Nimetoa machozi leo;ukija kwako ufanyie kazi pls

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,947
22,096
Ndugu wapendwa,

Jumamosi iliopita saa saba na nusu mchana kwa walio Tanki bovu kule chini jiran na Mh Mboma wanakumbuka kilitochotokea
nikiwa na mama Didy nje tunapata juice ya origin kutoka kwa bibie huyo, akapita kijana mmoja ameshika baibo na kitambaa cha kupangusa majasho huku anaubiri.

Alipofika nilikuwa interested nae maana alikwenda kwa mzee mmoja jiran yangu kumsilamu akaanza kuhubiri yule baba akaanza kumtukana akamwambia nitakukata mapanga hapa kwangu toka nakwambia yule bwana akarudi mpakani kwangu na kwa huyo mzee akaendeleea kuhubiri, akasema ametoka Tandik, hajui amefikaje lakini ametumwa kwenye hiyo nyumba huu ndio wakati muafaka muamue moja leo hii kumpokea Yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yenu.

Yule baba akaendelea kumfwata yule kijana akaingia kwangu akiendelea kuhubiri akamtuma mtoto aje kwangu nimfukuze, nikamjibu hao ni masihi wa Mungu siwajui naweza kumfuka Yesu.

Yule bwana akuacha kulia jamani na kusema amewiwa kuomba wenye nyumba hii wampokee Yesu hawajui na hawamjui ..ila mwishoni nakumbuka akasema nikiwa kama mtumishi namasihi wa Mungu naomba niweke wazi nimenawa na ujumbe niliotumwa nimewaachia, mkipenda ufanyieni kazi.

Alintoa machozi nikaomba ale kwangu akakataa kabisa akasema ameonyeshwa huu mtaa anahitaji kuzunguka huku anahubiri, nikampa maji akanywa akaondoka na chupa nikampa alfu kumi, akasema hapana nikamwomba basi chukua hata alfu tano akakataa nikamwambia ubarikiwe mungu azidi kukutia nguvu.

Ndugu zanguni naelekea nyumban muda huu niko hapa plaza nimepigiwa na wife yule mzee amefariki muda si mrefu kisukari kimepanda gafla

Ndugu yangu pengine haitakujia nafasi kama hii kwako itakuja kwa njia nyingine, mwombe Mungu akusaidie kuuchukua ujumbe na kuufanyia kazi yule kijana ajui wala atambui kilichoteka leo mchana wanamzika jion hii; Mungu wa rehema awape rehema na uvumilivu wafiwa

Bwana ametoa .......ametwaaaaaaaaaa
 
thanx mkuu

Siku zote usimdharau usiyemjua!

R .I. P baba uliyekataa kupokea ujumbe.
 
Huwa tunapokuwa na uhai tuna ubishi sana na mambo ya Mungu lakini tunasahau kuwa Mungu na Neno lake halibadiliki liko pale pale ila sisi tunabadilika kulingana na tunavyofanikiwa na kupata kiburi cha uzima
 
yaani nimeuzunika sana ni jiran yangu alienipokea nikiamia mbezi beach kwa kweli imeuma mbaya sio yeye kufa bali wappi alipo sasa ndicho kinachoniuma jamani na imenikumbusha vita vyetu si ju ya damu nanyama ,nikakumbuka aliposhika lile panga alikuwa anamfwata nani akujua
anaenda kumkata YESU aliemjia kupitia kijana Mungu atusaidie nimeomba niweke hii sijui wako atakuja kwa njia gani ukamfukuza kama hivi
MUNGU atusaidie
 
sad story, kwa bongo ni kuwa makini sii kila mtu atakuwa anahubiri kiukweli ni kumchunguza anaekuja kwako wengine wanatumia njia kama hizi kuchunguza nyumbani kwako usiku wanakujia wazee wa kazi. mtumishi wa kweli ndio kama huyu haombi hela wala chakula bali mwenyeji ndio huamua kumkirimu..
 
Ooooohhh!
Wengi wetu tukiwa approached kwa njia hii tutapatikana!
Kaa ukimwomba Mungu aulainishe moyo wako!
Mbishi huyo na arehemiwe!
 
Ujumbe wa kijana yule, haukuwa mahsusi kwa yule baba marehemu, bali kwa wale waliobaki. Huyo baba kwa jinsi alivyokuwa mkaidi katika maisha yake huko nyuma, Mungu ameutumia huo ukaidi kama ishara kwa walengwa kwa nia ya kusababisha wakovu wao.
R.I.P baba mbeba panga dhidi ya mjumbe.
.
 
