Nimeufurahia utaratibu wa kuwaapisha wateule wa Rais; utaleta heshima na kutodharauliana

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,518
108,794
Nimejulishwa kuwa kuanzia sasa ( Awamu ya Mama japo ya Hayati ilijaribu ila ikatoweka ghafla ) ni kwamba ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Mabalozi, Wakuu wa Idara Nyeti na Wakuu wa Mikoa tu ndiyo watakuwa wanaapishwa na Rais akiwa mbele yao.

Kuanzia Wakuu wa Wilaya, DED na DAS sasa watakuwa wanaapishwa na Wakuu wa Mikoo tu huko ambako wamepangiwa baada ya Kuteuliwa.

Napongeza sana hatua hii ( Maamuzi haya ) kwani kwa Mtazamo wangu GENTAMYCINE nilikuwa naona 'Wateuliwaji' wote hawa ( hasa RC' na DC's ) Kuapishwa na Mheshimiwa Rais ilikuwa ni kutowapa Mipaka yao na hata Kuwafanya DC's wajione wako juu ya RC's wao na wakati mwingine hata 'wakidharauliana' pia.

Sawa DC's wote mmeteuliwa na Mheshimiwa Rais lakini 'Kudadadeki' zenu wote ( nyote ) kuanzia Kesho 'mtaapa' mbele ya RC's sasa ole wenu mkiwa huko mjifanye mpo juu yao au muanze kuwa 'Masnichi' na Kuwapikia 'Majungu' kwa Mama ili 'watumbuliwe' na mpandishwe Vyeo hivyo nyie.

Oya DC mpya wa Siha leo 'Gambe' wapi?
 
Mara nyingi kwa Hayati Dkt. JPM Yeye 'Shoo' zote hizo alikuwa anazisimamia Mwenyewe Ikulu na akimaliza 'Kuwaapisha' anaanza Kuwananga ( Kuwasema ) huku akiwapiga mno 'Mikwara' yake Mbuzi.
Mghwira leo amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya katika hafla fupi ya kuapishwa kwa mteule huyo wa Rais Magufuli katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro,Wakurugenzi,Makatibu tawala wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na ndugu na marafiki wa mkuu huyo mpya wa wilaya ya Hai.

IMG_0891.jpg
 
Pole sana huu utaratibu upo toka JPM akiwa Rais..... pole sana utakuwa ni either una matatizo ya kisaikolojia au una matatizo ya kutofatilia mambo ya msingi
Nilishaliona likifanyika kwa Hayati JPM.
 
Sio kwa DC na DAS
Makonda Kipindi cha Rais JK alipoteuliwa kuwa DC wa Kinondoni aliapishwa na nani? Nikumbusheni upesi.

Je, mna uhakika kuwa katika Uongozi wa Hayati Rais Dk. Magufuli 2015 hadi tarehe 17 Machi, 2021 hawa DC's achaneni na DED na DAS bawakuwahi Kuapishwa nae Ukumbini kwa Upamoja ( Uwingi ) wao?
 
Makonda Kipindi cha Rais JK alipoteuliwa kuwa DC wa Kinondoni aliapishwa na nani? Nikumbusheni upesi.

Je, mna uhakika kuwa katika Uongozi wa Hayati Rais Dk. Magufuli 2015 hadi tarehe 17 Machi, 2021 hawa DC's achaneni na DED na DAS bawakuwahi Kuapishwa nae Ukumbini kwa Upamoja ( Uwingi ) wao?
Hoja yako ni hipi mkuu?
 
Uamuzi mzuri sana, Nawaza Sabaya na Kiburi chake cha "uandakava"feki angeapa kwa mama mghwira kweli? Bora hata JOJO amepelekwa Dar apate mwanaueme aise, maana uzazi kwa wanawake unakoma miaka ikifika 40, sasa ana miaka 35 hana hata mchumba.
 
Mara nyingi kwa Hayati Dkt. JPM Yeye 'Shoo' zote hizo alikuwa anazisimamia Mwenyewe Ikulu na akimaliza 'Kuwaapisha' anaanza Kuwananga ( Kuwasema ) huku akiwapiga mno 'Mikwara' yake Mbuzi.
Siyo kweli; hakuna DC wala DAS aliyewahi kuapishwa na rais katika historia ya nchi hii! Mchukie na mlaumu JPM kwa mambo yoyote yale aliyofanya lakini usimzushie ambayo hakufanya
 
Back
Top Bottom