Nimetumia hela vibaya, ndugu zangu wanateseka. Moyo unaniuma

Maleven

JF-Expert Member
Sep 8, 2019
614
2,721
Naandika haya atleast kupunguza majonzi nilionayo moyoni.

Mimi ni kijana kutoka familia masikini sana, nimebahatika kupata kazi, nitazungumzia mshahara wa october.
Baada ya kupokea 280,000 kama mshahara wangu, nililipa elfu 60 deni lililokopa katikati ya mwezi, kisha nikamtumia mama elfu 10, nikamtumia mdogo wangu hela ya shule elfu 15 na rafiki yangu anaeoa machango wa 15 elfu. Roughly nilibakiwa na kama 180,000. (laki na themanini).

Sasa sijui imekuaje (naomba nisiseme ilivyotumia) ndani ya usiku mmoja nikatumia shiling 90 elfu kwa starehe tu za ajabu. Imeniuma sana kutokana na hali ya maisha ya nyumbani, ndugu zangu wengine hata kula ni shida. Sasa nimebakiwa na 90 elfu ambayo inabidi inifikishe mwisho wa mwezi wa kumi na moja.

Ni hayo tu ndugu zangu, siwezi kumwambia mtu huku
 
Hebu tuanze na hao ndugu zako:-

Ni watoto wadogo?

Ni wakubwa lakini ni wanafunzi na kwahiyo hawawezi kufanya shughuli ya ziada,

Ni wakubwa lakini wana ulemavu au magonjwa ya kudumu yanayowafanya washindwe kufanya kazi, au

Ndo ile midume na mijike ambayo unaikuta ina mikono miwili, miguu miwili, macho safi kabisa, hata ukucha haujang'oka, lakini ipo ipo tu inasubiri Bi Mkubwa afanye mambo, na yenyewe ikakae mezani?!

Sema dah, sijui kwanini nimejisikia uchungu sana ulivyoipigia bajeti hiyo 280K!! Yaani 280K bado kuna wengine wanakutegemea hapo hapo. Afrika tuna safari ndefu sana!

Ila unajua nini?! Kama huo ndo mshahara wako wa kwanza, poa tu... lazima uonje japo kidogo kile wanacho-enjoy vijana wenzako! Nakumbuka kazi yangu ya kwanza nilifululiza vyuku vya kienyeji mwezi mzima... asubuhi hadi jioni hadi ikafikia wakati nikimuona kuku tu anatembea, nikawa najisikia kama anataka kukimbilia tumboni jinsi ambavyo walinikifu!!!

Kwanini nisifululize vyuku wakati mkataba ulikuwa unahusisha posho ya Sh 55K kwa siku kwa miezi 2?!
 
Tunajifunza kutokana na makosa. Next time utakua makini. Usijirahumu sana mzee.
 

Similar Discussions

40 Reactions
Reply
Back
Top Bottom