Nimetukanwa na mke wa jirani yangu!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Kuna familia moja imejengea karibu kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi nikamshauri kwamba Wkend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.

From there onward inapotokea mmoja wetu amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya Weekends au public holidays.

Majuzi nilikuwa na Business moja ya kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni Bar moja ya karibu mtaani kwetu.

Mida ya saa moja na nusu usiku tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi 'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.

Baadaye jamaa akazima simu yake, tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani, akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.

Nimeumia sana kwasababu hata siku moja huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama ananiambia nimpuuze tu mkewe.
 
Kwa nini huyo mwanamke asiongee na mumewe aje kukufuata wewe?

Kama wake wenyewe ndio hawa, one can't even have a beer with buddies, marriage is overrated.

Sasa kama kamshindwa mume wake, anakulaumu wewe, wewe ukakata contact akaja rafiki mwingine napo atataka huyo mwingine asinywe bia na mumewe? Kama anataka mumewe asiwe na marafiki kwa nini asimwambie hivyo mumewe?

Unaweza kuivika dunia nzima zulia ili mguu wako ukikanyage ardhi, au unaweza kuvaa viatu tu.

Matatizo ya ndoa ni ya ndani, utatuzi uanzie ndani.

Tutasepa tu.
 
Mshtaki kwa kukutusi kwenye simu ili ashike adabu,.

''Mbwa akikuzoea hata msikitini ataingia na wewe''
 
nadhani hapo cha kwanza kufanya ni kumshirikisha mkeo kilichotokea ili yatakapojiri ya kujiri awe muelewa,pili mpuuzie huyo wife wa jamaa na jamaa jaribu kuwa naye mbali kidogo au mpe kitu live bila chenga then mind mambo yako km wewe kwani b4 ulikuwa na wakina nani?? but pole sana unajua siri ya nyumba iko kwa ukuta wa master bed room
 
Mvaa Tai, block namba ya huyo mama. Usimjibu chochote na kama ni mimi nongemuelezea mke wangu kabisa. Hana nidhamu kabisa, anawezaje kumconfront mume wa mwanamke mwenzie?
 
Last edited by a moderator:
Kuna familia moja imejengea karibu kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi nikamshauri kwamba Wkend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.

From there onward inapotokea mmoja wetu amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya Weekends au public holidays.

Majuzi nilikuwa na Business moja ya kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni Bar moja ya karibu mtaani kwetu.

Mida ya saa moja na nusu usiku tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi 'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.

Baadaye jamaa akazima simu yake, tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani, akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.

Nimeumia sana kwasababu hata siku moja huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama ananiambia nimpuuze tu mkewe.
sali rozari ya huruma ya Mungu, Kwa ajili ya mateso makali ya YESU
 
Mpuuze tu, mpuuzi dawa ake kumpuuza
pia tafuta njia umfikishie ujumbe kuwa hujapendezwa na upuuzi wake mambo yake na mumewe hayakuhusu

Kinachouma huyu ataendelea kuwa jirani yangu permanently, mbona maisha ya huku kununiana yatakuwa magumu sana?
 
mpuuzie kutokujiamini ndo kunamsumbua........ sasa mwanaume anawahi nyumbani ili afanye nini mwishowe aanze kukutuma maji ya kunywa loh.....! wakati we upo bussy na jiko mwanzo wakuanza kukerana hapo.....
 
Back
Top Bottom