Nimetupa kiatu cha mke wangu nikidhani ni cha mwanamke niliyempa lift siku iliyopita

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Jana ofisini kulikuwa na kaparty flani cha kumuaga Mkurugenzi wetu ambaye anastaafu.

Rosse ambaye ni mfanyakazi mwenzangu aligida sana pombe mpaka akapoteza network.

So ikanibidi nichukue jukumu la kumrudisha nyumbani kwake na gari yangu.

Nilirudi nyumbani kwangu ila sikumuambia chochote mke wangu sababu namjua ana wivu sana na alishaanza kutuhisi vibaya mimi na Rosse kutokana na ukaribu wetu, siku ikaisha.

Leo mchana mke wangu aliniambia nimpeleke kwa Shishi akale biriani, nikaona sio mbaya siku mojamoja kutoka lunch na mkeo.

Tukiwa njiani mke wangu alikuwa bize kuweka sawa makeup yake, ghafla kutupa jicho chini ya siti aliyokaa mke wangu nikaona kiatu cha kike. Nikajua moja kwa moja ni cha Rosse kutokana na pombe zake alikiacha kwenye gari.

Nikaona huu sasa ni msala shostito akikiona kitawaka wala hilo biriani halitolika tena.

Kimya kimya nikainama kukichukua na kwa umakini wa hali ya juu nikakitupa nje kupitia dirishani.

Nikashusha pumzi nikajua soo limeisha. Tulifika Shishi food kwa mahaba nikatangulia kushuka ili niwahi kumfungulia mlango malkia wangu.

Nikashangaa mwenzangu hashuki kan'gang'ania ndani mara ainame, mara ainuke, mara ageuke huku, mara ageuke kule.

Nikamuuliza "vipi mama tatizo nini tena?" "HONEY HIVI HUJANIONEA KIATU CHANGU KIMOJA, SIJUI KITAKUWA WAPI MBONA NILIINGIA NACHO LAKINI?" Duh dadekiiieee

Wanaume tuna mitihani, Wallahi
 
Hasira zilizidi alikiona kiatu cha Rose lakini kwa hasira macho yakawa hayaoni vizuri akaokota cha kwake akatupa dirishani kikabaki chake cha mguu mmoja na cha Rose

Avae tu na hicho cha Rose kama kinamtosha hata kama rangi tofauti na design tofauti akiulizwa kulikoni aseme ni new fashion ya uvaaji viatu
 
Mbona huo mchana unaousema bado haujafika maana hii post umeituma dk 50 zilizopita na sasa hivi no SAA tank. Au bado una mning'inio was pombe hijaamka?
 
IMG-20210111-WA0000.jpg





Kwahiyo ndio wewe huyu au 🤔🤔🤔
 
huu uzi umenichekesha

Sema mtoa post hujiamini,unashida mahari jichunguze vzr
 
Back
Top Bottom