Nimevutiwa na jinsi ambavyo vyombo vya usalama vya Taifa la Amerika vinafanya kazi kwa uhuru na bila kuingiliwa na wanasiasa kwa matakwa yao binafsi! Hillary Clinton, mgombea wa chama Democrats ana nafasi kubwa sana kushinda Urais wa taifa hilo kubwa na lenye nguvu nyingi duniani! Ila hilo halimfanyi awe juu ya sheria!!!
Kuitwa kwake kuhojiwa na FBI kuhusu matumizi ya anwani binafsi ya barua pepe kwenye maswala ya kiofisi akiwa mtumishi wa umma, kuna fundisho kubwa sana kwetu kuhusu siasa zetu, wanasiasa wetu, vyombo vya taifa vya usalama, na swala zima la maslahi mapana ya taifa vis-a-vis matakwa ya wanasiasa!