Kuwa Makini: Kuna Matapeli huko Instagram wanaodai kuuza iPhone na Smart TV etc wakidai wapo Pemba au Zanzibar

mkuu pole sana hilo ni kosa kisheria, na tunaweza ita kajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu au kuaminika ka sijakosea. unaweza kwenda kituo cha polisi na ukapata msaada hakuna mwizi smart kiasi ambacho haachia ushahidi nyuma ambao utasaidia kukamatika kwakee.
 
Umeingia kwenye top ten ya watu wapumbavu na wasiojielewa duniani. Congra next week unaweza kuingia top 5
hupaswi kumdhihaki mwenzako boss, matapeli wanabuni njia mpya kila uchao kama mtu uliyestarabika ungepaswa kumpa ushauri namna ya kumsaidia ili asipigwe tena ama kuipata pesa yake na sio kama unavyofanya hapa, sidhani kama ni ustarabu ndugu yangu.

Na kama vyombo vyetu vya usalama vingekuwa makini huyu mtu angetakiwa akamatwe ili asiendelee kuwatapeli wengine
 
Kuna mmoja alikua kupatana anauza mac book air au mac book pro kwa bei nyanya kweli kweli.

Mwenyewe alikua anaonyesha yupo Iringa.

I never thought atamnasa mtu mpaka siku nikakuta uzi humu eti jamaa katapeliwa na lile andazi.

Sasa wewe mtu anakwambia yupo Znz na bado unafanya naye business ya kumtangulizia pesa huku hana established trust yoyote kwako? Na kiukweli huyo mtu hayupo Znz. Atakua tu kijiwe fulani huku huku bara akiwapigia stori jinsi alivyomkamata mjinga wake.

Anyway, a sucker is born every second.
 
Wakuu kwema..

Mambo ya online business kuna page Instagram wanauza iPhone, nikachati na muuzaji anauza simu used kutoka UK nilitaka iPhone 7+ wao wanauza 450,000 nikawaomba wakanipunguzia mpka 430,000 ijumaa ya tarehe 22 nikawatumia pesa kwa tigo pesa wakala ...mwenyewe anadai duka lipo Zanzibar simu ukisha order inakuja na boat ya mchana kwa maelezo yake.... Nilivotuma hiyo pesa aka confirm kwamba kapokea akiniahidi kwamba atanipa mamba ya mtu anaefanya delivery huku Dar ndo maongezi yakaishia hapo...kila nkimwambia anitumie hiyo namba kimya na kaniblock jamani naombeni msaada nataka niende police je kuna utaratibu gani huko kwa kesi za kutapeliwa mtandaoni....?? Naombeni muongozo karibuni

IMG_4545.jpg

Jamaa nafkir ni huyu
 
Kuna mmoja alikua kupatana anauza mac book air au mac book pro kwa bei nyanya kweli kweli.

Mwenyewe alikua anaonyesha yupo Iringa.

I never thought atamnasa mtu mpaka siku nikakuta uzi humu eti jamaa katapeliwa na lile andazi.

Sasa wewe mtu anakwambia yupo Znz na bado unafanya naye business ya kumtangulizia pesa huku hana established trust yoyote kwako? Na kiukweli huyo mtu hayupo Znz. Atakua tu kijiwe fulani huku huku bara akiwapigia stori jinsi alivyomkamata mjinga wake.

Anyway, a sucker is born every second.
nilishakutana nae sana kupatana nikawa nacheka tu kwa sababu najua bei za apple devices
 
Back
Top Bottom