Nimeuchukia sana Mtandao wa Urais wa CCM 2005...

MSHAURI_WA_NCHI

Senior Member
Nov 10, 2015
139
73
Baada ya kazi nzuri kuanza kufanywa na inayoendelea kutekelezwa na Mh. Rais wetu mpendwa Pombe J. Magufuli nimeanza kuamini mtandao ule wa 2005 umeturudisha nyuma watanzania.

Na hivyo basi ombi langu ni kuwa asiwepo mtu kati yetu wana JF wa kushabikia watu hawa kwani wameturudisha nyuma sana kimaendeleo labda uwe ni sehemu yao kifikra na kimaslai.

KARIBU KWA FIKRA MBADALA.
 
magufuli ana miezi miwili madarakani, bado ana mkataba wa miaka minne na miezi kumi ya kuwatumikia watanzania, kwa miezi hii miwili HAJAFANYA VIBAYA SANA naimani kwa kipindi kilicho baki atawafanyia mazuri zaidi watanzania.

ccm ni ile ile
 
Baada ya kazi nzuri kuanza kufanywa na inayoendelea kutekelezwa na Mh. Rais wetu mpendwa Pombe J. Magufuli nimeanza kuamini mtandao ule wa 2005 umeturudisha nyuma watanzania.

Na hivyo basi ombi langu ni kuwa asiwepo mtu kati yetu wana JF wa kushabikia watu hawa kwani wameturudisha nyuma sana kimaendeleo labda uwe ni sehemu yao kifikra na kimaslai.

KARIBU KWA FIKRA MBADALA.
nakuvulia kofia. hongera kwa ushauri wako mzuri kwa watz kwamba hatupaswi kuwashabikia wanamtandao. si, wameturudisha nyuma tu bali waliharibu kabisa taswira ya ccm mbele ya jamii. waliisaka ikulu yetu kwa udi na uvumba lakini Mungu hakuwa upande wao, wakangukia pua.

nawasihi watz, hasa vijana,tuwatambue wanamtandao na kamwe tusiwape ikulu yetu, watatumaliza. nimewataja vijana kwani uchaguzi uliopita wengi walisombwa na wanamtandao, waliosema wataingia ikulu hata kwa kupitia dirishani. wale waliosema watachukua nchi mapema asubuhi. tuwakatae kabisa hata kama watakuja kupitia chama kingine.

namalizia kwa kuwataka watz wa rika zote kuwa tusijewapa uongozi wa juu wa taifa letu yeyote katika kizazi cha wanamtandao kwani hakuna wa kutufaa hasa wanyonge wa taifa letu.
 
Haina maana kumumunya maneno jk na El wahasisi wa mitandao ndani ya CCM ndio waliotufikisha hapa ,mitandao waliianzisha 1995 baadae wakazulumiana mmoja kaenda kununua chama cha upinzani ili naye atutafune kama kama swahiba wake wa zamani boyz 2 men mwenzake
 
Baada ya kazi nzuri kuanza kufanywa na inayoendelea kutekelezwa na Mh. Rais wetu mpendwa Pombe J. Magufuli nimeanza kuamini mtandao ule wa 2005 umeturudisha nyuma watanzania.

Na hivyo basi ombi langu ni kuwa asiwepo mtu kati yetu wana JF wa kushabikia watu hawa kwani wameturudisha nyuma sana kimaendeleo labda uwe ni sehemu yao kifikra na kimaslai.

KARIBU KWA FIKRA MBADALA.
Wewe utakuwa ni ''a typical Tanzanian!'' Uwezo wako wa kufikiri unaakisi uwezo wa watanzania wengi! Kwanini nasema hivyo? Kwa sababu kitu ambacho kuna watu walikiona kabla ya uchaguzi wa 2005, yaani wakati wakina Kikwete and CO wanafanya kampeni, wewe ndio unaanza kukiona leo! Hata nikisema uwezo wako wa kufiria ni kama nyumbu, nitakuwa nimewadhalilisha nyumbu wote!
 
Huwezi kuizungumzia mitandao bila ya kuzungumzia uhusiano wa wafanyabiashara na viongozi, walijenga uhusiano ambao ulionekana ni msingi wa uongozi wa nchi. Yaani ili uweze kupata uongozi ni lazima ulinyenyekee lile tabaka la wafanyabiashara. Tetesi zinasema kwamba rais wa awamu ya tano alikataa na anakataa kuwanyenyekea wafanyabiashara. Hataki kuiuza nchi, hataki kugeuka kuwa mtumwa wa wachache, ambao walipoumbwa na Mungu hawakupewa kibali cha kuwaongoza kiuchumi walio wengi. Na iwapo waliumbwa ili wahangaike kama walivyo wengine, kwanini waabudiwe na kuonekana eti wanachokifanya ni cha kipekee sana na eti hakiwezi kufanywa na wengine!?. Ni mategemeo ya wengi kuwa rais wa awamu ya tano hana deni binafsi ambalo chanzo chake ni yeye kutaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Yule wa UKAWA na yule wa awamu ya nne ni matunda ya "networks", siamini kuwa udhaifu wa yule wa awamu ya nne usingekuwa pia ni udhaifu wa yule wa UKAWA iwapo angepewa nafasi. Ikiwa yule wa UKAWA ndio alikuwa meneja wa kampeni za rais wa awamu ya nne, sidhani kama angekuja na taratibu za kiuongozi ambazo zingekuwa na uthubutu wa kuwaweka wafanyabiashara mbali na Ikulu. Ni maoni yangu lakini, hayana nia ya kumkwaza wala kumuudhi mtu yoyote yule.
 
wenye akili ndo maana tulimkataa mamvi coz tulishajuta kwa madudu ya mtandao
 
Baada ya kazi nzuri kuanza kufanywa na inayoendelea kutekelezwa na Mh. Rais wetu mpendwa Pombe J. Magufuli nimeanza kuamini mtandao ule wa 2005 umeturudisha nyuma watanzania.

Na hivyo basi ombi langu ni kuwa asiwepo mtu kati yetu wana JF wa kushabikia watu hawa kwani wameturudisha nyuma sana kimaendeleo labda uwe ni sehemu yao kifikra na kimaslai.

KARIBU KWA FIKRA MBADALA.
Na ndo umetulete umasikini mpaka sahivi kama si wao tungekuwa mbali na uchumi ungekuwa unakua kwa 10% ...hawa jamaa wanastahili kupigwa viboko 12.
 
Pombe awafunge Mkwere, Edo, Rostiham na Kalamaji kwa kulipotezea muda taifa na kuliibia kwa miaka 10 mfululizo! Akiwa serious zaidi awanyonge
Ahsante kwa kunisoma Pombe
 
Baada ya kazi nzuri kuanza kufanywa na inayoendelea kutekelezwa na Mh. Rais wetu mpendwa Pombe J. Magufuli nimeanza kuamini mtandao ule wa 2005 umeturudisha nyuma watanzania.

Na hivyo basi ombi langu ni kuwa asiwepo mtu kati yetu wana JF wa kushabikia watu hawa kwani wameturudisha nyuma sana kimaendeleo labda uwe ni sehemu yao kifikra na kimaslai.

KARIBU KWA FIKRA MBADALA.

Mtandao ule ndio uliotufikisha hapa. Lilikuwa ni genge hatari. Mwaka ule (2005) kilichofanyika ni mapinduzi ndani ya CCM ambapo matajiri na CCM maslahi wakiwemo vijana wengi wakafanya mapinduzi makubwa na kushika dola. Utaratibu wa mtu mmoja kura tatu kwa wajumbe wa NEC ukavunjwa na ikawa mtu mmoja kura moja. JK akapita akiwa ni mmoja wa watu watatu waliopelekwa kwenye mkutano mkuu. Lakini pamoja na yote JK amefuta makosa yake kwa kugoma kuwapa madaraka kupitia Lowassa.
 
Namshukuru mungu kumfunua Mhe JK na kutambua madhaifu haya na kujisahihisha kwa kumuunga mkono Magufuli na kumkataa Lowasa mara baada ya kushauriwa vema na baraza la wazee Wa chama.

Ni vema mkatubu dhambi hii kwa mungu.
 
Hapa mjadala unaakisi u Tanzania wetu. Naipenda Tanzania. Nakushukuru MUNGU kutupa akili na ufahamu wa kuukataa uhuni.
 
Daaaa sina LA kusema nchi ilikuwa tuipoteze kama ndo angeingia huyo mamnvi ndo ingekuwa tumekwisha aiseee.
 
kikwete ndiye aliye wachosha watanzania maana maneno na vitendo vili pishana kamasio kupoteana kabisa maisha bora yaka wa kinyume
 
Back
Top Bottom