Nimetapeliwa nauli na mrembo niliyekutana naye mtandaoni

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,351
40,224
Mnavyojua tena, maisha ya harakati huwa hayana mwisho. Wiki tatu zilizopita nilikuwa nachat na mrembo mmoja matata, niliyekutana naye katika mtandao mmoja wa kuonyesha sura.

Nilitokea kumpenda sana huyo binti, na tukafahamiana vizuri tu. Yeye yuko kwenye mambo ya mitindo. Tatizo yeye anaishi mkoa tofauti na niliopo mimi; nikawa nimemjulisha wikiendi ijayo tuweze kuonana, na tukawa tumeafikiana. Sasa leo asubuhi, akawa amenijulisha anataka aje kuniona; mi nikaona sawa tu hakuna shida.

Akaomba nauli, nami nikamtumia mara mbili yake. Kilichonishtua zaidi, kuwa nauli imeliwa, alianza kuniambia nitume na hela ya mafuta fulani kwa ajili ya massage, yanagharimu 50,000; nikatafakari, nikamwambia tutayanunua huku huku ukishafika.

Baada ya hapo, nikipiga simu haipokelewi, meseji hazijibiwi, w/app hajibu. Imebidi ni hitimishe tu; nauli yangu imeliwa. Ingawa angekuja ningetumia zaidi pamoja na posho ya kwake, lakini kilichoniuma zaidi ni kutokuwa muaminifu.

Wakuu, nimfanyeje huyu mkulungwa?
 
Ubahili 3:5-6 usitume nauli kwa mtu usiemjua hata Kama mmechati kwamiak mingi Kama hamjawahi onana face to face usitume.

Wewe mtu umemjulia Badoo unamtumia nauli seriously!

Unakua na uhakika gani kuwa picha zile ni zake? Kama Mimi tu nimefungua account Badoo kwa fake name nimechukua picha za jamaa mwingine toka Facebook Kama 20 ivi kwahiyo ukiperuzi unajua ndo Mimi kumbe walaa!.

Halafu Kuna midume huwa inafungua account za kike kwaajili ya maboya Kama nyinyi.
 
Mnavyojua tena, maisha ya harakati huwa hayana mwisho. Wiki tatu zilizopita nilikuwa nachat na mrembo mmoja matata, niliyekutana naye katika mtandao mmoja wa kuonyesha sura.

Nilitokea kumpenda sana huyo binti, na tukafahamiana vizuri tu. Yeye yuko kwenye mambo ya mitindo.

Tatizo yeye anaishi mkoa tofauti na niliopo mimi; nikawa nimemjulisha wikiendi ijayo tuweze kuonana, na tukawa tumeafikiana. Sasa leo asubuhi, akawa amenijulisha anataka aje kuniona; mi nikaona sawa tu hakuna shida.

Akaomba nauli, nami nikamtumia mara mbili yake. Kilichonishtua zaidi, kuwa nauli imeliwa, alianza kuniambia nitume na hela ya mafuta fulani kwa ajili ya massage, yanagharimu 50,000; nikatafakari, nikamwambia tutayanunua huku huku ukishafika.

Baada ya hapo, nikipiga simu haipokelewi, meseji hazijibiwi, w/app hajibu. Imebidi ni hitimishe tu; nauli yangu imeliwa. Ingawa angekuja ningetumia zaidi pamoja na posho ya kwake, lakini kilichoniuma zaidi ni kutokuwa muaminifu.

Wakuu, nimfanyeje huyu mkulungwa?
🤣🤣🤣 Yani katika utapeli hakuna njia inayopitwa na wakati, hii mbinu kumbe bado watu wanapigwa
 
Ameogopa picha zake kazichapa filter ila uhalisia yupo kama mfalme Zumaridi. Usije mkimbia bure.
😄😄unashida gani lkn
FB_IMG_16459835190639484.jpg

nishashika hapa sema mkuu mwenyewe number busy, sijui keshanizoom😄😄😄
 
Back
Top Bottom