Ndugu wapendwa,

Jumamosi iliopita saa saba na nusu mchana kwa walio Tanki bovu kule chini jiran na Mh Mboma wanakumbuka kilitochotokea
nikiwa na mama Didy nje tunapata juice ya origin kutoka kwa bibie huyo, akapita kijana mmoja ameshika baibo na kitambaa cha kupangusa majasho huku anaubiri.

Alipofika nilikuwa interested nae maana alikwenda kwa mzee mmoja jiran yangu kumsilamu akaanza kuhubiri yule baba akaanza kumtukana akamwambia nitakukata mapanga hapa kwangu toka nakwambia yule bwana akarudi mpakani kwangu na kwa huyo mzee akaendeleea kuhubiri, akasema ametoka Tandik, hajui amefikaje lakini ametumwa kwenye hiyo nyumba huu ndio wakati muafaka muamue moja leo hii kumpokea Yesu kama bwana na mwokozi wa maisha yenu.

Yule baba akaendelea kumfwata yule kijana akaingia kwangu akiendelea kuhubiri akamtuma mtoto aje kwangu nimfukuze, nikamjibu hao ni masihi wa Mungu siwajui naweza kumfuka Yesu.

Yule bwana akuacha kulia jamani na kusema amewiwa kuomba wenye nyumba hii wampokee Yesu hawajui na hawamjui ..ila mwishoni nakumbuka akasema nikiwa kama mtumishi namasihi wa Mungu naomba niweke wazi nimenawa na ujumbe niliotumwa nimewaachia, mkipenda ufanyieni kazi.

Alintoa machozi nikaomba ale kwangu akakataa kabisa akasema ameonyeshwa huu mtaa anahitaji kuzunguka huku anahubiri, nikampa maji akanywa akaondoka na chupa nikampa alfu kumi, akasema hapana nikamwomba basi chukua hata alfu tano akakataa nikamwambia ubarikiwe mungu azidi kukutia nguvu.

Ndugu zanguni naelekea nyumban muda huu niko hapa plaza nimepigiwa na wife yule mzee amefariki muda si mrefu kisukari kimepanda gafla

Ndugu yangu pengine haitakujia nafasi kama hii kwako itakuja kwa njia nyingine, mwombe Mungu akusaidie kuuchukua ujumbe na kuufanyia kazi yule kijana ajui wala atambui kilichoteka leo mchana wanamzika jion hii; Mungu wa rehema awape rehema na uvumilivu wafiwa

Bwana ametoa .......ametwaaaaaaaaaa

Duh wana tangi bovu poleni kwa msiba. Aisee hii story yako nlitaka kuishia njiani baada ya kuona ni ya kawaida sana. Lakini kila nilivokuwa nasoma neno moja baada ya jingine ikawa inajipambanua kuwa ni ya kipekee zaidi. Aisee huyo jamaa yaonekana ni mtumishi kweli kweli yaani kakataa pesa! Sababu wenzake wanaohubiri katika mabasi hudai pesa mwisho wa mahubiri kwa njia ya sadaka. Lakini zaidi kilichonishtua ni habari ya huyo mzee aliyekataa kusikiliza neno na mwisho wa siku mauti yamemfika aisee I'm speechless.
 
Very bad news, R I P babu, hekima ya kimungu anahitajika sana kwenye maisha ya sasa maana na manabii wa uongo nao wamekuwa wengi, tunahitaji kumuomba Mungu sana atufunilie kweli yake na watu wake
 
yaani nimeuzunika sana ni jiran yangu alienipokea nikiamia mbezi beach kwa kweli imeuma mbaya sio yeye kufa bali wappi alipo sasa ndicho kinachoniuma jamani na imenikumbusha vita vyetu si ju ya damu nanyama ,nikakumbuka aliposhika lile panga alikuwa anamfwata nani akujua
anaenda kumkata YESU aliemjia kupitia kijana Mungu atusaidie nimeomba niweke hii sijui wako atakuja kwa njia gani ukamfukuza kama hivi
MUNGU atusaidie

pdidy ni kweli?aisee unajua mambo mengine sio ya kudharau hata kidogo,kwa sababu ukikubali hakuna kitakachopungua kwako
 
Alikuwa malaika au jini, mbona hata hela na chakula alikataa akanywa maji tu. Majuto ni mjukuu huja nyuma.
 
asante sana Pdidy kwa habari hii yenye mafunzo
Lakini mwenyezi mungu ni mwingi wa rehema na hutoa nafasi kwa wateule wake ya kutubu..
Huwezi jua kipindi cha mahangaiko ya maumivu ya huyu baba alitubu na kugundua kama alikosea
 
Aiseeee, pole zao kwa wafiwa, hilo tatizo wanalo wengi sana ila Mungu atusaidie kwani wakati mwingine unaweza kumfukuza malaika aliyetumwa na Mungu bila kujua kama ilivyokuwa kwa huyu mzee, ahsante sana Pdidy
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom