Nimetolewa mdudu mkubwa kwenye kidonda kidogo kilichoanza kama punye: Ameingiaje?

Hiyo hutokea pale mdudu haswa hawa warukao wanapoacha yai kwenye kidonda kidogo sana juu ya ngozi yako...

Baade kile kidonda kikija kufunga na mdudu humea ndani...

Wengine hutolewaga kwenye masikio, vichwani, kwenye kuta za vidole...


Cc: mahondaw
Duuuuuhh
 
Hadi mwili umesisimka.
Nakupa pole dada imekuwaje ukashtuka hivyo?? Hujawahi kukumbana naye huyu mdudu?? Je, una mtoto? Je, maisha yako ni matawi ya juu au ya kati?? Kama ni ya kati, ukiwa na watoto 3 hivi hili laweza kukupata au mtoto
 
Hawa huwa wanang'ata wanaingia wanakuwa wadogo kama viroboto. Kadri anavyonyonya dam anakua hadi anakuwa mkubwa
 
Asante sana daktari, bado sijasafisha. Nitapata shida gani?
Kama mdudu alitoka mzima bila kutumbulikia humo akaacha usaha wake na weye ukiwa na afya tele mbona unapona vizuri tu. Huyo funza haachi chochote ndani. Ni msafi sana ka alivyo mweupe.

Ule unyevunyevu unaotokelezea nje ndiyo uchafu anaoutoa. Hana mavi kwa sababu anakutegemea weye kumlisha chembechembe bora zinazoulisha mwili wako.

Hivyo kama mwili utoavyo jasho kama kuisafisha damu naye ndivyo kwa sababu hujiunganisha nawe kama sehemu ya mwili wako
 
Naona kidonda kinaanza kukauka, nikakitumbue tena niioshe na hiyo iodine hospitalini?
Nimeshakujibu kwamba; Huna haja ya kuogopa chochote. Mwili wako una kinga tosha kabisa kujiponya. Huyo mdudu haachi chochote ndani yako kwa sababu huishi nawe kama part of yu. Kuosha huwa tunaosha kusiingie tatizo jingine kwani ni kama umepafungua
 
Aliwahi kunitokea nikiwa f2 nilifanya siri baada ya kumchomoa kidonda kulipona ila kamebak kakovu.
Wife anauliza hili kovu la nn....namdanganya lilikuwa jipu...
 
Mimi kama Doctor ila si wa aina ya Mshana Jr nasema hivi, kuna dalili wewe unaingia chumvini. Moja ya side effects za kuingia chumvini ni hizi zako, wahi muhimbili kwa upasuaji kabla hao wadudu hawajamultiply na kukuota sehemu za haja kubwa.
 
Pole sana. Kuna nzi fulani wakubwa sana, wenye rangi ya kahawia. Hupenda kuruka kwa kelele sana yaani sauti kubwa tu. Akitua mahali saa hiyo hiyo hutaga kiwavi hai. Huyu kiwavi ni sharp sana kujichimbia chini ya ngozi haswa kama akikuta kuna ulowevu wa maji maji. Yaweza kuwa maji maji ya jasho, mkojo au nguo ambayo haijakauka vyema na kupigwa pasi...

Hapa funzo ni kunyoosha kwa pasi nguo unapoanika nje. Hao wadudu huacha mayai yao kwenye nguo hasa chupi. Waathirika wakubwa ni watoto wanaotumia nepi.
 
Aliwahi kunitokea nikiwa f2 nilifanya siri baada ya kumchomoa kidonda kulipona ila kamebak kakovu.
Wife anauliza hili kovu la nn....namdanganya lilikuwa jipu...
Shemeji yuko humu kaona, ngojea aje ukwambie ukweli
 
Mimi kama Doctor ila si wa aina ya Mshana Jr nasema hivi, kuna dalili wewe unaingia chumvini. Moja ya side effects za kuingia chumvini ni hizi zako, wahi muhimbili kwa upasuaji kabla hao wadudu hawajamultiply na kukuota sehemu za haja kubwa.
Doctor umeniogopesha, Mhimbili kitengo kipi?
 
Kama mdudu alitoka mzima bila kutumbulikia humo akaacha usaha wake na weye ukiwa na afya tele mbona unapona vizuri tu. Huyo funza haachi chochote ndani. Ni msafi sana ka alivyo mweupe. Ule unyevunyevu unaotokelezea nje ndiyo uchafu anaoutoa. Hana mavi kwa sababu anakutegemea weye kumlisha chembechembe bora zinazoulisha mwili wako. Hivyo kama mwili utoavyo jasho kama kuisafisha damu naye ndivyo kwa sababu hujiunganisha nawe kama sehemu ya mwili wako
Asante kwa ufafanuzi mzuri
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom