Uchaguzi 2020 Nimetia nia kesho nitamkuchulia fomu ya kugombea Urais Zanzibar, Sheikh Mselem kupitia CHADEMA

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Jun 26, 2014
545
684
Nimeweka nia ya kumchukulia fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Sheikh Mselem Ali kwa tiketi ya Chadema kesho tar 20/07/2020

Sheikh Mselem Ally ana haki ya kuchaguliwa kama walivyokuwa na haki waznz wengine.

Haya ni maono yangu binafsi kama Mtanzania. Kulalamika tu pembeni bila kuchukua hatua yeyote hakutowasaidia wafungwa hawa kutoka kifungo walichofungwa bila ya kushtakiwa.

Kura zetu ndio silaha pekee ya kuwaweka Viongozi hawa HURU.

Narudia tena, haya ni maono yangu binafsi. Hata hivyo naamini maono haya yanaakisi maono ya Wazanzibar walio wengi.

Hatutaki kuathiri mchakato wa kuunganisha nguvu za vyama kushirikiana. Hata hivyo tunadhani Sheikh Mselemu Ally ni mgombea bora na anakubalika zaidi ya wagombea wote wa Urais Znz.

Pamoja na ubora alionao hata hivyo tunahitaji waznz wampigie kur ya HURUMA.

Pamoja na kuwa mchakato huu kuchukua na kurudisha fomu utafungwa rasmi kesho hata hivyo tunaamini chama kinaweza kuongeza siku walau moja zaidi ili tuweze kupata wasaa wa kuongea na vyombo vya habari kwa nia ya kuwahabarisha waznz ujio wa Sheikh Mselem ktk nyanja za siasa.

NB. Sheikh Mselemu kwasasa si mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Na Sijatumwa na mtu yyt ktk zoezi hili, Bali ni maono yangu binafsi, nikiamini yatapokelewa na znz wengi.

Baada ya mchakato huu kukamilika ndipo tutakapoenda kwa Shekh Mwenyewe kumuomba akubali ombi hili la watanzania wengi.
 
Kamchukulie uunganishwe nao (katika kuny_ _ makopo)

Usalama wa nchi yetu kwanza
 
Tatizo ni namna gani tutapigania Hawa masheikh watoke kizuizini. Fomu inaweza kuchukuliwa tu.
Mashehe wa JUMUKI au Uamsho kwa jina maarufu ni wakubaki ndani daima ili iwe fundisho kwa itikadi kali wote; wavunja amani, usalama; & wapinga muungano.
 
Pamoja na kuwa mchakato huu kuchukua na kurudisha fomu utafungwa rasmi kesho hata hivyo tunaamini chama kinaweza kuongeza siku walau moja zaidi ili tuweze kupata wasaa wa kuongea na vyombo vya habari kwa nia ya kuwahabarisha waznz ujio wa Sheikh Mselem ktk nyanja za siasa
Siku zote ulikua wapi mpaka unakuja kurupuk leo
 
Kamchukulie uunganishwe nao (katika kuny_ _ makopo)

Usalama wa nchi yetu kwanza
Hilo ndio tatizo la CCM kuona mtu mwenye mawazo yaliyo tofauti na serikali hiyo huhatarosha amani ya nchi.

Nchi hii ni yetu sote na kwa silka ya watanzania hatua RAIA au kikindi chenye kutaka kutaharisha amani ya nchi.

Matukio yanayohisiwa kutokea ni uoga usiokuwapo. Na matukio yaliyotokea huko nyuma mengi hukulikana kama FALSE FLAG ACT.
 
Umepewa hiyo ruhusa na huyo uliyemchukulia fomu? alikuwa ni mwananchama wa Chadema?
 
Niko tayari kuchangia!! ubarikiwe kiongozi!!
Naam nishafika viunga vya ofisi kuu chadema znz.

Nimeambiwa mchakato rasmi wa chama wanafungwa Leo. Hata hivyo mchakato huu ni wa ndani ya chama tu. Hivyo milango iko wazi kwa kundi lolote la jamii linaloamini linanyimwa haki kwa sababu ya muonekano wao au kwa sababu ya kabila yao, au kwa sababu ya rangi zao na wanahiso wana kura ya turufu, na wanahitaji maslahi yao yasikizwe. CHADEMA iko tayari kuwapokea na kuungana nao kwa nia ya kuondoa uovu uliopo.
 
Mashehe wa JUMUKI au Uamsho kwa jina maarufu ni wakubaki ndani daima ili iwe fundisho kwa itikadi kali wote; wavunja amani, usalama; & wapinga muungano.
Maoni yako yaweza kuwa sawa kwa mujibu wa upeo wako ila siku yakikufika au yakamfika mtu wa karibu yako usipanue domo wala kujuta. Malipo ni hapahapa duniani
 
Naam nishafika viunga vya ofisi kuu chadema znz.

Nimeambiwa mchakato rasmi wa chama wanafungwa Leo. Hata hivyo mchakato huu ni wa ndani ya chama tu. Hivyo milango iko wazi kwa kundi lolote la jamii linaloamini linanyimwa haki kwa sababu ya muonekano wao au kwa sababu ya kabila yao, au kwa sababu ya rangi zao na wanahiso wana kura ya turufu, na wanahitaji maslahi yao yasikizwe. CHADEMA iko tayari kuwapokea na kuungana nao kwa nia ya kuondoa uovu uliopo.
Kwahiyo umechukua hatua gani mkuu!!! Shukran in advance
 
Kwahiyo umechukua hatua gani mkuu!!! Shukran in advance

Stay Tune,

Tayari tumekutana na viongozi wa jamii.

Uzuri wa awamu hii tunaambiwa na viongozi wetu tumtamgulize Mungu.

Hivyo Usiku wa Leo kutakuwa na dua ya kutaka Ushauri Mungu wetu.

Vikao rasmi vitaendelea kesho tukijaaliwa
 
Back
Top Bottom