Nimevuna nazi takriban 8000, natafuta madalali wa nazi soko la Ilala na Temeke Stereo

Bora uuzie mzigo shambani.. Ukishampa dalali mzigo kwa mali kauli, hesabu maumivu.. Au bora ukakomae mwenyewe sokini.. Tafuta kizimba.
 
Kweli aisee,umasikini nje nje hapo.
Kilimo ni long-term betting inayohusisha mtaji wa kudunduliza tu.😂😂😂!!!

Mkeka unaweza win kwa odd nyingi au ukatoa odds ndogo tu. Unalima kwa mtaji wa 3M unavuna mazao ya 3.5M ukiangali muda uliowekeza kwa pesa hio hio ungeweza ku secure returns kubwa zaidi katika mambo mengineo.
 
Kilimo ni long-term betting inayohusisha mtaji wa kudunduliza tu.!!!

Mkeka unaweza win kwa odd nyingi au ukatoa odds ndogo tu. Unalima kwa mtaji wa 3M unavuna mazao ya 3.5M ukiangali muda uliowekeza kwa pesa hio hio ungeweza ku secure returns kubwa zaidi katika mambo mengineo.

Unamfahamu mshikaji wako yoyote yule ambae ni mkulima na shughuli hio ilimfanya kawa fogo man?
 
Ndio maana kilimo sitaki hata kukisikia.
Kama hutaki kilimo kisa unamuogopa dalali labda nikukumbushe tu kwamba hata ajira siku hizi zinapitia kwa madalali! Ukitaka kupanga au kununua nyumba, kiwanja, dalali unae anakusubiri!
 
Kama hutaki kilimo kisa unamuogopa dalali labda nikukumbushe tu kwamba hata ajira siku hizi zinapitia kwa madalali! Ukitaka kupanga au kununua nyumba, kiwanja, dalali unae anakusubiri!

Na ndio maana wakulima ni maskini
 
Na ndio maana wakulima ni maskini
Umaskini wa mkulima hautokani na dalali bali unatokana na uzalishaji wa kizamani wa kutegemea mvua kwa 100% na pia kutokana na mfumo mbovu wa mnyororo wa masoko! Ajabu ya Watanzania, au inawezekena Waafrika kwa ujumla, hata sehemu zenye vyanzo vya kutosha vya maji kama vile mito na maziwa, bado na wenyewe watasubiri msimu wa mvua ndipo waanze kilimo! Ni kana kwamba tunadhani kinachoweka hai mimea ni mvua na sio maji! Matokeo, zao x linajaa sokoni kwa wakati mmoja kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa sababu wakaulima wa zao husika walilima kwa wakati mmoja. Ukishakuwa na high supply, hakuna jinsi bali ni kushuka kwa bei na hivyo kumfanya mkulima ashindwe hata ku-cover gharama za uzalishaji, na hatimae kuendelea kuogelea kwenye poverty circle!
 
Back
Top Bottom