"Nimetumia zaidi ya 20,000 katika matangazo lakini sijapata Faida, nifanyeje?" - JINSI NILIVYOMSHAURI

Max Marketer

Member
Oct 13, 2020
46
49
Habari za leo wakuu,

Leo nimerudi tena and hopefully tutakuwa pamoja kuendelea kujifunza kuhusu social media marketing and advertising

Leo nataka nishee nanyi jibu ambalo nililitoa baada ya kuulizwa na mfanyabiashara ambaye nilimfundisha kufanya sponsored ,alikuwa hafahamu kabisa lakini hatimaye akawa ameanza kufanya mwenyewe

Aliniuliza "itanichukua muda gani kuanza kuona returns, maana nimetumia zaidi ya 20,000 katika sponsored ads lakini sijapata faida yoyote bado.. Au niweke hela zaidi?

Hili swali nilivyoliangalia nilitambua linahitaji majibu katika angle 2, yaani upande wa mindset kwanza and then Upande wa Strategies.

Pamoja na vitu ambavyo vinaweza kufanyika ili kuweza kuona return ya hela aliyoitumia kama bajeti ya matangazo (20k+)

Nikamuuliza what's your Goal?..unapotangaza huwa unalenga utimize lengo gani?

Hapa lengo ni kuijenga mindset ili ufahamu ukiweka hela yako, utapimaje matokeo kama umefanikiwa au lah.

Unapofanya matangazo, kuna malengo ya Aina 2 ambayo unatakiwa kuwa nayo na kwenda nayo sambamba

1.KUJENGA AWARENESS
2.KUPATA WATEJA au LEADS

Hivyo basi inabidi uhakikishe tangazo lako linalenga moja kati ya hivyo vitu 2,.. mtu akufahamu, akutafute au anununue kabisa.

Pia kuna aina mbali mbali za matangazo unayoweza kufanya kwa kila aina ya goal,

Mfano kuna matangazo ya kuuza directly, kuna matangazo ya kutafuta leads, Na pia mengine ya kujenga awareness..

Usitegemee tangazo la aina moja kukamilisha yote hayo.

(We'll dive deep into these Ad types in upcoming posts)

Baada ya kuweka mindset sawa na ukatambua nini unataka kuachieve,

Tunaweza sasa kwenda sehemu ya pili ya mbinu ili kuhakikisha matangazo yako na hela unayotumia inakuletea Faida.

Kwa case kama hiyo, Vitu hivi 3 ni muhimu zaidi kuviangalia na kuboresha.. Hasa hasa Kama unaona unaweka hela ktk Ads na hupati faida

1.Unatoa OFFER gani (Bidhaa/huduma)

- Hapa simaanishi ofa zile za discount, Bali namaanisha unauza nini na mteja wako anapata faida gani kutoka kwako?

- Lazima ufahamu hichi kitu, kwani kupata wateja online inaweza kuwa rahisi au vigumu kulingana na biashara unayofanya.

- Kuna baadhi ya biashara Kama wauza nguo, viatu, pochi, simu, electronics ni rahisi kupata wateja..

-Lakini biashara nyingine zinahitaji mteja apitie hatua tofauti tofauti mpaka aje kununua (sales funnel),

Mfano mzuri biashara ya huyu aliyeniuliza swali (hospitality industry).

- Inabidi utambue biashara yako and how to position your offer, ili uweze kupata wateja wa kutosha

2.USHAWISHI KWA WATEJA ILI WAKUTAFUTE

- Hiki ni kitu muhimu pia, ukiangalia matangazo mengi yako boring hayana hata chembe ya ushawishi kwa mteja

- Unakuta mtu kaandika tu maelezo kama essay, matokeo yake anakosa watu despite kuwa ana bidhaa/huduma nzuri tu

- Please jitahidi katika ushawishi,mpe mteja sababu ya kukutafuta Mfano weka Free Delivery, Toa 20% discount , Free samples, Yani weka viofa ofa vya hapa na pale ili umpate mteja.

