Nimeupenda uwezo wa kufikiri wa viongozi wa CHADEMA. Mchezo mnaucheza vyema

ngichinwe

Senior Member
Oct 15, 2018
156
430
Kuna kitu hamjaelewa.chadema ni watu makini kupita Maelezo, yaani hawa wote wamejitokeza ili kunogesha mchakato ila washajua mgombea ni nani na anajulikana.

Isingekuwa busara hata kidogo kwa chama cha siasa kufanya mchakato muhimu kama huu bila ya kuvutia hisia za watanzania.

Na njia mujarabu ya kufanya hivyo ni kuhakikisha vigogo wa CHADEMA kwa asilimia kubwa wanaingia kwenye kinyang'anyiro ili siku ya uchaguzi wa mgombea macho na masikio ya wapiga kura wote yawe mkutano mkuu wa CHADEMA atapita nani.

Bahati nzuri mwaka huu CHADEMA wana mtu ambaye anaweza kumtoa kamasi Rais aliyeko madarakani na uchunguzi unaonyesha kwamba Rais anamwogopa Tundu Lissu kuliko hata anavyoiogopa korona na ndio maana hata baada ya kuwa sawa kiafya hakurejea nchini kwa sababu haukuwa muda mwafaka.

Hebu fikiria kama Tundu Lissu angerejea mwaka jana, leo hii nani angekuwa anamzungumzia maana jamaa ni mabingwa wa kutengeneza matukio ili kuua hoja au trend ya upinzani.Maana kama juzi tu alitangaza nia ya kugombea, kesho yake Mbowe akavunjwa mguu, baada ya hapo Bunge zima na Serikali ikaanza kazi ya kupotosha ukweli

Msidhani kwamba hayo yamefanyika kwa bahati mbaya walijua kabisa wakimgusa Mbowe basi mjadala mzima utahama toka Tundu Lissu kutia nia na kuanza kujadili kuvamiwa kwa Mbowe, kwa kiasi wamefanikiwa.

Hebu niulize kitu..ni nani anafahamu kwamba baada ya Tundu Lissu kushambuliwa walitengeneza tukio la kushambuliwa yule mwanajeshi ili kutuaminisha kwamba nchi si salama na tukio la Tundu Lissu ni kama hili nani anakumbuka hata hilo sakata liliishia wapi?

Sasa muda sahihi wa Tundu Lissu kurudi ni baada ya kutangazwa rasmi na chama akirejea nchini ile hamasa watu waende nayo hadi siku ya kuimwaga pombe mgaroni.

Viva CHADEMA, viva mwenyekiti, viva viongozi waandamizi wa kamati kuu. Mchezo mnaucheza vyema hakika mwaka huu kama ikipatikana tume huru joka litatolewa pangoni na kukatwa kichwa..
 
Msije mkasema matokeo yalipangwa gizani tu muda ukifika
.
IMG_20200531_072737_186.jpg
 
Usimuamshe aliyelala
 
Magu anamuogopa Lissu kwa sababu dunia nzima macho na masikio yatakuwa hapa...alafu Lissu atue siku ya kwanza ya kampeni...Bongo itazizima
 
Mnajitia moyo, mtapata tabu Sana, endeleeni kumuenzi Mbowe mtashtuka miaka imeenda.
 
Back
Top Bottom