Nimeumizwa sana naomba faraja yenu

Simplelady

Member
Oct 26, 2009
44
22
Habari zenu wana jf. Mchumba wangu nimemfumania na mwanamke mwengine na kwa hasira nikagombana na huyo mchmba wangu, pia niakenda kumwambia huyo mwanamke amwache mchumba wangu. Lakini mwanaume akasema mimi siwezi mwacha huyo mwanamke kwani nampenda.

Nikaamua kuondoka zangu lakini roho inaniuma sana kwa kitendo alichonifanyia huyu bwana na sasa nimekuwa mpweke kwani sikuwa na mwanaume mwingine wa pembeni ambaye labda angenifariji sasa.

Naomba ushauri wenu nifanyeje ili kukabiliana na maumivu haya ya mapenzi?
 
dada, hivi huwa huelewi tunavyokwambia wanaume wengi sana ni WATHINZI? ina maana ha huyo alikuwa kwenye hili kundi! ,Mrudie Mungu atakupa faraja ya kweli, binadamu faraja yao ni ya kitambo tuuu!
 
Muda huponya majeraha. Its okay kuwa mpweke na kukasirika, ila sasa isiwe milele. Jipe muda wa kupona, hakufai wala hakustahili manake sio muaminifu wala mstaarabu. Jiweke busy, soma vitabu, anzisha project itakayokuchukulia muda kwa faida, na ujifanyie mambo yatakayokupa furaha mpya. Kosa kubwa ni kukimbilia kwa mwanaume mwingine, huhitaji mtu wakati uko varuvaru. Jipe muda na furahia maisha yako ya sasa.

Pole sana.
 
pole sana dada kwanza nakushukuru sana kwa kuwa mwaminifu katika mapenzi hakika mungu atakusitiri na kukupa yule anayefaa mtegemee yeye naye atakuwezesha

mimi ntakuweka kwenye maombi ninayofanya na mungu atafanya njia
 
Habari zenu wana jf. Mchumba wangu nimemfumania na mwanamke mwengine na kwa hasira nikagombana na huyo mchmba wangu, pia niakenda kumwambia huyo mwanamke amwache mchumba wangu. Lakini mwanaume akasema mimi siwezi mwacha huyo mwanamke kwani nampenda.

Nikaamua kuondoka zangu lakini roho inaniuma sana kwa kitendo alichonifanyia huyu bwana na sasa nimekuwa mpweke kwani sikuwa na mwanaume mwingine wa pembeni ambaye labda angenifariji sasa.

Naomba ushauri wenu nifanyeje ili kukabiliana na maumivu haya ya mapenzi?
Jipe muda wa kutafakari mahusiano yako na mwenzako na jipe muda ili usiumie tena.Naamini yuko mtu sahihi kwaajili yako anakusubiri.So usikate tamaa wanaume wema wapo na wabaya pia wapo.Kila jema nakutakia!
 
Mmmhhhhhhhh! Ndo imemwagika huna hata kidumu!!!!!!!? Unaloooo hilo! Mimi nikifuga MIZOMBII iso na idadi watu wananirushia maweee!!!!! Saivi wangekuwa wa muhimu kweli mda kama huuuu!!!!!!!

Im not good in SIPMPATHISING an sit back n do nothing, or forgive n forget philosphy!!!!!!! Ngoja nitoke BARUUUUU! Kabla sijachafua hali ya hewa!

Jst incase you decide NOT TO BE A SHMUCK, and do something abt it, like take some REVENGE! to restore your Honour, and take care of those who DISRESPECTED you purposesly CALL ME ILL BE BACK IN WAR MODULE!!!!!!!!

Adios Amigo!!!!!!!!!
 
kha!! mwwngine nae katendwa...kumbe wee ukikuwa just a sexmate..aibu!!! mwaka huu wanaume tupo juu...gegeda alafu unaenda oa mwengine!

kuabaliana na hali alisi...ndio umebwagwa bana sasa chakufanya nikutulizana machungu yatapita baada ya muda ila usipaparikie mwanaume kwa sasa. utaishiwa megwa tuu.
 
Hee?? Mweeehh pole wajameni.........aisee nayajua hayo maumivu yalivyo makali kwako kwa sasa.......

Moja: Usikurupuke kuwa na mwanaume mwingine kwa sasa sababu for sure utakuwa umefanya maamuzi si sahini kwa sana sababu ya kuwa na hasira na maumivu vumilia tu yatakwisha haya wala usijali mdada...............