- Ukishampata mteja kwa mara ya kwanza,ni rahisi kwake kununua kwako tena na tena Kama Huduma itakua nzuri .

- Kazi ya Sponsored ni kukuletea wateja kama hao, na wewe unawafanya kuwa loyal customers.. That's how your business will grow

3. TANGAZO LAKO LINA UBORA UNAOTAKIWA?

- Hili swala la matangazo ya sponsored nimeliongelea kwa kina in my e-book, na nimeweka mifano zaidi ya 30 ya matangazo mazuri ya kuigwa (Facebook and Instagram)

- Hapa kuanzia picha/video/graphics unazotumia ktk matangazo yako, tunakuja pia ktk maelezo (ad copy) na call to action zako

- Hivyo vitu inabidi vikae sawa, ili kuweza kuwashawishi wateja wako na kuwafanya waweze kununua au kukutafuta.. Picha ikiwa nzuri huku maelezo hayajakaa sawa, utaishia kupata likes kibao na comments za kuuliza bei, lakini wateja inakuwa shughuli

- There are multiple ways to advertise your business, make your ads, kuwa creative na hakikisha matangazo yako yanavutia

MY FINAL ADVICE

- Kuna mdada mmoja ni mtaalamu kweli kweli katika matangazo (Facebook ads) anaitwa Sally , huwa anasema ukitaka kufanikiwa katika ads "TEST, DON'T GUESS"

- HIvyo nilimshauri mfanyabiashara huyu kuangalia vitu hivyo, na kurekebisha kisha kuendelea kufanya ads kwa malengo zaidi

- Uzuri wa matangazo ni hesabu eventually,

- Mfano mimi kuna tangazo nilitumia $2~4000tsh, lakini nlipata mteja aliyelipa Tsh 60,000/= ..Hivyo ukifahamu mteja wako analipa kiasi gani, you can spend enough money to get them

Finally

- Kama unahangaika kutafuta wateja online, unatamani kufanya sponsored kweli lakini hujui pa kuanzia, au unafanya lakini hupati wateja wa kutosha

- Ninayo e-book ambayo nimeiandaa ikusaidie kujifunza vitu hivyo, hatua kwa hatua, na kukurekebisha makosa yapi hutakiwi ufanye katika sponsored plus more

- Nimeweka picha zake apo, kama utahitaji e-book hii

- Tuma ujumbe "E-BOOK" kwenda 0752226475 whatsapp, nitakupa utaratibu

Asante sana kwa kusoma, tukutane Next lesson

------------------------------
By : Max Marketer Tz
Social Media Marketing and Advertising
Q1.jpg
Q3.jpg
Q2.jpg
SUMAKU-P1.jpg
EBOOK-LESSONS.jpg
 
Asante kwa tangazo zuri.

Na namba ya simu...

E-book sh ngapi hiyo? Kuna mtu nadhani itamfaa
0752226475 .... Nitumie ujumbe whatsapp kuna additional benefits ambazo kila mteja wa e-book anapata ikiwemo my personal support katika mchakato wa kufanya sponsored ads vizuri... Bei 10,000/= Tu
 
Mimi nilifikiri lengo la kutangaza biashara ni moja tu kupata wateja hence pesa!
 
Asante kwa somo hili

Niliagiza mzigo wangu kutoka China ni Mzigo wa school bags, Bahati mbaya mzigo ulichelewa kufika ukifika wiki ambayo shule zimefunguliwa 😪

Nikaona isiwe tabu acha nifanye ads kubust mauzo

Budget ilikua 10$

Katika hiyo Nimefanikisha kupata wateja watatu mmoja kati ya hao alimleta mwenzie so nikauza bags 3 tu. Lakini nilipata Simu na text kutoka sehemu Mbali na nilipo changamoto niliyoiona ni UAMINIFU mteja akisikika uko mkoa flani unasikia anaguna Nafikiria anawaza kutapeliwa hivyo Biashara inafia hapo (hapa kama kuna mtaalam ANISAIDIE kutatua hili)

Lakini kati ya wale walionunua wako mkoa tofauti lakini walituma hela na jana kanijulisha AMEPOKEA mzigo wake.

