Nimetumia zaidi ya laki 6 kutengeneza hii website Tanzania haipo. Watanzania tusikariri Blog na Adsense

muvika online

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
375
283
Baada ya kutengeneza App ya kutazama movie zilizotafasiriwa Kiswahili inayoitwa Muvika Online, ambayo niliiweka Google Playstore August 24, 2019 mpaka kufika siku ya leo ambapo naandika thread hii September 17, 2019 App hiyo tayari imeshapakuliwa zaidi ya mara 5,000+ hii nikiwa na maana imeweza kupata download 5,000 ndani ya siku 24.

Haya ni mafanikio makubwa kwangu, nashukuru kwa hilo, kwa makadirio ya haraka ili kuisimamisha App hii nimetumia $25 kununua Code kupitia Codecanyon pia $50 kwa ajili ya kumlipa Developer aweza kufanya reskin kwani unaponunua ni lazima uirekebishe, pia natumia $30 kwa kila update inapotoka hii namlipa Developer aweze kuifanyia App yangu update.

Hivyo nimetumia jumla ya $105 katika kuisimamisha App hiyo, ila ukiachana na hayo kila siku lazima nitumie shilingi 5000 (1000 kwa ajili ya kukodi CD na 4000 kwa ajili ya bando) ili niweze kupandisha movie kwenye App hiyo. Kwa sasa bado sijaanza kupata faida yoyote kupitia app hiyo kwani Google Adsense hawaruhusu App ya namna hiyo kwa ajili ya matangazo.

1568740675561.png


Huo ulikuwa ni utangulizi tu kwani sio jambo lililo nifanya niandike thread hii. Twende kwenye point yenyewe.

Lakini Itambulike kuwa Sijaandika thread hii kwa ajili ya kupromote Website ama App yangu bali kwa ajili ya kuwapa funzo Watanzania wenzangu.

Mnamo mwanzoni mwa mwezi huu wa 09 nilijiwa na wazo kwanini nisetengenze website amabayo inahusika na Micro Task kama vile Amazon Mechanical Turk inayomilikiwa na Amazon, ndipo nikaamua kununua Domain ya $15, VPS ya $20 (ambayo nalipia kila mwezi) kisha baada ya hapo nikatafuta Script ambayo niliinunua $200. Kutokana na mimi kuwa na uzoefu mkubwa sana wa masuala ya Script za Php hivyo kwa upande wa customization sikuhangaika kwani niliweza kuifanya mwenyewe mwanzo mwisho.

Kisha baada ya kumaliza kila kitu, Nikatufa mtu wa kuweza kunifanya SEO hivyo nikamlipa $50. Jumla nikawa nimetumia $285.

1568742687756.png


Jinsi hii Website inavyofanya kazi

Kwanza kabisa kuwa watu wa aina mbili ambao wanatakiwa kujiunga na hii website, wa kwanza ni mwajiri na wa pili ni mfanyakazi. Mwajiri kazi yake inakuwa ni kupost kazi ndogo ndogo (Mfano tuseme kuna Website inalipa kupitia referral hivyo mwajiri anatafuta watu wajiunge kupitia link yake Ili yeye apate pesa za referral), sasa mfanyakazi kazi yake inakuwa ni kufanya kazi ambayo mwajiri ameitoa.

Inatakiwa afanye hiyo kazi kama mwajiri alivyoelekeza na atakapokamilisha kazi atatuma kuthibitisho kinachoonyeza kuwa amemeliza kazi, mwajiri ataikagua kazi na kisha atamlipa mfanyakazi kiasi ambacho website imepanga kutokana na ukubwa wa kazi, ila kazi ambayo mfanyakazi anatakiwa afanye ni ile kazi ndogo ambayo inachukua chini ya dakika 5 kuimaliza.

Hapo nadhani nimeeleweka, ila ili uwe mwajiri ni lazima uwe na mtaji kwa kuwa utatakiwa uweke pesa kwenye akaunti yako ambayo utaitumia kuwalipa wafanyakazi wako kiwango cha chini cha kuweka pesa ni $5 kwa sasa ila mwezi ujao itapanda nakuwa $10.

1568740772210.png


Mbali na hapo ndani ya website yangu kuna referral program ambayo ukimualika mtu ajiunge basi tunakulipa $0.20, ila ni lazima huyo mtu awe amefanya angalau kazi moja sio hivyo tu kwa yule ulie mualika kila akifikisha $5 basi wewe uliemualika tunakupa pia. Ila kwawale wanopenda kutumia trick hapa hamtaweza kwani endapo ukifanya withdraw (ambayo kima cha chini ni $5) basi kabla ya kukulipa ni lazima tuipitie akaunti yako na za watu uliowaalika na tukibaini udanganyifu basi imekula kwako.

