TL. Marandu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 3,625
- 5,810
Nikiri kuwa huko nyuma nilishawahi kuomba sana Vyama Vinavyounda Ukawa wampe Magufuli Ushirikiano, Kisha Nikaenda Mbali na Kusema Kuwa Magufuli ni Mtu Mzuri, Ila sasa Pasipo na Shaka kwa Tamko lake la Kidictator na Kinafiki sana, la Kuzuia Shughuli za Kisiasa ati mpaka baada ya Miaka mitano imenifanya Niwone Magufuli Kuwa Ni Mvunja katiba asiyejua Tofauti ya Shughuli za Siasa na Kampeni. Na Mvunja Katiba hakuna neno lingine la Kumuita hata kama tunataka kumpenda sana Kuvunja Katiba ni Uhalifu.
Tumeona Pia Magufuli akitumia Polisi, Kiharamu na Kihalifu, akiingilia sherehe, mikutano na vikao vya vyama vya upinzani kwa Visingizio vya Uwongo kama ilivyokuwa Kuzuia matangazo ya Bunge ya Moja kwa Moja ya TBC. Alipotumia Polisi Kuvamia Sherehe za wanachuo wa Chadema walidai kuwa kwanini walikuwa na sare na Bendera, lakini walipoona kuwa Hata Maafali ya CCM yalihusisha sare za chama na Bendera wakabadilisha maneno na Kusema ilikuwa ni kwa sababu ya Ugonjwa uliozuka Dodoma ingawa, mikusanyiko na sherehe za wengine ziliendelea kama kawaida.
Napenda Niwaase sana Watanzania, Msidanganyike na sijui Kutumbua majipu, sijui huduma za afya na elimu bure, Kwa asilimia 90% Magufuli ni Mnafiki wa Kutupa, Katika hili hana nia yoyote njema. Aeleze wazi Ni kwa Jinsi Gani Vikao, Sherehe, Mikutano, na Masikini hata Misiba ya Vyama vya Upinzani Vitamzuia Kufanya Kazi zake na Kutekeleza ahadi zake.
Amesema Pia na Nikamsikia Kuwa atashirikiana na Vyama vya Upinzani, Kivipi, kama haruhusu wakutane, wafanye Mikutano, au Watoe hoja Bungeni, atapata wapi mawazo yao? Atamtuma Mkewe akapate mawazo yao majumbani kwao au?
Pia Mh. Magufuli Amesema Kuwa ati hatamvumilia Mtu yeyote atakayemchelewesha,
Labda Nimuulize Maswali Kama 4,
1) Ni jinsi Gani Mazishi ya Alfonzo Mawazo yangemchelewesha Kutekeleza Ilani ya CCM?
2) Ni Kwa Jinsi Gani sherehe za Wanachuo wa Chadema kama zilivyokuwa kwa wahitimu wa CCM Zingememchelewesha Kuwawajibisha wezi wa Lugumi?
3) Ni Kwa Jinsi Gani Mkutano wa Zitto Ubungo au Mkutano wa Mbowe Mwanza Ungemchelewesha Kutoa elimu ya bure aliyoiahidi?
4) Ni Kwa Jinsi Gani TBC kutangaza matangazo ya Bunge live kunamchelewesha Kufuta Mkataba wa IPTL ambao kwa Kumtumia "Mbia hewa" ambaye hakuwa na Mtaji wowote akishirikiana na CCM waliwaibia Wananchi kwa Kulipa bili kubwa za Umeme Kiasi cha Kuwezesha hisa zao hewa zikafikia $ 75,000,000 ambazo walivuna kwa wire na pesa Taslimu za Magunia na Marumbesa. (Anitajie Mtu Mtaji wa "Mwakilishi wa Mafisadi IPTL, Uliomwezesha Kuvuna Kiasi hiki kwa niaba yao, maana aliwagawia kila mtu)
5) Ni Jinsi gani Maswali ya Tundu Lisu yanamzuia anayeshughulikia Wafanyakazi hewa ashindwe kuvunja Mikataba ya Kiwizi ya Mafuta, na Kuivunja Bank iliyotakatisha fedha za Escrow ya Stanbic, Kama Vile ilivyotaifishwa bank ya Meridian "Beyao" Bank miaka ile ya 90. Anijibu tu haya Mimi nitaona kweli ni, "Msema kweli" ha
Kama alivyosema Zitto Kabwe Mapema sana, Na Huyu Kijana Tunu na Shujaa wa Tanzania ni kama Nabii, Magufuli ni Dictator, Waliiba Urais kwa Kiburi Kikubwa kwa Kunyang'anya Computer, Wakafuta Matokeo ya Uchaguzi wa Zanzibar ambapo Maalim Seif alishinda, Walipoonda Wapinzani Wapenda amani wamekaa Kimya wakanusa Udhaifu.
Nimalize kwa Msemo usemao Mtu mwovu Ukimpa inch, hatasema asante, atachukua mile. Sasa ifike mahali Wapinzani tutathmini kama kweli tunataka kuendelea Kuwapa picha hii kuwa Sisi ni Dhaifu.
Kama Nelson Mandela, Naona kama tumefikia wakati wa Kuendelea Kukubali Kupigwa Mabomu, kudhalilishwa, Kuvunjiwa katiba juu ya Vichwa vyetu, pale ambapo tunataka Kushiriki Kwa Mujibu wa Katiba, Maswala ya Kuitumikia Jamii yetu, Kisiasa na Kiuchumi. Kama Magufuli na CCM hawataamua Kuwa na Busara na Kuitii katiba na Kujua hii ni nchi yetu sote, Watakuwa wamejidanganya sana. Na ndoto zao za Kutawala Tanzania miaka 100 kwa Nguvu na Mizengwe itageuka Jiinamizi.