Nimetembea na ‘house Girl’ wangu na sasa ana mimba

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
213
Naitwa baba Zai wa Buguruni Dar, nimeoa na tumebahatika kupata mtoto mmoja. Kutokana na mke wangu kuwa anafanya kazi, tulilazimika kutafuta mfanyakazi wa ndani.

Mke wangu amekuwa akirudi kutoka kazini usiku sana na mimi huwa narudi nyumbani saa nane mchana. Nimejikuta muda mwingi nakuwa na mwanangu na ‘hausi geli' tu ambapo mke wangu tumekuwa tukiwa na muda mzuri wa kuvinjari siku moja tu kwa wiki.

Nisiwafishe ‘hausi geli' huyu alitokea kunipagawisha kutokana na umbile lake, sijui ni tamaa au nini lakini nikajikuta nimezama katika dimbwi la mahaba kiasi cha kufikia hatua ya kumchukulia kama mke wangu kwasababu huduma nyingi alikuwa akinipatia.

Kinachonipa wakati mgumu sasa ni kwamba, mke wangu anahisi kuwa natembea na huyu mfanyakazi wangu na kwamba ikibaini hivyo kwa ndugu jamaa na marafiki itakuwa ni aibu. Mbaya zaidi ‘hausi geli' huyo sasa anadai ana mimba yangu. Hebu naomba unishari nifanye?
 
Kwa Hiyo Umekula suria Wako.....?
Kwa Hiyo Wewe Ni king Solomon......?
Basi Lea Mwana Wa Kiuno Chako, Mpende Mkeo Mara Dufu. Na Huyo Kijakazi Asimdharau Mkeo ( Sara & Habili) .....!
Ila Mwana Wa Kijakazi Hatarithi Pamoja Na Isaka.....!
 
Mahouse girl nao wakipata soap soap na lishe nzuri hubadilika na kuanza kuvutia sana kama huwezi kuyazuia matamanio yako basi ni lazima yaliyotokea yatokee. Sasa hivi kipaumbele chako ni kuhakikisha ndoa yako haivunjiki na pia kumpa matunzo mazuri huyo binti ili ajifungue mtoto mwenye afya.
 
Baba Zai

ndio ukome kabisa ubazazi, ukipanda vitunguu unadhani uavuna nyanya. Hakuna rangi utaacha ona balahau.
 
‘hausi geli' huyu alitokea kunipagawisha kutokana na umbile lake, sijui ni tamaa au nini lakini nikajikuta nimezama katika dimbwi la mahaba kiasi cha kufikia hatua ya kumchukulia kama mke wangu kwasababu huduma nyingi alikuwa akinipatia.

...Hebu naomba unishari nifanye?


1* mtafutie makaazi mapya huyo 'mrembo', kisha umuoe.
(a bird in hand worth two in a bush...)

2* mjulishe mkeo kuhalalisha hizo zamu.
(j'3-ijumaa bi mdogo, wikiendi bi mkubwa)

Kila la heri!
 
Shy, kwanza hongera kwa kuwa uko mbioni kuwa baba kwa mara ya pili at least. Mie nakushauri utumie UZOEFU wa Shaggy na Mzee Mahita. Shaggy kwake yeye aliimba ule wimbo wa IT WASN'T ME na Mahita akautumia kwa utetezi wake. Kile kitoto kinafanana kabisa na Mahita (kama ule wimbo wa Sikinde --- jamaa kazaa na Binamu yake akidai eti ni nyama ya hamu na badaadaye binadamu kajifungua ,...Ohhh mtoto SURA YAKO). Lakini bado Mahita anadai kuwa SI WAKE. Ila tu jiandae kuitwa MTU MZIMA OVYO.
Shy, kumbuka siku nyingine kwa AFYA yako na MKEO basi ukitaka kUCHEZA ukumbuke kuvaa MADARUGA na siyo kujitupa uwanja wa FUNDI SEREMALA ukiwa pekupeku.....
 
Unajua hapo shy kwa kulinda heshima ya ndoa inabidi uweke siri kibindoni.
KIsha kama una uwezo mfanyie makeke na umpangie nyumba mbali na mkeo kusudi mburudike vizuri huko uswazi kwani umesema unarudi saa 8 mchana toka mzigoni.
KAma huwezi na hutaki huyo kijakazi akuzalie basi ni bora ukaitoa mimba ili kuepuka aibu.
 
Unajua hapo shy kwa kulinda heshima ya ndoa inabidi uweke siri kibindoni.
KIsha kama una uwezo mfanyie makeke na umpangie nyumba mbali na mkeo kusudi mburudike vizuri huko uswazi kwani umesema unarudi saa 8 mchana toka mzigoni.
KAma huwezi na hutaki huyo kijakazi akuzalie basi ni bora ukaitoa mimba ili kuepuka aibu.

Mkuu,

Haya mambo yapo na sioni haja ya kulifanya hilo jambo kuwa siri eti kulinda heshima ya ndoa yako...Nina imani ulipokuwa ukibanjuka na house girl wako bila condom ni dhahiri ulijua kitakachotokea so mzee relax,
mi nakushauri kuwa kwanza hiyo mimba wa usiitoe, pili mueleze wife hali halisi najua utashuhudia vurumai na machungu mengi lakini ni sehemu ya mchezo ukizingatia kuwa kama wife atakumwaga basi house girl achukue nafasi kwani nina imani kuwa ana viwango na ndio maana mzee ukajitoa muhanga mpaka kula mzigo bila kinga.....

Na hata huyo house girl nina imani kumpatia soap soap na mambo mengine muhimu atakuwa juu kinoma. Kwani kuwa house girl ni tatizo au ni mgawanyiko wa majukumu katika jamii tu??

Lea mimba hiyo binti akijifungua lea mtoto maisha yanaendelea hakuna cha aibu wala nini kama ulijua itakuwa aibu angalau ungevaa condom basi lakini weee ah!! ukateleza tu kama uko kitonga vile..Shabash!!!!!!!
 
Shy - Baba Zai .. you are not alone in this only that umejitangaza ... a lot of men find themselves in such situations ... especially kwakuendekeza tamaa za mwili .. its very unfair na mkeo ataumia saana .. lakini you have to tell her as the situation is up tight now ... she is prone to find out sooner or later ... the only way ni kumfahamisha mkeo that you made a mistake na mshirikiane katika kulitatuwa hili ... msichana arudishwe kwao ... take care of all mahitaji yake na akishajifungua take care of the kid .. ukimshirikisha mkeo then hiyo aibu anaeikwepa kwa ndugu haitokuwepo na stara itapatikana

Ila one thing you have to swear that this will be the first and last mistake .. asilete tena house girl mwengine halafu ukafanya vile

And next time .. dont blame your wife .. kwani unasema you only make love once in a week ... why drag her kwenye dhambi zako .. akisafiri je zaidi ya miezi miwili utafanya nini ... ukiendekeza hili hata mwanao wa kumzaa utaona halali yako ... acha tabia hizi mara moja
 
Unajua hapo shy kwa kulinda heshima ya ndoa inabidi uweke siri kibindoni.
KIsha kama una uwezo mfanyie makeke na umpangie nyumba mbali na mkeo kusudi mburudike vizuri huko uswazi kwani umesema unarudi saa 8 mchana toka mzigoni.
KAma huwezi na hutaki huyo kijakazi akuzalie basi ni bora ukaitoa mimba ili kuepuka aibu.

NO NO NO!!!!! Usitoe mimba dhambi nyingine hiyo. Ushauri wangu ni huu mpende sana huyo binti aje akuzalie mtoto mwenye afya nzuri. Ila msafirishe huyo binti kwao kisha hakikisha unampa matumizi ya kila aina au mpangie chumba mbali na hapo Buguruni.
 