Tulia kabisa tena kama unaweza ukiona muda huna cha kufanya kanunue/kakodi CD za kina Ray (hata kama huzipendi/huangilii) jitahidi uangalia upoteze muda na ucheke kidogo....... ama tafuta kijishughuli hata kupiga deki/kuosha vyombo nk hapo mawazo yatajikuta yanaondoka

Lingine: Hebu kumbuka yale maudhi amewahi kukufanyia mkiwa wote hapo hutamtamani tena kumuona..............ha ha ha hii ndo njia mie hutumia kumsahau mtu sikumbuki mazuri yake.......................
 
Pole sana kwa yaliyokukuta.Huyo mwanaume alikwisha kukuacha siku nyingi na alikuwa anasubiri tu umfumanie labda baada ya kuona kila analofanya kukuonyesha kuwa hana mapenzi nawe kushindikana ndio maana hata baada ya kumfumania aliweza kukwambia kuwa hayupo tayari kumwacha huyo mwanamke mwenzako.

Inaumiza sana hasa kama ulijitoa kwake kwa mapenzi yote,inauma kalini si mwisho wa dunia na Mungu amekupa nafasi nzuri ya kujua cha kufanya mbele ya safari maana hilo ni fundisho kwako hivyo ukipona maumivu na kutaka kujiingiza tena kwenye mahusiano utajua namna ya kuishi na utatengeneza mazingira mazuri ya kudumu kwenye mahusiano.

Unaweza kutaka kufanya mambo mengi sana kwa sasa kama vile kulipa kisasi na mengineyo lakini bado nakwambia si suluhisho la matatizo uliyonayo,kama u muumini mzuri na unaamini Mungu ndiye kila kitu kwako basi mshukuru Mungu kwa kukuonesha jambo hilo na muombe akutie nguvu na utashinda maumivu uliyonayo.
 
Kila ukitaka kukasirika kunywa maji, huwa yanashusha lile dude linalokaba kooni

Kama huna pesa ya kuanzisha mradi wa maendeleo, anza hata mazowezi yanakusaidia kulala
Kama vipi fikiria kurudi shule ili kujipa hamasa ya maisha zaidi.

Concentrate na maisha yako, yape kipaumbele, yaongezee chachandu

Hii itakusaidia kupitisha muda ukiwa unapona taratibu
 
Muda huponya majeraha. Its okay kuwa mpweke na kukasirika, ila sasa isiwe milele. Jipe muda wa kupona, hakufai wala hakustahili manake sio muaminifu wala mstaarabu. Jiweke busy, soma vitabu, anzisha project itakayokuchukulia muda kwa faida, na ujifanyie mambo yatakayokupa furaha mpya. Kosa kubwa ni kukimbilia kwa mwanaume mwingine, huhitaji mtu wakati uko varuvaru. Jipe muda na furahia maisha yako ya sasa.

Pole sana.

Labda hajui hii kitu hapa chini:
"Anyone can have sex with u but u need to be connected to someone in body, mind and spirit to make Love"
 
Pole mdada,
1.Jipe likizo ya mapenzi kwa muda

2.Usijenge moyo wa kuwachukia wanaume kutokana na hili lililokupata, bado kuna wanaume wema huko nje

3. Mkumbuke Muumba wako maana ni yeye pekee hutoa faraja ya kweli.

4. Epuka muda mwingi kukaa mwenyewe, tafuta shughuli za kufanya kama jogging, kuogelea, kuangalia filamu(zisiwe za mapenzi).
 
naona kama una regrets mbili hapo..

moja regrets ya kuachwa
mbili regrets ya kutokuwa na kidumu...

as if hii issue ya vidumu sasa ni 'kitu cha kawaida mnoo' ..

Kweli sasa dunia ni yako,chaguo ni lako...
 
Take your time kufanya ishu zako, jichanganye na watu utasahau japo it will take time....
kama upo rock city twende malaika tukaogelee
 
Habari zenu wana jf. Mchumba wangu nimemfumania na mwanamke mwengine na kwa hasira nikagombana na huyo mchmba wangu, pia niakenda kumwambia huyo mwanamke amwache mchumba wangu. Lakini mwanaume akasema mimi siwezi mwacha huyo mwanamke kwani nampenda.

Nikaamua kuondoka zangu lakini roho inaniuma sana kwa kitendo alichonifanyia huyu bwana na sasa nimekuwa mpweke kwani sikuwa na mwanaume mwingine wa pembeni ambaye labda angenifariji sasa.

Naomba ushauri wenu nifanyeje ili kukabiliana na maumivu haya ya mapenzi?

Umemfumania akiwa ana do au anaongea na huyo mdada? Maisha ya leo kaazi kweli kweli...
 
Back
Top Bottom