Hayo ni macheche tu yapo mengi sana, hivyo napenda kuwafumbua macho blog na adsense sio zenyewe tu ndio zinalipa na ukiaangalia sasa hivi kuanzia Facebook hadi adsense pote wamebana mimi kupitia website yangu naamini ndani ya miezi mitatu ijayo nitaanza kutengeneza pesa za kutosha kutoka na fee mbalimbali kama vile, kwa mwajiri anapoweka kazi yake (Campaign) basi tutamkata $0.50 kama "Approval fee" pia kwa upande wa wafanyakazi tuna fee mara 2, moja kwa kila kazi unayofanya na kulipwa basi tunakukata 10% ya pesa uliolipwa na pili kila unapofanya withdraw basi kuna fee ya 3% ila unaweza kuondoa hiyo fee ya 3% endapo ukialika watu 100 kujiunga na website hivyo utabakiwa na fee ya 10% tu.

Kwa wale wanahitaji kuitazama website yangu basi tazama hapa >> DiaWokers

Ifaamike sijaandika thread hii ili kujipatia watembeleji bali ili kufungua bongo zenu hasa kwa wale wana blogger au wanaotaka kutengeneza pesa kupitia Online

Kwa leo naomba niishie hapa, ila muhimu ninachotaka ni sikiliza maoni na ushauri kutoka kwenu

Pia kwa wale wanao au watakao jiunga kama waajiri kila muda ninapopata nafasi nitakuwa natoa vocha ya $5 ambayo utaweka kwenye akaunti yako na utapata pesa ambayo utaitumia kwenye campaign.

Kwa wale waajiri ingia kwenye akaunti yako upande wa generate/ redeem vouchers na weka hizi code utapata $5 F32BB7D0B4 Tumia hizi $5 ndani ya siku 3 baada ya hapo nitazichukua

View attachment 1210538

Hadi kufikia leo ndani ya Muvika Online tayari nimeisha pandisha Movie 92, Series 6 Pamoja na Live Tv 2
 
Umejiaandaje siku wenye movie zao wakiamua ku log lawsuit? Au huwa unapata kibali chao?
Wenye movie zao unamaanisha waigizaji kama kina Jet Lee? Hapana sina kibali vilevile hao wanaotafasiri hawana kibali cha kutafasiri hizo movie, hivyo wote tunafanya kinyume
 
ila hiyo application ya Muvika it`s a matter of time. Google wataipiga chini due to copyright.
Sio tatizo kwangu maana nitaendelea kuitangaza na watu watakuwa wana download APK na kingine angalia Play Store kuna app nyingi sana za movie na bado hazifungwa na kingine nilichokwepa ni kuwa App yangu haipatikani katika nchi zile kubwa mfano USA, Canada, UK na Germany.
 
muvika online,

It is a very good move lakini kama kweli umetumia hizo gharama basi naona haukupata tech consultation nzuri ambayo ingekuelekeza uinvest kwenye part ipi.

I am a little bit experienced in this field and I had the same app like Muvika Online na ilikuwa na users wengi sana (400+ within 5 days) na hapo nilikuwa bado sijaiweka Play Store but niliipromote tu jukwaa la movies hapa JF.

App za aina hio utapata users wengi sana lakini faida yake ni ndogo sana. Kama unategemea ads itakulimit coz Adsense na Admob hawasapoti apps kama hizo. Unless ujaribu Ad sellers wengine.

Nielewe kwanza lengo langu ni kukushauri kwamba umefanya wrong investment. Sometimes you need to get advice from some experienced people in this field ili wakupe trending ya market ya hizi mambo.

Sababu kubwa hizi tech products za bongo hazitusui na zinakufa baada ya muda ni kwamba watu hawataki kukaa chini wakashauriana na kufikiria kuboresha au kucustomize products za mambele ili zitumike kutokana na mazingira ya hapa bongo.

Utakuta mtu kisa ameona netflix anataka atengeneze vile vile netflix yake ya kibongo na aiite 'swahiliflix' bila kujua netflix ilitengenezwa kutokana na mazingira ya wenzetu huko mambele. Sikatai kuiga lakini nasisitiza kuiga kwa kutumia akili. Yaani boresha kidogo ili iwe customized kwa ajili ya audience yako (hapa naongelea hiyo web yako)
 
1568802124880.png


Hadi kufikia leo ndani ya Muvika Online tayari nimeisha pandisha Movie 92, Series 6 Pamoja na Live Tv 2
 
kali linux Gharama za matangazo kwani huwa natumia Twitter Ads katika kuipromote, sijaweka gharama kwakuwa kwenye Twitter Ads huwa natumia janja janja napata $50 za kufanyia promotion, gharama inakuja kwenye kununua akaunti za Twiiter ambapo akaunti moja nanunua kwa $5 huwezi pata download 5000 pasipo promo za aina yeyote
Sijaongelea hilo labda haujaelewa nilichomaanisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom