Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

Nashangaa jamaa wanalazimisha kuwa nimeibiwa na ndugu yangu ninayeishi naye, wakati naishi peke yangu

Mkuu wewe kama uko karibu na kigamboni sema tufanye mpango nikununulie kibubu niliponunua mimi na nikupe bure kabisa, weka hela na baada ya muda kivunje unipe taarifa.
Asante sana kwa offer mkuu. Kwa sasa sipo karibu ila wazo lako nimelipenda. Pia kuna wakati nilishaomba sana hapa JF watu wanaojua nyumba zenye majini, mizimu na kila aina ya mauzauza na watu wanaogopa kulala ndani basi waniambie ili nikalale huko hata mwezi mmoja. Hizo fedha zako kuna mtu tu alikuwa anakulia time na kuiba kama kweli hukukosea kuhesabu.
 
Tena wanawake ndo wanapenda sana kutumia vibubu

Halafu nashangaa hii mbinu ya kuchomoa noti kwa kutumia sindano wengi hawaijui

Kuna mdada mmoja sogea tukae nikiwa chuo nilikua nazitumbua hela zake Balaa. Alikua anaweka ef20 au 30 au 50 kila siku (Alikua mfanyakaz wa sheli bamaga/mwenge/victoria)

Sema nilikosea nilikula hela hadi ya ada ya mwanae wa chekechea. January anavunja alikuta elfu40 tu aliyoweka usiku wa mwaka mpya.

Ila uzuri au ubaya aliamini kuwa kile kibubu kina chuma ulete akalia masikini akaanza kukimwagia mafuta ya olive ya kakobe. Angejuaa......Angejuaa chuma ulete nilikula mimi bwana wake dah

Monique nisamehe beby. Ulikua ujana tu ule (circa 2011)
Mtafute umuombe msamaha.
 
Wakuu kama kuna mtu haamini hii kitu, anunue kibubu (huenda vibubu vingine havina chuma ulete, sielewi katika hili) aweke hata buku kila siku (kwa walau siku kumi)

And then avunje aje atupe mrejesho!
Mi natumia mara nyingi sijakutana na hicho ukisemacho.
 
Nilitaka kutengeneza mwenyewe, tatizo muda kaka!

Ubize mwingi, na nilipoona hivyo vidude vinauza buku tu nikaona kitonga hii hapa naserereka na buku langu, kumbe ni matatizo!
Kibubu cha ukweli ni Kopo la Dawa ya Mbu ya Rungu kopo kubwa lile ikiisha unatoboa kwa nyuma size ya kupenya Coin na Noti tuu
 
Hivi vibubu mnawezaje?

Mi ni mtaalamu wa kujiibia mwenyewe kwa kutumia kitu chenye ncha nachomoa tunoti.

Afu zikiwa hazitoki tena natikisa mpaka chenchi zote ziishe.

Ila mwisho wa mwaka ndo nitavunja kabisa sijawahi kujua huwa nategemea kukuta nini 🤣🤣
🤣🤣🤣🤣🤣🤣aiseeh
 
Tena wanawake ndo wanapenda sana kutumia vibubu

Halafu nashangaa hii mbinu ya kuchomoa noti kwa kutumia sindano wengi hawaijui

Kuna mdada mmoja sogea tukae nikiwa chuo nilikua nazitumbua hela zake Balaa. Alikua anaweka ef20 au 30 au 50 kila siku (Alikua mfanyakaz wa sheli bamaga/mwenge/victoria)

Sema nilikosea nilikula hela hadi ya ada ya mwanae wa chekechea. January anavunja alikuta elfu40 tu aliyoweka usiku wa mwaka mpya.

Ila uzuri au ubaya aliamini kuwa kile kibubu kina chuma ulete akalia masikini akaanza kukimwagia mafuta ya olive ya kakobe. Angejuaa......Angejuaa chuma ulete nilikula mimi bwana wake dah

Monique nisamehe beby. Ulikua ujana tu ule (circa 2011)
Dhulma hii
 
Back
Top Bottom