Nimetapeliwa na aliyekuwa mpenzi wangu

Hajaacha ata ka boxer kake ama nguo yake apo magettoni? Tumia tamaduni kama revenge! Mtie kitu tu, maana maisha yenyewe taflani, akupigae ngumi ya jicho we mtandike ya sikio.
 
Kitu Cha msingi kwa sahiv we tafuta mume akuowe maana umri ukashipindukia 30 kwa mwanamke sisi wanaume huwa tunaogopa kuwatongoza tunawaona mashangazi labda mtutongoze wenyewe hvyo kupata mume tena inaweza kuwa ngum Kama hujui kutongoza wanaume au kumloga mmoja
 
Huyo jamaa hiyo nyumba alikuwa anajenga yeye amekudanganya tu kuwa ni mtu baki. Ukitaka kujua nenda site hamisha materials uone kama kuna mtu atalalamika. Wala hujatapeliwa bali jamaa anakuchezea akili tu. Trust me
 
Kama mtu ana nia ya kumsaidia huyu dada kazi au hifadhi kwa muda iyo 75,000 kodi afanye kwa moyo mmoja na siyo kusaidia ili amkomoe au apate lolote.

Between that pole sana binti, jipe moyo na tafuta hata kazi ya kuosha vyombo na ninakusihi usimuamini mtu yoyote kwa makubaliano ya pesa au kuwekeza.

Pambana upate mtoto na umtunze kwako.
Ukiwa mwema jaribu utafute mwema mwenzako.
Hatuna cha kukushauri kwamba utakomboa mali sababu jamaa amekutapeli tayari kuliko kumfatilia ni bora ugange kwingine kivyako.
 
weka hapa kapicha tukusaidie kumsaka....ndio wale wasemaga ""urembooo"".....3 yrs mnakulana tuu...duh...pole mdogo wangu ...wanasema mapenzi upofu...rudi kwa mama ukajipange upya....hawa ndio wanasababisha warembo wa siku hizi wanakawia kukugea nyapu....eti.. "nipe muda au bado nakutafakari""" :cool::cool:
 
Acha weeeee.

Wewe huyu huyu au mwingine.

Thread 'Gardener anatafuta kazi.' Gardener anatafuta kazi.
Post zangu almost zote nimepost on behalf.Vijana wengi baada ya kufanya kazi zangu huhitaji kuendelea kufanya kazi,nami nina limit ya vijana/staff that's why nakuja kuwatangazia huku JF na kwingineko.
Mm nimeacha kuajiriwa zaidi ya miaka 7 iliyopita.
Kwenye ajira zangu zote zilizopita nilikuwa kwenye senior position.
Sasa hivi ni Owner wa some projects.
Karibu PM kama hutajali..!
 
Habari ya saizi waungwana?? Naamini mu wazima wa afya kabisa. Bila kupoteza muda niingie kwenye maada.

Kwanza kabisa. Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa bado na mahusiano yangu yamevunjika wiki tatu zimepita na ndicho chanzo cha mkasa wangu.

Hapo nyuma wakati nipo home mama alinipa sh lak tatu nifanye biashara maana aliamini nina mkono wa biashara na kiukweli nilipoaanza kuuza sendo za kimasai zile niliuza kwa mafanikio makubwa. Tuachane na hilo.

Wakati nafanya biashara nilikutana na boyfriend ambaye tulijikuta tunapendana kweli kweli. Huyu bwana alikuwa muuza urembo. Tumedumu nae kwa muda wa miaka mitatu. Alikuwa na wivu mno hadi alivunja laini zangu na kunisajiria mbili kwa majina yake yeye.

Mwaka jana aliniambia tununue uwanja tujenge nikaona wazo zuri, akaniambia bei ya uwanja akapendekeza tuchangiane, kweli nilichangia kiasi fulani hivi tukapata uwanja. Mwaka huo huo akasema tujenge msingi, tukajenga. Na mwaka huu tulikuwa tunamalizia kuijenga.

Mimi kulingana na mtaji wangu na hela niliyotumia kujengea nyumba nikaishiwa kabisa na yeye akaniahidi kunipa mtaji mwingine tena maana alitaka tuchukue mkopo benki kwa dhamana ya nyumba mimi nikagoma kabisa.

Basi majukumu yangu yote akayavaa yeye kuanza kunilisha, kodi ya nyumba na vingine vingi maana mimi niliishiwa hela. Shida imekuja baada ya kodi kuniishia mimi nikamwomba awekee milango nyumba yetu ili mimi nihamie akasema kwa sasa hana hela, nikamwomba basi anilipie kodi sh elfu 75 tena akaanza kalenda.

Nilivyombana sanaa akawa mkali ndipo akafunguka sasa. Kumbe ile nyumba na uwanja si vyetu tena, alikuwa anamsaidia rafiki yake mwanajeshi, kwa hiyo yeye alikuwa msimamizi tu. Hela nilizokuwa natoa mimi sijui alichozifanyia na alivyoona nimekuwa mkali akakimbia na kwenda huko kusikojulikana.

Kwa hiyo nimetapeliwa na huyu bwana kwa namna hiyo. Sasa saizi mwenye nyumba kanibana ananipa vitisho vya kunitimua nami hapa sijabaki na hela. Nimesharipoti polisi kuhusu kutapeliwa na bado anatafutwa kubaini aliko.

Mwisho, naombeni msaada wa hali na mali jamani niweze kulipa kodi ya chumba sh 75,000. Na pili naomba ushauri wenu nifanyaje zaidi ili niweze kurudishiwa hela nilizotaperiwa na je siwezi kusimamisha ile nyumba kuguswa na mtu hadi kibari cha mahakama kitoke kwa maridhiano?

Naomba kuwasilisha.
Hii ni chai tu Wala sio kweli ,mtaji wa ulembo na sendo mjenge nymba Tena mwaka mmoja tu hii haipo .Pia huwez kununua kiwanja na muanze ujenzi bila kiwa na barua ya mauziano .kuwa mkweli kama una shida omba msaada usaidiwe
 
Pole sana, unaonaje ukirudi nyumbani kwa mama hadi biashara yako ikisimama tena.
Maana utasaidiwa kodi ya mwezi mmoja, na miezi inayofata itakuaje
Soma maelezo yake vizuri hii n stor katunga tu .lengo ANAHITAJI msaada Ivo kailjificha kwenye kivuli Cha utapeli
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom