Dakika 45 za Mhe. Mwigulu Nchemba nilisikiliza kwa umakini mkubwa na baadaye nimekubaliana naye juu ya tozo ya miamala ya simu kwa sababu zifuatazo:- (1) Alitamka wazi kuwa makato yanayoelezwa na watu kuwa ni kubwa ni upotoshaji.
Yeye alisema kama mtu atatuma mathalani Tshs.1,000,000 makato yake yatakuwa siyo zaidi ya Tshs.10,000 ambayo kwangu naona ni sawa. (2) Makusanyo haya yanaenda kugharamia ujenzi wa madarasa, vituo vya afya, Mabweni ya wasichana kwa kila Mkoa.
Kwa maelezo yake sioni ubaya wowote. Nchi inajengwa na wenye nchi hivyo kama wananchi inatupasa tujenge nchi yetu.
ANGALIZO:- Sisi kama wananchi tunataka makusanyo haya mwisho wa siku yatolewe taarifa na kazi zilizofanyika na Serikali kuonyesha kila mradi uliotekelezwa kinyume cha hapo hatutakubaliana na maelezo ya Mhe. Waziri.