Nimeviagiza vyombo vyetu vya ulinzi

Mmang'ati

Senior Member
Jan 8, 2011
184
49
Imekuwa ni mazoea sasa kila siku kuwasikia viongozi na watendaji hasa wa jeshi la polisi inapotokea maafa kama ya milipuko ya Arusha kutangaza kuwasaka wahusika popote walipo na kuwachukulia hatua.
Mi binafsi matamko haya yananikera hasa ukizingatia msisitizo unaotolewa lakin mwisho wa siku hakuna ufumbuzi wowote hata harufu tu inayohusiana na kilichotokea.
Ahadi za wanausalama kufanya kazi USIKU NA MCHANA zote zimepotea hewani kama mvuke wa petrol pasi majibu.
Ushauri wangu kwenu viongozi kwa sasa msitoe tena ahadi bali mkifika eneo la tukio tamkeni "kazi ya Mungu hatuna la kufanya"hii itatufariji watanzania na itawajengeeni heshima viongozi kuliko ahadi za tutamsaka mpaka apatikane.
 
Back
Top Bottom