So nimejifunza sana somo hili NITAKUTAFUTA mkuu
 
Asante kwa somo hili

Niliagiza mzigo wangu kutoka China ni Mzigo wa school bags, Bahati mbaya mzigo ulichelewa kufika ukifika wiki ambayo shule zimefunguliwa 😪

Nikaona isiwe tabu acha nifanye ads kubust mauzo

Budget ilikua 10$

Katika hiyo Nimefanikisha kupata wateja watatu mmoja kati ya hao alimleta mwenzie so nikauza bags 3 tu. Lakini nilipata Simu na text kutoka sehemu Mbali na nilipo changamoto niliyoiona ni UAMINIFU mteja akisikika uko mkoa flani unasikia anaguna Nafikiria anawaza kutapeliwa hivyo Biashara inafia hapo (hapa kama kuna mtaalam ANISAIDIE kutatua hili)

Lakini kati ya wale walionunua wako mkoa tofauti lakini walituma hela na jana kanijulisha AMEPOKEA mzigo wake.

So nimejifunza sana somo hili NITAKUTAFUTA mkuu
KUHUSU KUPATA WATEJA WA MBALI

Nakushauri hiyo Ads ungeiset itembee kwenye Mkoa wako unaoishi tuu.. ungepata watu wengi zaidi wanaoishi hapo.




KUHUSU SUALA LA UAMINIFU

Kwanza jijengee mazingira ya kuaminika mfano :-

1) watu wakujue wewe mwenyewe, kikawaida mtu hawezi kufanya biashara kutoka kwa mtu asiemjua hata Abc zake, Mfano wewe hapo umeagiza mziko kama ni kupitia alibaba au kwengineko baada ya wewe kuwafahamu vizuri na kuwaamini japo kwa asilimia ndogo.


2) Wajue location yako/Office yako, ikitokea mtu amepata matatizo kwenye bidhaa yako akupate wapi ? ukisema atakupata kupitia simu tuu bado haijakaa sawa maana hata matapeli nao hutumia simu na zimesajiliwa kabisa na TCRA.


3) Wajengee watu imani kwamba unao uwezo wa kumfikishia mzigo wake popote alipo (katika sehemu ambazo unao uwezo huo) na ikitokea mzigo umepotea mikononi mwako au kuharibika basi unao uwezo wa kuurefund.



ni hayo kwasasa!
 
KUHUSU KUPATA WATEJA WA MBALI

Nakushauri hiyo Ads ungeiset itembee kwenye Mkoa wako unaoishi tuu.. ungepata watu wengi zaidi wanaoishi hapo.




KUHUSU SUALA LA UAMINIFU

Kwanza jijengee mazingira ya kuaminika mfano :-

1) watu wakujue wewe mwenyewe, kikawaida mtu hawezi kufanya biashara kutoka kwa mtu asiemjua hata Abc zake, Mfano wewe hapo umeagiza mziko kama ni kupitia alibaba au kwengineko baada ya wewe kuwafahamu vizuri na kuwaamini japo kwa asilimia ndogo.


2) Wajue location yako/Office yako, ikitokea mtu amepata matatizo kwenye bidhaa yako akupate wapi ? ukisema atakupata kupitia simu tuu bado haijakaa sawa maana hata matepeli nao hutumia simu na zimesajiliwa kabisa na TCRA.


3) Wajengee watu imani kwamba unao uwezo wa kumfikishia mzigo wake popote alipo (katika sehemu ambazo unao uwezo huo) na ikitokea mzigo umepotea mikononi mwako au kuharibika basi unao uwezo wa kuurefund.



ni hayo kwasasa!
Asante sana Mkuu nimelichukua hili
 
Back
Top Bottom