Lakini swala linakuja hapa je kama kweli mke wake atakuridhia kwa yote yaliyo tokea.
Na je hamuoni kama mke naye atataka naye amlipe jamaa?
Mara nyingi vitu kama hivi iwa vinasababisha wanawake nao kutafuta jamaa wa pembeni au Serengeti boy nje.
 
NO NO NO!!!!! Usitoe mimba dhambi nyingine hiyo. Ushauri wangu ni huu mpende sana huyo binti aje akuzalie mtoto mwenye afya nzuri. Ila msafirishe huyo binti kwao kisha hakikisha unampa matumizi ya kila aina au mpangie chumba mbali na hapo Buguruni.

Baba Zai kama sijakosea dini yako inakuruhusu wake zaidi ya mmoja sasa Baba Zai hunahaja ya kutoa MIMBA wala kumsafirisha huyo mzazi mwenzio mtarajiwa. Wala usiseme ilikuwa bahati mbaya maana kama BATI ni BAYA basi Ungetumia VIGAE ama ungerudi zama za UJIMA ukatumia NYASI

Kingine Baba Zai kuna huu wimbo wa UKIMWI kila siku unaimbwa je mwenzangu RADIO na TV yako hazifanyi kazi??

Umeshamharibia binti wa watu maisha sasa Baba Zai huo ni msalaba wako ubebe hadi mwisho wa maisha yenu. Chamsingi tafuta mshenga kalipe mahari kwa binti mchezo uishe. Kumbuka kutuambie harusi lini tuje kuserebuka:)
 
[KAma huwezi na hutaki huyo kijakazi akuzalie basi ni bora ukaitoa mimba ili kuepuka aibu.[/QUOTE]

KUTOA MIMBA? KUUA? ILI USIAIBIKE? USHAURI WA AJABU HUU! KAMA MIMBA ZA NJE YA NDOA ZINGEKUWA ZINATOLEWA KULINDA HESHIMA KUNA MAJINA MAKUBWA SANA SUNGEYASIKIA KWA KUWA WALISHAUUWA KWA KUTOA MIMBA ZAO UTOTONI, EG. BILL CLINTON

MIMBA TANGU SIKU YA KWANZA INAPOTUNGWA NI BINADAMU ALIYE KAMILI.KUTOA MIMBA NI MAUAJI YA HALI YA JUU, KWA KUWA UNAUA BINADAMU ASIYEWEZA KUJITETEA.
 
Naitwa baba Zai wa Buguruni Dar, nimeoa na tumebahatika kupata mtoto mmoja. Kutokana na mke wangu kuwa anafanya kazi, tulilazimika kutafuta mfanyakazi wa ndani.

Mke wangu amekuwa akirudi kutoka kazini usiku sana na mimi huwa narudi nyumbani saa nane mchana. Nimejikuta muda mwingi nakuwa na mwanangu na ‘hausi geli’ tu ambapo mke wangu tumekuwa tukiwa na muda mzuri wa kuvinjari siku moja tu kwa wiki.

Nisiwafishe ‘hausi geli’ huyu alitokea kunipagawisha kutokana na umbile lake, sijui ni tamaa au nini lakini nikajikuta nimezama katika dimbwi la mahaba kiasi cha kufikia hatua ya kumchukulia kama mke wangu kwasababu huduma nyingi alikuwa akinipatia.

Kinachonipa wakati mgumu sasa ni kwamba, mke wangu anahisi kuwa natembea na huyu mfanyakazi wangu na kwamba ikibaini hivyo kwa ndugu jamaa na marafiki itakuwa ni aibu. Mbaya zaidi ‘hausi geli’ huyo sasa anadai ana mimba yangu. Hebu naomba unishari nifanye?

Jitundike tu, yaani jinjonge, hiyo ndio dawa pekee ya kuficha aibu ya umalaya wako.
 
Kama tungeacha ngono na kujenga nchi yetu tungekuwa mbali sana. Nafikiri hili ni kosa kubwa sana housegirl ni mtoto wewe un akili timamu na unajua hii inaweza kuwa sexual harrassment issue. GO GET FISADIS USE YOUR ENERGY THAT WAY.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom