu yangu, ninaithamini sana kura yangu, na sitaki ichezewe, na ninataka kuhoji mara ninapohisi kuwa 'imenajisiwa.' Sasa kwa sababu mwanya wa kufanya hivyo haupo, basi sitapiga kura - kwa Kiingereza 'abstaining' na wala sio 'apathy.' Na hii ni haki yangu ya msingi ya kidemokrasia.

Na hiki ndio moja ya vipimo vya mwanadamu au mtu aliyetimamu kabisa, na anayeyaona haya basi huyo yupo vizuri.
 
Back
Top Bottom