Nimetolewa mdudu mkubwa kwenye kidonda kidogo kilichoanza kama punye: Ameingiaje?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,198
6,416
Halo JF Doctor.

Hivi karibuni kama juma moja limepita, nimetokewa na kipunye mgongoni na kadri siku zilivyoenda ilivimbisha eneo kubwa mgongoni na niliimwa sana Leo usiku.

Kutokana na maumivu makali nilimwambia laazizi wangu awashe taa aicheki Leo usiku. Baada ya kuangalia alisema kuna usaha na majimaji. Alikitumbua na kutokea mdudu mkubwa kama wale watokeao kwenye mizoga.


Doctor aliingiaje wakati Mimi ni msafi na kila wakati nimevaa nguo na mgongo haupo wazi?

Asante kama utanijibu maana tuna wasiwasi sana.
 
Pole sana. Kuna nzi fulani wakubwa sana, wenye rangi ya kahawia. Hupenda kuruka kwa kelele sana yaani sauti kubwa tu. Akitua mahali saa hiyo hiyo hutaga kiwavi hai. Huyu kiwavi ni sharp sana kujichimbia chini ya ngozi haswa kama akikuta kuna ulowevu wa maji maji. Yaweza kuwa maji maji ya jasho, mkojo au nguo ambayo haijakauka vyema na kupigwa pasi.

Huwezi amini ila kale kaulowevu kadogo na kama kuna uchafu wowote wenye harufu mbaya tu, tiyari huyo kiwavi anafanya njia kuingia mwilini. Akiingia ndio ataanza kutaka kuishi juu ya damu yako ka mlo wake. Atajishibisha haraka sana na kuvimba. Huu ni mtindo wa wadudu kama funza anavyoingia akiwa kwenye form ya kiroboto mdogo halafu anageuka bonge la mdudu ka kitunguu ghafla chini ya siku 3. Huwezi amini ila ana uwezo wa kujirutubisha mwenyewe na kutaga mayai yenye rutuba kamili na kuwa funza hai wengi tu. Ukubwa wake ndio huozesha tissue yote iliyomzunguka na kusababisha joto kali.

Usidhani kuwa kuoga kwako ndo kutamuua bali kunaifanya nyama iliyomzunguka kuwa laini na anajipanua bila shida.
Tiba, kumung'oa tu na kusafisha eneo hilo kwa iodine tincture.
 
Asante kwa ufafanuzi wako mkuu hata mm ilishantokea lkn kitambio sana miaka ys 90 huko secondary. Asikuwmbie mtu ilinitesa sana kwa mawazo na nilifanya siri nikapona kibingwa hakuna niliemwambia kwani nilihisi ni uchafu wa kiwango cha juu sana.
Pole sana. Kuna nzi fulani wakubwa sana, wenye rangi ya kahawia...
 
Asante kwa ufafanuzi wako mkuu hata mm ilishantokea lkn kitambio sana miaka ys 90 huko secondary. Asikuwmbie mtu ilinitesa sana kwa mawazo na nilifanya siri nikapona kibingwa hakuna niliemwambia kwani nilihisi ni uchafu wa kiwango cha juu sana.
Huyo nzi hana saa maalum ya kushambulia. Huyo kiwavi akiisha zaliwa anajificha hapo kwenye ulowevu kimya akingojea saa ya mashan=mbulizi. Hivyo, wewe hutajua saa ameshambulia. Yawezekana umeikalia hiyo nguo kwa ghafla tu naye akabamba.
Si lazima iwe ni kwako, hata kwenye gari, hospital, church etc.
 
Hadi mwili umesisimka.
Pole sana. Kuna nzi fulani wakubwa sana, wenye rangi ya kahawia. Hupenda kuruka kwa kelele sana yaani sauti kubwa tu. Akitua mahali saa hiyo hiyo hutaga kiwavi hai. Huyu kiwavi ni sharp sana kujichimbia chini ya ngozi haswa kama akikuta kuna ulowevu wa maji maji. Yaweza kuwa maji maji ya jasho, mkojo au nguo ambayo haijakauka vyema na kupigwa pasi...
 
Pole sana. Kuna nzi fulani wakubwa sana, wenye rangi ya kahawia. Hupenda kuruka kwa kelele sana yaani sauti kubwa tu. Akitua mahali saa hiyo hiyo hutaga kiwavi hai. Huyu kiwavi ni sharp sana kujichimbia chini ya ngozi haswa kama akikuta kuna ulowevu wa maji maji. Yaweza kuwa maji maji ya jasho, mkojo au nguo ambayo haijakauka vyema na kupigwa pasi..
Asante sana daktari, bado sijasafisha. Nitapata shida gani?
 
Huyo nzi hana saa maalum ya kushambulia. Huyo kiwavi akiisha zaliwa anajificha hapo kwenye ulowevu kimya akingojea saa ya mashan=mbulizi. Hivyo, wewe hutajua saa ameshambulia. Yawezekana umeikalia hiyo nguo kwa ghafla tu naye akabamba.
Si lazima iwe ni kwako, hata kwenye gari, hospital, church etc.
Naona kidonda kinaanza kukauka, nikakitumbue tena niioshe na hiyo iodine hospitalini?
 
Hiyo hutokea pale mdudu haswa hawa warukao wanapoacha yai kwenye kidonda kidogo sana juu ya ngozi yako...

Baade kile kidonda kikija kufunga na mdudu humea ndani...

Wengine hutolewaga kwenye masikio, vichwani, kwenye kuta za vidole...


Cc: mahondaw
 
Freed Freed Umenikumbusha mbali sana mkuu, kule kwetu wakati tunakuwa hayo yalikuwa kitu cha kawaida, tukiyaita "amanyorosi" Duuh!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom